Ulukolokwitanga
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 8,396
- 7,968
- Thread starter
- #61
Dawa ni kuwa mfanyabiashara kuepuka kulipa kodi kubwa
Hata Robert Kiyosaki ameliongelea hilo...
Dawa ni kuwa mfanyabiashara kuepuka kulipa kodi kubwa
Sijui serikali ina promote watu wawe wafanyabiashara sijui, mambo ya kodi yangewekewa mkazo kama wabunge nao wangekuwa wanakatwa kodi mapato yao hivyo practically wangeelewa kile ambacho wananchi wanalalamika. Kuhusu hili suala la EFD nadhani serikali kuna haja ya kuangalia hizi kodi zao kama ni kubwa kiasi cha kumuumiza mwananchi na kuzifanyia marekebisho ili wananchi wengi walipe kodi huku ikipandisha mdogo mdogo baada ya wananchi kuelewa umuhimu wa kodi (yote yafanyike lakini serikali irudishe feedback kwa wananchi kwa kuleta maendeleo). Ila wakati mwingine huwa najiuliza inakuaje maduka ya wahindi wao hata kabla ya EFD wamekuwa mstari wa mbele kutoa receipt na wanakuandikia kabisa VAT ni hii na amount ya mzigo uliochukua ni huu tena wanakupa receipt bila kuomba (hapa ndio huwa nachanganyikiwa kwanini wengine inakuwa issue)Hata Robert Kiyosaki ameliongelea hilo...
Sijui serikali ina promote watu wawe wafanyabiashara sijui, mambo ya kodi yangewekewa mkazo kama wabunge nao wangekuwa wanakatwa kodi mapato yao hivyo practically wangeelewa kile ambacho wananchi wanalalamika. Kuhusu hili suala la EFD nadhani serikali kuna haja ya kuangalia hizi kodi zao kama ni kubwa kiasi cha kumuumiza mwananchi na kuzifanyia marekebisho ili wananchi wengi walipe kodi huku ikipandisha mdogo mdogo baada ya wananchi kuelewa umuhimu wa kodi (yote yafanyike lakini serikali irudishe feedback kwa wananchi kwa kuleta maendeleo). Ila wakati mwingine huwa najiuliza inakuaje maduka ya wahindi wao hata kabla ya EFD wamekuwa mstari wa mbele kutoa receipt na wanakuandikia kabisa VAT ni hii na amount ya mzigo uliochukua ni huu tena wanakupa receipt bila kuomba (hapa ndio huwa nachanganyikiwa kwanini wengine inakuwa issue)
Kama sio biashara ya kiongozi moja wa serikali basi tra iruhusu wafanyabiashara waagize wenyewe wanaojua iwe china uarabuni au hara mbinguni haafu serikali isajili tu na kuzipa namba au laa serikali iagize popote na kuwapa bure wafanyabiashara maana hawa ni vitegauchumi (sehemu ya kukusanyia kodi serikali hivyo ni muhimu kuwakopesha au kuwapa bure
Ila saiv walau tunaenda kuzuri. Naona had wakwepa kodi mashuhuri (wahindi) waameanza ,na katika migomo hyo nadhan wahind watakuwa wachache sanaa au hawapo.kwa wale wachache naowafaham hapa dar naona wapo very careful kwenye kufuata sheria now.kuna vipenalt wamepigwa hv karibun vimewashtua.,
Watanzania TUTAMANI MAENDELEO NA HATUTAKI KULIPA KODI Ni aibu iloje . Kwenye hili Serikali isimame imara na isiyubishwe na wahuni.
Serikali hii ya MIZIGO kamwe hawezi kununua EFD na kuwapa bure wafanyabiashara, hapo wameishika pabaya. Nasema wagome Tu, tumechoka
Kiongozi tunayo nafasi pia ya kudai uwajibikaji wa serikali na matumizi sahihi ya kodi zetu. Wakati huu tunagomea au hatutaki kulipa kodi, hata hicho kidogo kingechopatikana huenda kingeokoa maisha ya watanzania wenzetu kwa angalau kiasi kidogo cha dawa za kutibu magonjwa yao. Then ikifika 2015 tufanya maamuzi sahihi kwa kuweka serikali itakayojali matumizi ya kodi zetu. I understand your frustrations kiongozi...
MKUU WA MKOA MWANZA CHUKUA HATUA
Leo ni siku ya tatu tangia kuwe na mgomo wa wafanyabiashara katika jiji la Mwanza ambao umepelekea maduka kufungwa.
Maduka mengi yaliofungwa ni yale ya katikati ya mji, na moja ya sababu iliyosababishwa maduka kufungwa ni malalamiko ya muda mrefu ya wafanya biashara wa mji huo dhidi ya mashine za EFD na utaratibu mzima wa kupata leseni na mambo mengine mengi ambayo wamesema sasa ni wakati wa kufikisha ujumbe.
Kiukweli hoja zao ni za muhimu na zinatakiwa kufanyiwa kazi lakini kuna jambo moja ama mawili yamenistua kwanza baada ya kuwepo eneo la tukio nilibahatika kuonana na wazee mbali mbali ambao wengi wanamatatizo ya afya kama inavyojulikana asilimia kubwa ya wazee wetu afya zao hazipo sahihi,wazee hao wanalalamika kufungwa kwa maduka ya Dawa nay a Vyakula hii inawaumiza sana.
Baadhi ya Wafanyabiashara wengi wamesema wao wapo tayari kufungua Maduka yao lakini wanatishiwa kufanyiwa fujo na makundi ya wahuni na wamedai hili suala lipo chini ya kikundi kimoja cha wahuni kinachodhaminiwa na chama kimoja cha siasa.
