Mgomo wa EFDs: Kilichopo nyuma ya pazia. Serikali isimame IMARA

Umeona eeh!
Wafanyakazi wanalipa kodi kubwa kuliko mtu mwingine yoyote, tena unailipa kabla hata hujapokea huo mshahara. Mfanyakzai huyo huyo akija mtaani anaendelea kulipa kodi kwa kila huduma anayohitaji, wao wafanyabiashara walipe kodi tuwaache longo longo

Mkuu tuungane na serikali katika hili, hawa wafanyabiashara wanataka ku Blackmail serikali kwa maslahi yao binafsi. Lazima walipe kodi, mbona wafanyakazi wanakatwa juu kwa juu na hawajawahi kugoma na kodi wanayolipa ni kubwa kwa asilimia kuliko za wafanyabiashara
 
Mleta mada naona umezungumzia jambo moja tu la wafanyabiashara kugomea mashine ama kulipa kodi. Tatizo sio kodi kama ulivyodai wewe Mwanza wana kero nyingi ambazo zimepelekea mgomo huo kutokea, kuna kero zinazohusu maofisa wa TRA na kero za jiji, na hili la mashine ikiwa ni mojawapo na iliyobeba kero zote. Wewe unadhani ni sahihi kununua mashine hiyo kwa Tsh.800,000/ service 60,000/ kuna rim page moja yenye receipt 6 tu sh.2000/ na ukikosea kidogo tu receipt moja faini kuanzia 1,500,000 - 5,000,000/ (ikifikia hapa kuna majadiliano ya kulipia pesa hiyo hotelini/bar hii ndio ijengayo sijui) usisahau wino siuji sh. ngapi vile. Wacha wagome kwani tuumio ni sisi end user.
 
Hakika tunatakiwa kuiunga mkono serikali isirudi nyuma katika hili la mashine za efd.Pengine wapunguze tu ama wafanyabiashara wakopeshwe na malipo yake yajumuishwe kwenye kodi.Hatuwezi kuvumilia biashara za ujanja ujanja na dili nyingi wakati taifa linakosa kodi.Tena TRA wanapaswa kuchunguzwa kwani mimi pia nilipokuwa naenda kulipa kodi nikauliza kidogo kuhusu hizo mashine mtu mmoja hapo tra alinitisha sana kuhusu mashine hizo huku akiniambia wala nisizishobokee!sasa unadhani kama mtu aliyepaswa kutoa elimu ya umuhimu wa efds badala yake anakatisha watu tamaa,nini kitaendelea kama si migomo?Watu wa tiss mpo?ishaurini serikali vizuri maana huko ndio kuna wabaya wake na sio CDM kama mlivyokariri

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Umeona eeh!
Wafanyakazi wanalipa kodi kubwa kuliko mtu mwingine yoyote, tena unailipa kabla hata hujapokea huo mshahara. Mfanyakzai huyo huyo akija mtaani anaendelea kulipa kodi kwa kila huduma anayohitaji, wao wafanyabiashara walipe kodi tuwaache longo longo

samahani mkuu naomba nikuulize na wewe pia,uko sober kweli mkuu?
 
