Mgomo wa madereva unatufundisha nini?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Siku ya Ijumaa tarehe 10 mwezi wa 4 mwaka 2015, haitasahaulika na watanzania wengi kwa kipindi kirefu kwa jinsi 'walivyohenyeshwa' na mgomo wa madereva wa vyombo mbalimbali vya usafiri kwa nchi nzima.

Ingawa kwa sasa hali ya usafiri kwenye vyombo vya usafiri imerejea katika hali ya kawaida kwa nchi nzima, lakini jambo la kutafakari kwa sasa ni kuwa tumejifunza nini kutokana na mgomo huo wa madereva?

Baada ya kusikia maelezo ya viongozi wa chama cha madereva hapa nchini, waliyoyatoa mbele ya waziri wa kazi, Gaudensia Kabaka, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar-es-salaam, Suleiman Kova na mkuu wa mkoa huo Meck Sadiki, tulichogundua wananchi wengi ni kuwa madereva wamekuwa na malalamiko yao ya muda mrefu, lakini vyombo mbalimbali ambavyo vilipaswa kushughulikia malalamiko hayo, inaonekana vilikuwa vikiyapuuzia.

Miongoni ya malalamiko yao ni kama haya yafuatayo;
1. Kutokuwa na mikataba ya kazi
2. Kutakiwa kwenda refresher course ya udereva, kwenye Chuo cha Usafirishaji kila baada ya miaka mitatu wakati wa kurenew leseni, kwa gharama ya zaidi ya shilingi 500,000 ambapoi dereva mwenyewe ndiye anayepaswa kujilipia.
3. Kero mbalimbali wanazopata njiani kutoka kwa askari wa barabarani, zikiwemo za kuonyeshewa tochi,zenye lengo tu la askari hao kuwataka pesa za rushwa.

Hata hivyo ingawa malalamiko yao yamekuwa ya muda mrefu, imeonekana kuwa yamekuwa yakipuuzwa na vyombo husika na mbaya zaidi ikatokea kuwa hao viongozi wakaswekwa ndani na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuwatisha madereva wengine wasalimu amri mpango wao wa kulalamikia manyanyaso mengi wanayopata wakiwa njiani safarini.

Jaribu kuimagine mmiliki anampa Dereva basi la thamani la zaidi ya shilingi milioni 700, ambapo hana mkataba wa ajira, na badala yake anafanya kazi kama kibarua, kwa kuwa halipwi mshahara mwisho wa mwezi, badala yake anapewa tu posho ya siku 1 kila anapolifikisha basi hilo mwisho wa safari yake.

Jaribu tena kuimagine dereva huyo anapatiwa shilingi elfu 30 tu kila anapolifikisha basi hilo kituo cha mwisho, ikiwa na maana pesa hizo licha ya kulipia malazi na chakula awapo njiani, lakini pia anapaswa kutuma pesa kwa familia yake alioiacha nyumbani kwake.

Si hivyo tu tumeelezwa pia na viongozi hao wa chama cha wafanyakazi wa madereva kuwa usalama wa ajira yao hiyo ya udereva ni ndogo mno, kiasi ambacho unaweza ukakuta dereva ameondoka na basi Ubungo akiwa anaelekea Mbeya na anapofika Morogoro tu, anakuta ujumbe kwa wakala wa basi hilo, ambao amepewa na mmiliki wa basi hilo kuwa funguo za basi hilo anapaswa apewe dereva mwingine atakayekuwa ameandaliwa na mmiliki wa basi hilo, ili aendelee na basi hilo hadi mwisho wa safari yake huko Mbeya.

Wakati dereva huyo akiachishwa kazi 'kienyeji' kiasi hicho, hata mafao yake ya kuachishwa kazi kwa mujibu wa sheria za kazi za nchi yetu nayo ananyimwa!

Kutokana na hali hiyo ambayo madereva wengi wanajiona wanafanya kazi hizo za madereva kama 'madeiwaka' ndiyo wakati mwingine huwa inanasababisha ajali barabarani kutokana na hizo frustrations za kazi na kukosa morali wa kazi kwa madereva hao.

Kwa hiyo ni vyema kwa sasa wamiliki wa mabasi hayo wawe wamepata fundisho kuwa hawapaswi kuwatreat madereva wao wa mabasi kama vyombo tu vya kuendelea kuwazalishia wao wamiliki utajiri wa kupindukia, bila kuwathamini watu hao wanaowazalishia utajiri huo wanaoupata.