Ombi lao kubwa ni kwa mkuu wa mkoa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuruhusu maduka yafunguliwe kwa walio tayari na kuhakikisha ulinzi wa hali ya juu.
Inasemekana kuwa CHADEMA ndio wameanzisha hoja hiyo na ni maandalizi ya Mbowe kuja kuhutubia mjini hapo,la msingi Mbowe na Chama chake lazima watambue kuwa mpaka wao wanafika mwanza kuhutubia mamia ya watanzania wasiokuwa na mitazamo ya kisiasa watakuwa wamekufa kwa kukosa Dawa na Chakula,wafanyabiashara ambao mitaji yao midogo ndio watakuwa wamefilisika kabisa na kusababisha matatizo makubwa kwao na familia zao.
Ifike wakati kabla ya kuanzisha mchakato wasomi wake chini na kupanga vizuri maana kama Mbowe ukiumwa unaweza tibiwa na kupata dawa popote lakini si raia masikini wa Mwanza maana duka hata la Panadol mmefunga!MKUU WA MKOA MWANZA CHUKUA HATUA
Leo ni siku ya tatu tangia kuwe na mgomo wa wafanyabiashara katika jiji la Mwanza ambao umepelekea maduka kufungwa.
Maduka mengi yaliofungwa ni yale ya katikati ya mji, na moja ya sababu iliyosababishwa maduka kufungwa ni malalamiko ya muda mrefu ya wafanya biashara wa mji huo dhidi ya mashine za EFD na utaratibu mzima wa kupata leseni na mambo mengine mengi ambayo wamesema sasa ni wakati wa kufikisha ujumbe.
Kiukweli hoja zao ni za muhimu na zinatakiwa kufanyiwa kazi lakini kuna jambo moja ama mawili yamenistua kwanza baada ya kuwepo eneo la tukio nilibahatika kuonana na wazee mbali mbali ambao wengi wanamatatizo ya afya kama inavyojulikana asilimia kubwa ya wazee wetu afya zao hazipo sahihi,wazee hao wanalalamika kufungwa kwa maduka ya Dawa nay a Vyakula hii inawaumiza sana.
Baadhi ya Wafanyabiashara wengi wamesema wao wapo tayari kufungua Maduka yao lakini wanatishiwa kufanyiwa fujo na makundi ya wahuni na wamedai hili suala lipo chini ya kikundi kimoja cha wahuni kinachodhaminiwa na chama kimoja cha siasa.
Ombi lao kubwa ni kwa mkuu wa mkoa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuruhusu maduka yafunguliwe kwa walio tayari na kuhakikisha ulinzi wa hali ya juu.
Inasemekana kuwa CHADEMA ndio wameanzisha hoja hiyo na ni maandalizi ya Mbowe kuja kuhutubia mjini hapo,la msingi Mbowe na Chama chake lazima watambue kuwa mpaka wao wanafika mwanza kuhutubia mamia ya watanzania wasiokuwa na mitazamo ya kisiasa watakuwa wamekufa kwa kukosa Dawa na Chakula,wafanyabiashara ambao mitaji yao midogo ndio watakuwa wamefilisika kabisa na kusababisha matatizo makubwa kwao na familia zao.
Ifike wakati kabla ya kuanzisha mchakato wasomi wake chini na kupanga vizuri maana kama Mbowe ukiumwa unaweza tibiwa na kupata dawa popote lakini si raia masikini wa Mwanza maana duka hata la Panadol mmefunga!
Kuna haja kila Mtz apewe TIN yake hata kama ameajiriwa kile anachokatwa kinakuwa indicated kwenye TIN yake ili wajenga nchi watambuliwe pia endapo mtu unakuwa unaingiza mihela ambayo haileweki inakuwa rahisi kuangalia profile yako TRA maana kwa nchi yetu ni kawaida kukuta mtu ana mali za milioni 300 ukifuatilia kodi katika kipindi cha miaka 10 akijitahidi amelipa 5 million. Hata hawa wanasiasa wanapotaka kuomba kura ingekuwa vyema kama kigezo cha ulipaji kodi angalau miaka 5 mfululizo nacho kitumike ili kujenga taifa la walipa kodi unless shughuli anazozifanya ni zile ndogo ndogo zinazoangukia kwenye ushuru wa halmashauri (hata hapa awe na receipt wakati wa kuchukua fomu). Yaani kama watu wangekuwa wanalipa kodi kihalali hata Profesa Muhongo asingepata jeuri ya kusema 'watz hatuwezi kuwekeza kwenye gas' maana njia pekee ya kisayansi ya kumwangalia mtu mwenye fedha ni kwa kuangalia mamlaka zinazohusika na ukusanyaji wa mapato na si kuangalia idadi ya maghorofa anayomilki, tukifanya hivi watu watakuwa wanalipa kodi ili wasikose deal mbalimbali za serikaliTatizo la kutolipa kodi hapa kwetu ni la kimfumo. Kumbuka hata wabunge wakati wa upangaji bajeti ya serikali linapokuja suala la kodi za magari huwa wanahakikisha kuwa aina ya magari ambayo wabunge wengi wanatumia hayawekewi kodi kubwa licha ya kuwa ni magari ya bei mbaya. Nchi nyingine watu wamebadilika sana, nchi kama Denmark ukikwepa kodi hadi watoto wa kuwazaa mwenyewe wanakukana kuwa sio baba yao. Kukwepa kulipa kodi huko ni Anti-social behavior. Huku kwetu wakwepa kodi ndio mashujaa na ndio wenye maisha mazuri