View attachment 129543
Jana wafanyabiashara wa Mwanza walianza kile wanachokiita Mgomo usio na Kikomo kugomea mashine za kutunza kumbukumbu za mauzo na kukadiria ushuru zijulikanazo kama EFD. Pia siku za nyuma tulisikia mgomo wa aina hiyo hiyo Dar na Mbeya. Sababu wanayotumia ni ya msingi sana kuwa hawawezi kununua mashine hizo kwa bei ya shilingi laki nane (800,000=) tena kwa makampuni maalum wakati mashine hizo China zinauzwa dola 50 tu (kama 80,000 za kitanzania) na Kenya ziko madukani kwa retail price ya 150,000Tshs. Hapo TRA inastahili lawama kwa kutumia mfumo CCM ambao kila kunapokuwa na bidhaa mpya watu wanakimbilia kupiga dili, ilitokea kwenye Speed Governer, Plate namba za magari na hata kwenye mikanda usalama ya mabasi. Hapa kuna makandokando yanaoonesha kuna dili inapigwa TRA ndo maana hawataki Biashara huria ya EFD wao kazi yao iwe Calibration tu ya mashine. Pia mashine hizi za bei mbaya pia zinaharibika haraka na wao wateule wanouza wamejipa na dili la kufanya maintenance kwa shilingi kuanzia elfu sitini (60,000) na kuendelea, wakati kiuasilia hizi mashine ni kama Calculator ya kawaida iliyoongezewa akili kidogo tu hivyo hazina gharama kubwa kihivyo kutengeneza. Kumbuka wengine tukipeleka gari garage za ushwahilini kufanya service huwa tunalipa elfu kumi, iweje mashine hizi service au maintenance iwe elfu sitini na kuendelea. Hapo TRA jitazameni, hiyo ni hoja ya wafanyabiashara

Ukweli halisi ni kuwa wafanyabiashara wanachogomea ni KULIPA KODI kwa kuwa hizi mashine zinatunza kumbukumbu vizuri na zinazuia kila aina ya Magumashi ambayo ndio msingi wa biashara nyingi Tanzania. Wakati wa uhamasishaji wa mgomo wa Mwanza, tulielezwa na wachochezi wa huo mgomo kuwa kama zikitumika hizi mashine wafanyabiashara wengi watafilisika kwa maana toka zimeanza kutumika hizi mashine wengi wanalipa kodi kubwa kuliko zamani. Kwa kuwa utamaduni wetu watanzania sio kulipa kodi na serikali haisimamii kisawasawa masuala ya ulipaji kodi (Sijawahi kusikia mtanzania amefungwa kwa kukwepa kodi) wafanyabiashara wameamua kusimama imara kuibabaisha serikali hadi ilegeze uzi tubakie na mfumo wa zamani wa kukwepa kodi. Pia jana simu za pongezi kutoka mikoa mingine zilipigwa kwa wafanyabiashara wa Mwanza kuwa wakaze uzi, wawe ngangari. Pia baadhi ya maafisa wa TRA walikuwa wanahamasisha kichinichini huu mgomo kwa vile matumizi ya hizi mashine yanawanyima ile dili yao iliwafanya wajenge magorofa ya KUKADIRIA KODI. Kwa hiyo kinachopingwa kwenye huu mgomo sio bei ya mashine za EFD, bali ni matumizi ya EFD ili kuendeleza utamaduni wa kukwepa kodi. Bei ni kisingizio tu, nashauri serikali iwanunulie iwape bure kwani itarudisha tu hela zake, ingawa huku Mwanza hata za bure hawataki kama picha hapo juu inavyoonesha

Katika nchi ambayo zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wake hawalipi kodi, ni ndoto kuwa na miundombinu bora, elimu bora, afya bora na huduma zingine. Mama zetu wanalala wanne kitanda kimoja wakati wa kujifungua kwa kuwa pamoja na utawala mbovu wa CCM lakini pia wameshindwa kupata TAX BASE kubwa. Kama chini ya asilimia 20 ya wananchi ndio wanalipa kodi ina maana hao 80% wanatunzwa na hao 20%. Serikali inatakiwa kusimama imara kwenye huu mgogoro kwani matumizi ya EFD ndio future ya biashara Tanzania. Kwa sasa ukwepaji kodi ndio Competitive Advantage ya biashara nyingi, ili upate faida kubwa zaidi lazima uwakwepe/uwahonge TRA usilipe kodi ili uuze bei rahisi, wakati umefika serikali kuwa imara. Waacheni wafanyabiashara wafunge maduka hadi panya wamalize bidhaa za dukani, njaa zikiwauma watafungua tu. Pia ulinzi uimarishwe kwa wafanyabiashara walio tayari kulipa kodi na kutumia EFD kwa kuwa zinazuia kuibiwa pia.

