Mgomo wa EFDs: Kilichopo nyuma ya pazia. Serikali isimame IMARA

Mtoa Mada Tafadhali UCPOTOSHE UMMA: Kama Hujui Sababu Ya Mgomo Ni Bora Ukanyamaza... Nianze Na Hili La Bei Umesema Katika Post Yako Dubai Ni US50/TSH ELEU 80 TU. Ukatoatoa Mfano Kenya Ni Tsh 150,000= Pamoja Na Kutokuwa Sahihi Bei Zako Je Wewe Unaweza Nunua Kitu Cha Elf 80 Kwa Laki Nane?? Na Kama Tatizo Ni Mashne Kwann Wasiruhusu Wafanyabiashara Waagize/wanunue Wenyewe Sehemu Wanayotaka??? Je Ni Kwann Walazimishe Service Ya Mashine Iwe Elf 60 Hata Kama Ni Kubadilisha Karatasi Zikiisha??? Hv Mazingra Kama Haya Ndg Yangu Wewe Unayaona Ni Sahih Mpaka Wafanyabiashara Wakubali Wizi Huu Wa Kimachomacho Wanaofanyiwa Na Serikali Yao Kumbuka Kuna Wegne Wamekopa Kwa Wizi Huu Lazima Watafungwa LAKIN Kubwa Kumbuka Mfanyabiashara Hana Hasara Maumivu Ya EFDs Atakaye Yabeba Ni Mimi Na Wewe Mimi Nilifikiri Tunawasaidia Wafanyabiasha Kudai Hili Ili Unafuu Upatikane Kwetu WALAJI.. Msimamo Huo Ungeiambia Serikali Na Misamaha Ya Kodi Kwa Makampuni Makubwa Na Ya Nje Wewe Unashadadia Walalahoi Wenzako... Buushit

Ninyi ndiyo tunawaita mbumbumb na wadandiaji mambo, mnashabikia hata kitu usichokifahamu! Hebu nisomee hayo maandishi kwenye bango kuu la wafanyabiashara wa Mwanza, HAWATAKI MASHINE HATA BURE! Mimi nauza hizi mashine, kampuni nayochukua mashine wanahiyo project kenya na Malawi, hakuna nchi wanayouza chini ya laki 4!!! Na hiyo ni baada ya serikali kufuta kodi na kusubsidize, hapa Tanzania mashine technically ZINAGAWIWA BURE!!! Kuhusu matengenezo, hiyo elfu 60 ya matengenezo ni kama hauna contract na kampuni, ukitaka kuingia mkataba na kampuni gharama za matengenezo hazizidi laki na 20 kwa mwaka (wastani wa elfu 10 kwa mwezi!!), kila ofisi lazima iwe na angalau technician mmoja, analipwa si chini ya 350,000 kwa mwezi!!! Wafanyabiashara, mimi nikiwemo tunaelewa wazi kuwa ukiwa na EFD kukwepa kodi inakuwa ngumu, labda uandike risiti bei chini, au usiandike kabisa jambo ambalo unaweza kupigwa fine ya mpaka 5M!!! ACHENI USHABIKI WA MAMBO MSIYOYAFAHAMU!
 
Mleta mada naona umezungumzia jambo moja tu la wafanyabiashara kugomea mashine ama kulipa kodi. Tatizo sio kodi kama ulivyodai wewe Mwanza wana kero nyingi ambazo zimepelekea mgomo huo kutokea, kuna kero zinazohusu maofisa wa TRA na kero za jiji, na hili la mashine ikiwa ni mojawapo na iliyobeba kero zote. Wewe unadhani ni sahihi kununua mashine hiyo kwa Tsh.800,000/ service 60,000/ kuna rim page moja yenye receipt 6 tu sh.2000/ na ukikosea kidogo tu receipt moja faini kuanzia 1,500,000 - 5,000,000/ (ikifikia hapa kuna majadiliano ya kulipia pesa hiyo hotelini/bar hii ndio ijengayo sijui) usisahau wino siuji sh. ngapi vile. Wacha wagome kwani tuumio ni sisi end user.

like mkuu, tena big like

mtawalazimisha ila kumbukeni hidden costs zote mtaletewa final consumers.
 
Mleta mada naona umezungumzia jambo moja tu la wafanyabiashara kugomea mashine ama kulipa kodi. Tatizo sio kodi kama ulivyodai wewe Mwanza wana kero nyingi ambazo zimepelekea mgomo huo kutokea, kuna kero zinazohusu maofisa wa TRA na kero za jiji, na hili la mashine ikiwa ni mojawapo na iliyobeba kero zote. Wewe unadhani ni sahihi kununua mashine hiyo kwa Tsh.800,000/ service 60,000/ kuna rim page moja yenye receipt 6 tu sh.2000/ na ukikosea kidogo tu receipt moja faini kuanzia 1,500,000 - 5,000,000/ (ikifikia hapa kuna majadiliano ya kulipia pesa hiyo hotelini/bar hii ndio ijengayo sijui) usisahau wino siuji sh. ngapi vile. Wacha wagome kwani tuumio ni sisi end user.

Mkuu, wewe unatumia mashine aina gani, inaonekana uko misinformed na unamislead watu!
 
Acha wagome tu maana hata hiyo kodi kidogo wanayopata hawaitumii ipasavyo. Hopitali hazina dawa, umeme sio wa uhakika, barabara mbovu basi taabu tu, wao kila siku tuongeze kodi kwa manufaa yao na familia zao. Mgomo uendeleee,

Mkuu samahani je unaweza kujaribu kutafakari tena na ukapima usahihi wa hiki ulichokiandika?
 
