Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,486
- 30,166
Siku ya Ijumaa tarehe 10 mwezi wa 4 mwaka 2015, haitasahaulika na watanzania wengi kwa kipindi kirefu kwa jinsi 'walivyohenyeshwa' na mgomo wa madereva wa vyombo mbalimbali vya usafiri kwa nchi nzima.
Ingawa kwa sasa hali ya usafiri kwenye vyombo vya usafiri imerejea katika hali ya kawaida kwa nchi nzima, lakini jambo la kutafakari kwa sasa ni kuwa tumejifunza nini kutokana na mgomo huo wa madereva?
Baada ya kusikia maelezo ya viongozi wa chama cha madereva hapa nchini, waliyoyatoa mbele ya waziri wa kazi, Gaudensia Kabaka, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar-es-salaam, Suleiman Kova na mkuu wa mkoa huo Meck Sadiki, tulichogundua wananchi wengi ni kuwa madereva wamekuwa na malalamiko yao ya muda mrefu, lakini vyombo mbalimbali ambavyo vilipaswa kushughulikia malalamiko hayo, inaonekana vilikuwa vikiyapuuzia.
Miongoni ya malalamiko yao ni kama haya yafuatayo;
1. Kutokuwa na mikataba ya kazi
2. Kutakiwa kwenda refresher course ya udereva, kwenye Chuo cha Usafirishaji kila baada ya miaka mitatu wakati wa kurenew leseni, kwa gharama ya zaidi ya shilingi 500,000 ambapoi dereva mwenyewe ndiye anayepaswa kujilipia.
3. Kero mbalimbali wanazopata njiani kutoka kwa askari wa barabarani, zikiwemo za kuonyeshewa tochi,zenye lengo tu la askari hao kuwataka pesa za rushwa.
Hata hivyo ingawa malalamiko yao yamekuwa ya muda mrefu, imeonekana kuwa yamekuwa yakipuuzwa na vyombo husika na mbaya zaidi ikatokea kuwa hao viongozi wakaswekwa ndani na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuwatisha madereva wengine wasalimu amri mpango wao wa kulalamikia manyanyaso mengi wanayopata wakiwa njiani safarini.
Jaribu kuimagine mmiliki anampa Dereva basi la thamani la zaidi ya shilingi milioni 700, ambapo hana mkataba wa ajira, na badala yake anafanya kazi kama kibarua, kwa kuwa halipwi mshahara mwisho wa mwezi, badala yake anapewa tu posho ya siku 1 kila anapolifikisha basi hilo mwisho wa safari yake.
Jaribu tena kuimagine dereva huyo anapatiwa shilingi elfu 30 tu kila anapolifikisha basi hilo kituo cha mwisho, ikiwa na maana pesa hizo licha ya kulipia malazi na chakula awapo njiani, lakini pia anapaswa kutuma pesa kwa familia yake alioiacha nyumbani kwake.
Si hivyo tu tumeelezwa pia na viongozi hao wa chama cha wafanyakazi wa madereva kuwa usalama wa ajira yao hiyo ya udereva ni ndogo mno, kiasi ambacho unaweza ukakuta dereva ameondoka na basi Ubungo akiwa anaelekea Mbeya na anapofika Morogoro tu, anakuta ujumbe kwa wakala wa basi hilo, ambao amepewa na mmiliki wa basi hilo kuwa funguo za basi hilo anapaswa apewe dereva mwingine atakayekuwa ameandaliwa na mmiliki wa basi hilo, ili aendelee na basi hilo hadi mwisho wa safari yake huko Mbeya.
Wakati dereva huyo akiachishwa kazi 'kienyeji' kiasi hicho, hata mafao yake ya kuachishwa kazi kwa mujibu wa sheria za kazi za nchi yetu nayo ananyimwa!
Kutokana na hali hiyo ambayo madereva wengi wanajiona wanafanya kazi hizo za madereva kama 'madeiwaka' ndiyo wakati mwingine huwa inanasababisha ajali barabarani kutokana na hizo frustrations za kazi na kukosa morali wa kazi kwa madereva hao.
Kwa hiyo ni vyema kwa sasa wamiliki wa mabasi hayo wawe wamepata fundisho kuwa hawapaswi kuwatreat madereva wao wa mabasi kama vyombo tu vya kuendelea kuwazalishia wao wamiliki utajiri wa kupindukia, bila kuwathamini watu hao wanaowazalishia utajiri huo wanaoupata.
Kwa upande wa viongozi wetu wa serikali nao wanapaswa kutopuuzia malalamiko mbalimbali wanayopata kutoka kwa wafanyakazi mbalimbali wa sekta mbalimbali hapa nchini, kwa mtazamo tu kuwa kazi hizo zinazofanywa na hayo makundi mengine, hazina umuhimu sana kwenye jamii, ukilinganisha na kazi wanazoziona wao kuwa na umuhimu mkubwa kama za uanasiasa na za utawala kwenye serikali yetu.
Hata hivyo hao hao wanasiasa na watawala wetu wa serikali, walishuhudia wenyewe jinsi nchi ilivyotikisika kwa masaa hayo manane tu ambayo madereva waligoma, kiasi cha wao wenyewe kusalimu amri na kuamua kuyatekeleza madai yote yaliyotolewa na madereva!