View attachment 129539

Wewe ndio umefilisika kabisa kimawazo je unaweza kutuambia kwa kodi inayolipwa hivi sasa ni kiasi gani kinarudi kwa mwananchi na kiasi gani kinaingia mifukoni mwa watu au kuwekwa uswiss kwenye mabenki? kuna uhakika gani ongezeko la kodi linalosakwa halitaingia mifukoni mwa watu lote au kutumika kuibulia EPA nyingine kwa ajili ya uchaguzi? ishu sio kukusanya ishu ni zinatumikaje? Tatizo lingine ni kwamba Tanzania ina kodi nyingi mno na kubwa na hakuna mfanyabiashara yoyote anayeweza kuzilipa kiuhalali bila kuuwa mtaji na kufilisika; sasa swali ni nani alibuni hii mifumo ya kodi isyofaa ili kushinikiza watu wategemee rushwa na ukwepaji kodi? kwanini walipaji kodi wakubwa ni walalahoi wakati makampuni makubwa ya kifisadi yanasamehewa na kukwepa kodi bila kuhojiwa? badala ya kumuinua mwananchi aliyeuza thamani zake za ndani afanye biashara wakati serikali imemnyima ajira na elimu ni serikali hiyohiyo imeweka mbele kumkandamiza. Kwa vyovyote siungi mkono migomo lakini ni muhimu kuliangalia jambo hili kwa uzito unaostahili na si kulisemea kishabiki.
 
Umeona eeh!
Wafanyakazi wanalipa kodi kubwa kuliko mtu mwingine yoyote, tena unailipa kabla hata hujapokea huo mshahara. Mfanyakzai huyo huyo akija mtaani anaendelea kulipa kodi kwa kila huduma anayohitaji, wao wafanyabiashara walipe kodi tuwaache longo longo

na ni nyie nyie mnaongoza kwa kula rushwa!!
 
  • Thanks
Reactions: ram
Serikali isimame imara kama ilivyosimama imara wakati wa kuhamia digitali.
 
View attachment 129543
jana wafanyabiashara wa mwanza walianza kile wanachokiita mgomo usio na kikomo kugomea mashine za kutunza kumbukumbu za mauzo na kukadiria ushuru zijulikanazo kama efd. Pia siku za nyuma tulisikia mgomo wa aina hiyo hiyo dar na mbeya. Sababu wanayotumia ni ya msingi sana kuwa hawawezi kununua mashine hizo kwa bei ya shilingi laki nane (800,000=) tena kwa makampuni maalum wakati mashine hizo china zinauzwa dola 50 tu (kama 80,000 za kitanzania) na kenya ziko madukani kwa retail price ya 150,000tshs. Hapo tra inastahili lawama kwa kutumia mfumo ccm ambao kila kunapokuwa na bidhaa mpya watu wanakimbilia kupiga dili, ilitokea kwenye speed governer, plate namba za magari na hata kwenye mikanda usalama ya mabasi. Hapa kuna makandokando yanaoonesha kuna dili inapigwa tra ndo maana hawataki biashara huria ya efd wao kazi yao iwe calibration tu ya mashine. Pia mashine hizi za bei mbaya pia zinaharibika haraka na wao wateule wanouza wamejipa na dili la kufanya maintenance kwa shilingi kuanzia elfu sitini (60,000) na kuendelea, wakati kiuasilia hizi mashine ni kama calculator ya kawaida iliyoongezewa akili kidogo tu hivyo hazina gharama kubwa kihivyo kutengeneza. Kumbuka wengine tukipeleka gari garage za ushwahilini kufanya service huwa tunalipa elfu kumi, iweje mashine hizi service au maintenance iwe elfu sitini na kuendelea. Hapo tra jitazameni, hiyo ni hoja ya wafanyabiashara