Kwa upande wa viongozi wetu wa serikali nao wanapaswa kutopuuzia malalamiko mbalimbali wanayopata kutoka kwa wafanyakazi mbalimbali wa sekta mbalimbali hapa nchini, kwa mtazamo tu kuwa kazi hizo zinazofanywa na hayo makundi mengine, hazina umuhimu sana kwenye jamii, ukilinganisha na kazi wanazoziona wao kuwa na umuhimu mkubwa kama za uanasiasa na za utawala kwenye serikali yetu.

Hata hivyo hao hao wanasiasa na watawala wetu wa serikali, walishuhudia wenyewe jinsi nchi ilivyotikisika kwa masaa hayo manane tu ambayo madereva waligoma, kiasi cha wao wenyewe kusalimu amri na kuamua kuyatekeleza madai yote yaliyotolewa na madereva!
 
Kwanza niweke sawa hapo.
Lengo la Tochi sio rushwa,lazima ujue kutofautisha vituviwili.
Najua point yake ina lenga na kuelekea wapi.

Hapa tatizo kubwa ni moja tu,ambalo ni mikataba.
Mikataba ya Muajiri na muajiriwa ikiwa sawa hata hili la kusoma wala halina tatizo.
Refresher kozi ni muhim kwa kasi ya dunia inavyokwenda,na wala madereva hawajagoma kusoma.Ila wametaka utaratibu ufuatwe.
Maana muda ambao unaenda kusoma huku gari anapewa mwingine na ukirudi bosi hadi akufikirie.
Suala lililofanya serikali kuripua zaidi hili ni wakati mgogoro wa muda mrefu wa Ajira zao ziwe rasmi,wao wakaingiza issue ya kusoma.
Hapo ndio watu wakaona hapa sasa wanazidi kutuchanganya na wao madereva wakalianzisha.
Natumai kwa somo hilo watu watajua wafanya nini.
Pia tutambue kwamba waajiri hili suala nalo wamekuwa wakitupa mpira.Maana wengi ni timua timua madereva,sasa wanajua wakiingia mkataba Drivers watakuwa wanahaki ya kudai fidia.
Ukitaka kujua hawa wamiliki wanaangalia sana pesa,subiri Driver aumwe,pale kuna ma drivers hata misiba ya ndugu zao hawaendi kwa kuhofia vibarua vyao.Halafu hao hao ndio wabeba hirizi za mabosi wao.
 
sitaongelea hao wa mikoani, ila hawa wa dsm, mimi walinifurahisha sana manake daladala zilipofutika barabarani, nilikanyaga mafuta toka mbezi luis hadi posta bila kusimama. nikajifunza kumbe haya madaladala ndio yanatuletea foleni hapa dsm mwezi wa sita wayafute yote tubaki na dart, halafu watu tufike posta toka mbezi kwa dakika 20 badala ya masaa matatu.
 
Funzo kubwa ambalo ata miaka ya nyuma niliandika ni kuwa vitu muhimu kama vituo vya mafuta,Mabasi ya usafiri nk ni lazima vimilikiwe na serikali(siyo kwa asilimia 100),ukishaachia sekta muhimu kama hii 100% kwa wananchi ni tatizo kubwa sana hasa wanapoamua kugoma,mwendo wa ajabu na kupandisha nauli ni vigumu sana kuwazuia(kumbuka pia mgomo wa vituo vya mafuta ulivyoendesha nchi !!!!!.

Uliona jana ata Kova alivyokuwa mpole mpaka anasema ataondoa Tochi barabarani(nilishtuka sana!!!). Leo hii sehemu kama U.A.E mpaka Taxi zipo za serikali,vituo vya mafuta nk.

Siku moja nilimsikia muheshimiwa mmoja akisema wananchi unganeni na mlete mabasi ya mwendokasi kwa Dar es salaam ni wazo zuri lakini Serikali pia wanatakiwa kuagiza mabasi yao,kama wakiachia 100% kwa matajiri wachache itakuwa tabu kubwa sana mbeleni....
 
