Mgomo wa madaktari wa kigeni wanukia... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari wa kigeni wanukia...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chal, Jul 1, 2012.

 1. C

  Chal Senior Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wakuu!
  kuna tetesi zimezagaa mtaani na humu jamvini kuwa serikali ina mpango wa kuleta madaktari kutoka nje ya nchi, hasa nchi ya Irani ikitajwa zaidi. Hawa ni madaktari wa kigeni ambao kama mpango huo utafanikiwa watakuja nchini ili kunusuru sekta ya afya.

  kwa maoni yangu ujio wa madaktari hawa (kama ni kweli wataletwa) utapelekea mgomo mwingine mkubwa zaidi katika sekta ya afya kuwahi kutokea. Mgomo huu ambao sasa utaratibiwa na kutekelezwa na madaktari wa kigeni utakuwa kwa sababu zifuatazo.

  Kwanza, madaktari wa kigeni watagoma kutokana na kuwako kwa vifaa duni vya kutolea tiba katika hospitali za umma hapa nchini ikiwamo hosp ya taifa muhimbili. Hili ni miongoni mwa mambo ambayo madaktari wazalendo wamekuwa wakilililia kila mara.

  Madaktari wa kigeni watagoma wakihitaji viletwe vifaa vya kisasa katika hosp watakazopelekwa ili kuendana na ujuzi na taaluma zao jambo litakalowawezesha kutoa tiba stahiki kwa wagonjwa.

  Suala la mishahara na posho za madaktari wapya (wa kigeni) litazua mjadala mzito zaidi kwani malipo kwa madaktari hao ni mara tatu zaidi ya yale ya madaktari wazalendo. Serikali itashindwa kuwalipa madaktari hawa kwani kwa maelezo yake ni kuwa haina fedha na kulingana na huko inapotarajiwa kuwaleta (Irani) kuna uwezekano wakajitoa muhanga pale muhimbili na kwingineko.

  Madaktari wa kigeni pia watagoma ili serikali ipeleke vitanda kwa ajili ya wagonjwa mahospitalini ili wagonjwa wasilale chini ama wawili wawili wodini hii ikiwa sambamba na kuhakikisha kuwa zipo dawa na vifaa tiba vya kutosha mahospitalini ili waweze kutoa huduma kwa wagonjwa.

  Hivyo basi suala la kuleta madaktari wa kigeni linaweza lisiwe suluhisho la mgomo wa madaktari iwapo mazingira ya kufanyia kazi na maslahi kwa madaktari hayataboreshwa! Serikali iliwahi kukiri kupitia waziri mkuu kuwa madai ya madaktari ni ya msingi nashauri msingi huo pia uzingatiwe katika majadiliano ili kufikiwe muafaka

  Serikali isitafute njia ya mkato kulishughulikia hili....
  kwani tatizo haliwezi kutatuliwa kwa kuliahirisha au kulikimbia...
   
 2. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Serikali itaabika!
   
 3. N

  Nambombe Senior Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha tuone mwisho wake
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kingine lugha, hao madaktari wa iran isije kuwa kama wachina na wajapan wanatumia lugha zao sasa wakija hapa kiarabu tutaweza? Watalala wapi, watafikaje hospitali ili hali ni wageni kabisa. Hata kama hawatalipwa lakini bado utata upo.
   
 5. C

  Chal Senior Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hapo kwenye lugha umenena kabisa, itabidi wagome wapelekwe swahili course ya mwaka mmoja ndiyo waje watoe huduma
   
 6. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Kuna faida gani ya kuwepo kwa madaktari wazawa wasiomthamini mgonjwa na wanaogoma kila baada ya mawiki kadhaa?
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Serikali legelege, rais daifu
   
 8. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  mkuu hiyo ni tathimini, na iko dhaifu sana. Suala kuu ni madai. upepo ukoje, kama maoni vile
   
 9. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Umefanya nimecheka sana hapo kwenye blue, wenzetu huwa hawatanii bado kazi ipo!
   
 10. Mbutunanga

  Mbutunanga Senior Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na migomo itaendelea kuwepo as long as the root problem haiondolewi bali kufunikwa. Kila huo mzizi unapokuwa mkubwa lazima mgomo( halafu mnafukia tena), yaani tutaenda hivyo mpaka ifikie kipindi muone solution si kuufukia bali kuung'oa.


  Chezea Mungu ya Ulimboka weye!
   
 11. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  ng'wanakidiku mkuu,
  kwanza hao magaidi wairan wakija mimi nitaishangaa sana sirkali yetu. wairan mfumo wao wa elimu toka vidudu hadi chuo kikuu ni kwa lugha yao ya taifa iitwayo Farsi au twaweza kuihta kiajemi. in that case ht hao madoc wao watakao kuja watakuwa wanaongea lugha hiyo. itabidi sirkali sikivu iajiri wakalimani kwa kila doc as per idadi ya madoc watakaokuja.

  swali ni kwamba, watz wangapi wanajua lugha yd kiajemi ili waajiliwe km translators? hata km wangekuwapo gharama ya kuwaajili nani atalipa?
   
 12. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duuu sasa hela zitatoka wapi wakati wanadai serikali haina hela????au ni project mpya ya ufisadi????
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  Wanatapatapa tu hawa na huku wakionyesha uwezo wao finyu katika kutatua matatizo mbali mbali yanayohusu nchi yetu. Sasa wanathubutu hata kudanganya eti madaktari 1,000 watakaoingia nchini hawatalipwa chochote!!! Pumbavu kabisa!!!
   
 14. m

  massai JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Akili ndogo kuongoza akili kubwa,kweli serekali legelege huzaa viongozi legelege,dhaifu,liwalo na liwe.
   
 15. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hapo ndio umuhimu wa kwenda Madrasa utaonekana maana waliopitia huko hawatapata shida kuwasiliana na madaktari toka Iran. Let's wait and see
   
 16. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huu ni umbeya/uongo. Huyu sijui anapata/anatoa wapi habari zake?.
   
 17. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,943
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  nikimaliza tu chuo, natimkia botswana..... huku longolongo tu
   
 18. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna faida gani kuwa na serikali dhaifu iliyoahidi kuboreshwa huduma za afya tena kwa kodi zetu kushindwa kutimiza hayo?
   
 19. Ngofilo

  Ngofilo JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wakuu hivi hao madoctor wa kiiran watacommunicate vipi bibi yangu ngw'ana mpandji wa hapa kisesa mwanza?manake nasubiri tu waanze kazi nimpeleke kwa ajil ya clinic yake ya moyo.tatizo bibi anapenda kueleza matatizo yake straight kwa doctor..cjui itakuwaje make bibi hataki upambe especially anapokuwa antaka kuongea na doctor yani hataki ukalimani..........nawasilisha
   
 20. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umuhim wa madrasa hapo haupo, kumbuka Iran(Persia) si waarabu, ni waajemi, wanaongea kiajemi/farsi.
  Watakuwa wanalipwa na Rostam, ni ndugu yao.
   
Loading...