ukweli halisi ni kuwa wafanyabiashara wanachogomea ni kulipa kodi kwa kuwa hizi mashine zinatunza kumbukumbu vizuri na zinazuia kila aina ya magumashi ambayo ndio msingi wa biashara nyingi tanzania. Wakati wa uhamasishaji wa mgomo wa mwanza, tulielezwa na wachochezi wa huo mgomo kuwa kama zikitumika hizi mashine wafanyabiashara wengi watafilisika kwa maana toka zimeanza kutumika hizi mashine wengi wanalipa kodi kubwa kuliko zamani. kwa kuwa utamaduni wetu watanzania sio kulipa kodi na serikali haisimamii kisawasawa masuala ya ulipaji kodi (sijawahi kusikia mtanzania amefungwa kwa kukwepa kodi) wafanyabiashara wameamua kusimama imara kuibabaisha serikali hadi ilegeze uzi tubakie na mfumo wa zamani wa kukwepa kodi. Pia jana simu za pongezi kutoka mikoa mingine zilipigwa kwa wafanyabiashara wa mwanza kuwa wakaze uzi, wawe ngangari. pia baadhi ya maafisa wa tra walikuwa wanahamasisha kichinichini huu mgomo kwa vile matumizi ya hizi mashine yanawanyima ile dili yao iliwafanya wajenge magorofa ya kukadiria kodi. Kwa hiyo kinachopingwa kwenye huu mgomo sio bei ya mashine za efd, bali ni matumizi ya efd ili kuendeleza utamaduni wa kukwepa kodi. Bei ni kisingizio tu, nashauri serikali iwanunulie iwape bure kwani itarudisha tu hela zake, ingawa huku mwanza hata za bure hawataki kama picha hapo juu inavyoonesha

katika nchi ambayo zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wake hawalipi kodi, ni ndoto kuwa na miundombinu bora, elimu bora, afya bora na huduma zingine. Mama zetu wanalala wanne kitanda kimoja wakati wa kujifungua kwa kuwa pamoja na utawala mbovu wa ccm lakini pia wameshindwa kupata tax base kubwa. Kama chini ya asilimia 20 ya wananchi ndio wanalipa kodi ina maana hao 80% wanatunzwa na hao 20%. Serikali inatakiwa kusimama imara kwenye huu mgogoro kwani matumizi ya efd ndio future ya biashara tanzania. Kwa sasa ukwepaji kodi ndio competitive advantage ya biashara nyingi, ili upate faida kubwa zaidi lazima uwakwepe/uwahonge tra usilipe kodi ili uuze bei rahisi, wakati umefika serikali kuwa imara. waacheni wafanyabiashara wafunge maduka hadi panya wamalize bidhaa za dukani, njaa zikiwauma watafungua tu. Pia ulinzi uimarishwe kwa wafanyabiashara walio tayari kulipa kodi na kutumia efd kwa kuwa zinazuia kuibiwa pia.

View attachment 129539

tatizo elimu tu
 
Aliyesema Mkuki kwa nguruwe... alikuwa na iq kubwa. Wafanyakazi tumekuwa tukipiga kelele tunakatwa kodi kubwa mno tena kila mwezi , wenzetu wafanya biashara wanacheka tu maana hawaguswi na tatizo hilo. Leo nao wametakiwa kununua EFD ili walipe kodi kama sisi wanaweweseka! Nunueni mashine fasta, hii nchi ni yetu wote, tuijenge wote. Serikali, kazg uzi wanunue. Asiyenunua funga biashara yake. Nymbaf
 
Nami nilihisi hilo. Sikuona sababu kubwa ya kugoma. Good observation! Mashine zipunguzwe bei na wafanyabiashara wote wanaotakiwa kutumia watumie. Serikali ikomae!
hata wapunguze bei,mashine zitaharibiwa.
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu,kusema ukweli mimi mwanzoni nlikuwa nawaunga mkono wafanyabiashara ila ni kwa misingi ya gharama ya mashine na kwa mantiki kuwa serikali ipunguze bei ila nimestuka kusikia wafanyabiashara wanadai eti hata zikiuzwa BURE HAWATAZITUMIA!!! Heee! Nimeshangaa sana na ndipo kutambua kuwa kumbe uyasemayo ndo ukweli wenyewe uliojificha humo ... cha kushangaza utasikia serikali inasema UTARATIBU WA ZAMANI UTUMIKE eti kisa hao ndo wapiga kura wetu... teh... hatufiki!
 