Ukiachia kila kitu kifanyw na private sector kwa 100% ktk nchi na serikali ikakaa kusubiri kodi basi tuw tayr kuyapokea yalotokea ulaya na marekani miaka ya 1929-1933
 
Funzo kubwa ambalo ata miaka ya nyuma niliandika ni kuwa vitu muhimu kama vituo vya mafuta,Mabasi ya usafiri nk ni lazima vimilikiwe na serikali(siyo kwa asilimia 100),ukishaachia sekta muhimu kama hii 100% kwa wananchi ni tatizo kubwa sana hasa wanapoamua kugoma,mwendo wa ajabu na kupandisha nauli ni vigumu sana kuwazuia(kumbuka pia mgomo wa vituo vya mafuta ulivyoendesha nchi !!!!!.

Uliona jana ata Kova alivyokuwa mpole mpaka anasema ataondoa Tochi barabarani(nilishtuka sana!!!). Leo hii sehemu kama U.A.E mpaka Taxi zipo za serikali,vituo vya mafuta nk.

Siku moja nilimsikia muheshimiwa mmoja akisema wananchi unganeni na mlete mabasi ya mwendokasi kwa Dar es salaam ni wazo zuri lakini Serikali pia wanatakiwa kuagiza mabasi yao,kama wakiachia 100% kwa matajiri wachache itakuwa tabu kubwa sana mbeleni....


Mkuu mtazamo mzuri sana lakini tuko miaka hamsini nyuma.
Ndoto hii ni mgumu kuifikia kama Serikali yenyewe ni hii ya CCM.

Kweli Kampuni/taasisi ya Umma ndogo kama UDA inauzwa tena kiufisadi badala ya kuipanua unafikiri huko unakosema tutafika lini
.



  1. [h=3]Wabunge waja juu, wahoji uuzwaji wa hisa UDA - Mwananchi[/h]May 16, 2014 - “Bodi ya wakurugenzi wa UDA iliendelea na uuzaji wa hisa bila kupata kibali cha Serikali na hata CHC,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.



  2. [h=3]Raia Mwema | UDA[/h]
    Kashfa ya UDA ina mizizi ya 'ukada wa CCM' ... ya madaraka pamoja na kuisababishia hasara Serikali wakati wa mchakato wa uuzaji wa shirika la UDA.





CCM-inaanza kuniingia kidogo kidogo kirefu hiki cha mtaani cha Chukua Chako Mapema.

Yako mengi na ukiamua kuorodhesha unaweza kudondoka na kupata presha Bure.
Maisha Bora kwa Kila Mtanzania.
 
Ukitaka ccm iondoke madarakani vitokee hivi;
(1)maji na umeme vikosekane week moja kabla ya siku ya kupiga kura,
(2)madereva,madaktari na walimu wagome week moja kabla ya siku ya kuvote..
Hapo watu watakuwa na hasira sana na hawatachagua ccm ng'oo
 
hata serikalini- kwenye wizara, madereva wengi ni vibarua: nao waajiriwe kuonesha mfano wa wamiliki wa magari
 
Nawaunga mkono hao madereva na ktk hilo tumepata picha nzuri sana, tunaelekea kwa wananchi, hapo ndipo mtajua nguvu ya raia.
 
hata serikalini- kwenye wizara, madereva wengi ni vibarua: nao waajiriwe kuonesha mfano wa wamiliki wa magari
Nakuunga mkono kwa asilimia 100, kama watawala wetu wanataka madereva wa mabasi wakasome, basi waanze kwanza na madereva wa STK, na wawape na mikataba ya ajira mizuri.
 
Wamethibitisha tu kile tunachokijua "umoja ni nguvu"! Madaktari, waalimu, etc. huwa wanajaribu lakini wao huwa wanagawanyika kirahisi.
 
Wamethibitisha tu kile tunachokijua "umoja ni nguvu"! Madaktari, waalimu, etc. huwa wanajaribu lakini wao huwa wanagawanyika kirahisi.
Siyo kwamba huwa wanagawanyika kirahisi, bali huwa 'wanagawanywa' kirahisi na watawala!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Inadhihirisha kwamba kila kada ni muhimu katika uchumi wa nchi hata wakiwa hawajasoma. Itakuwaje maendesha mikokoteni wote nchini wakigoma? Baamedi wote nchini wakigoma kutaka maslahi bora kazini itakuwaje?
 
Back
Top Bottom