Wewe ndio umefilisika kabisa kimawazo je unaweza kutuambia kwa kodi inayolipwa hivi sasa ni kiasi gani kinarudi kwa mwananchi na kiasi gani kinaingia mifukoni mwa watu au kuwekwa uswiss kwenye mabenki? kuna uhakika gani ongezeko la kodi linalosakwa halitaingia mifukoni mwa watu lote au kutumika kuibulia EPA nyingine kwa ajili ya uchaguzi? ishu sio kukusanya ishu ni zinatumikaje? Tatizo lingine ni kwamba Tanzania ina kodi nyingi mno na kubwa na hakuna mfanyabiashara yoyote anayeweza kuzilipa kiuhalali bila kuuwa mtaji na kufilisika; sasa swali ni nani alibuni hii mifumo ya kodi isyofaa ili kushinikiza watu wategemee rushwa na ukwepaji kodi? kwanini walipaji kodi wakubwa ni walalahoi wakati makampuni makubwa ya kifisadi yanasamehewa na kukwepa kodi bila kuhojiwa? badala ya kumuinua mwananchi aliyeuza thamani zake za ndani afanye biashara wakati serikali imemnyima ajira na elimu ni serikali hiyohiyo imeweka mbele kumkandamiza. Kwa vyovyote siungi mkono migomo lakini ni muhimu kuliangalia jambo hili kwa uzito unaostahili na si kulisemea kishabiki.

Mkuu usichanganye madesa!wafanyabiashara hawajagoma eti kwa vile kodi wanazolipa hazitumiki vizuri!wangegoma kwa issue hiyo hata mimi ningewaunga mkono!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mfanyabiashara mwenye mauzo ya Tsh 14,000,000 (milioni kumi na nne) kodi yake ni Tsh 364,000 kwa mwaka. Je atawezaje kuikata iyo garama ya mashine ya EFD kwa mwaka mmoja? Je anaweza kumudu garama za muhasibu (CPA (PP) kumtengenezea hesabu ili aweze kukata pesa alizonunulia mashine? Je huko wilayani kama Sikonge na Urambo ambako hata umeme hamna kuna wahasibu?
Nachangia tu.
 
Mkuu usichanganye madesa!wafanyabiashara hawajagoma eti kwa vile kodi wanazolipa hazitumiki vizuri!wangegoma kwa issue hiyo hata mimi ningewaunga mkono!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Hivi wewe jamaa yangu vipi wewe si ndiye uliyeleta mambo ya nyuma ya pazia tofauti na kile kilichoko mezani? sasa sisi tukikujibu nyuma ya pazia unaleta machozi ya mamba? yataenda na maji tuuuuu
 
Hapo utasikia chedema ndo wameandaa migomo yote kuanzia mbaya dar na sasa mwanza.
 
Mkuu tuungane na serikali katika hili, hawa wafanyabiashara wanataka ku Blackmail serikali kwa maslahi yao binafsi. Lazima walipe kodi, mbona wafanyakazi wanakatwa juu kwa juu na hawajawahi kugoma na kodi wanayolipa ni kubwa kwa asilimia kuliko za wafanyabiashara

uungane na serikali gani? serikali ya hovyo hivi?

kama wewe umeajiriwa na unalipishwa kodi kilazima kimpango wako.

serikali imaeshikwa pabaya, na hawana uwezo wa kwenda kinyume na matakwa ya wafanyabiashara.

viongozi wanafisadi, rasilimali zinachezewa halafu useme tulipe kodi ili baba mwanaasha aende nayo marekani kila kkicha?

kama ukitaka tukuunge mkono hakikisha misamaha ya kodi yote inafutwa na atleast hayo makampuni yaliosamehewa kodi wanalipa kuanzia 2000 had leo.
 
Back
Top Bottom