Hapana a2ibii serikar ila EFDs zinauzwa gharama kubwa na wakara pia znawah haribika Na gharama ya kuzitengeneza Ipo juu Na karatasi za receipt zinauzwa Na wakala huyo huyo kwabei anayotaka salsa hiyo cnibiashara ya ku2nyonya?????
 
Nashukuru sana mtoa hoja ulianza vzur sana mwanzoni kwa kueleza bei halis ya Electronic Fiscal Divices (EFD) ni kwel kabsa znapatikana kwa bei hiyo ila mwishon epotosha uma kwa kusa ni njia ya kukwepa kulipa kodi sio sahihi bali wanachogomea wafanya biashara huku mby ilikua ni bei ghali ya hzo machine bad, ndug zangu wa jf hakuna anaekimbia kulipa kodi km hamuamin shaurin serikal yenu ipunguze bei au igawe bure...
 
Serikali ianze kwa kurekebisha wafanyakazi wa mamlaka ya mapato . tuanze kwa kumwondoa Kamishna jerero. huyu mtu ana zaidi ya miaka stini. unakaa pale TRA kwa manufaa ya nani. kubebabeba vibabu kazini kunawanyima vijana ajiraaaa

Hii ni ajabu sana miaka nenda rudi Kamishna Jenero ni huyo huyo, hivi hakuna hata Fresh Start? Hawa wazee wa zama za analojia hawana cha kupoteza ndio maana kamvuta swahiba yake Blandina Nyoni. Ni dhahiri kuwa serikali hii ya CCM haioni umuhimu wa kodi ndio maana haitaki kufanya reform TRA, misaada ya wadhungu imetuchanganya kabisa.
 
Nashukuru sana mtoa hoja ulianza vzur sana mwanzoni kwa kueleza bei halis ya Electronic Fiscal Divices (EFD) ni kwel kabsa znapatikana kwa bei hiyo ila mwishon epotosha uma kwa kusa ni njia ya kukwepa kulipa kodi sio sahihi bali wanachogomea wafanya biashara huku mby ilikua ni bei ghali ya hzo machine bad, ndug zangu wa jf hakuna anaekimbia kulipa kodi km hamuamin shaurin serikal yenu ipunguze bei au igawe bure...
Huku Mwanza wanasema hata zikigawiwa bure hawachukui. Mkuu nimefanya utafiti wa kutosha kwa vile hata mimi ni mhanga wa huu mgomo wa Mwanza but mwisho wa siku nimegundua kwa uhakika kabisa kuwa kinachogomewa sio EFDs, zenyewe zimetumiwa kama chambo tu. Ni kweli kuwa TRA wana matatizo yao na ndio chanzo hata cha hii migomo, lakini kilichoko nyuma ya pazia ni zaidi ya kugomea mashine
 
Hapana a2ibii serikar ila EFDs zinauzwa gharama kubwa na wakara pia znawah haribika Na gharama ya kuzitengeneza Ipo juu Na karatasi za receipt zinauzwa Na wakala huyo huyo kwabei anayotaka salsa hiyo cnibiashara ya ku2nyonya?????

Hebu niambie aina ya biashara unayofanya na mashine unayotumia nikupe technical advice bure! Andika kwa kiswahili fasaha.
 
Ninyi ndiyo tunawaita mbumbumb na wadandiaji mambo, mnashabikia hata kitu usichokifahamu! Hebu nisomee hayo maandishi kwenye bango kuu la wafanyabiashara wa Mwanza, HAWATAKI MASHINE HATA BURE! Mimi nauza hizi mashine, kampuni nayochukua mashine wanahiyo project kenya na Malawi, hakuna nchi wanayouza chini ya laki 4!!! Na hiyo ni baada ya serikali kufuta kodi na kusubsidize, hapa Tanzania mashine technically ZINAGAWIWA BURE!!! Kuhusu matengenezo, hiyo elfu 60 ya matengenezo ni kama hauna contract na kampuni, ukitaka kuingia mkataba na kampuni gharama za matengenezo hazizidi laki na 20 kwa mwaka (wastani wa elfu 10 kwa mwezi!!), kila ofisi lazima iwe na angalau technician mmoja, analipwa si chini ya 350,000 kwa mwezi!!! Wafanyabiashara, mimi nikiwemo tunaelewa wazi kuwa ukiwa na EFD kukwepa kodi inakuwa ngumu, labda uandike risiti bei chini, au usiandike kabisa jambo ambalo unaweza kupigwa fine ya mpaka 5M!!! ACHENI USHABIKI WA MAMBO MSIYOYAFAHAMU!

Suala la kutotaka kulipa kodi hapa Tanzania ni la kimfumo zaidi. Watanzania tumezoea DEZO bila kuelewa kuwa kama hatutabadilika na kuanza kulipa kodi maendeleo kwenye nchi yetu tutayasikia bombani. Hata wakati tunatumia risiti za vitabu ambazo ni kazi ngumu zaidi kuliko kutumia hii machine bado kulikuwa na gharama za kununua vitabu vya risiti kwa wachapishaji. Wako wafanyabiashara wanatumia hadi vitabu 10 kwa siku ambayo gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko hata EFD. Mfano mzuri ukiwa pale Mlimani City, ukiingia duka la Game au Shoprite kila transaction lazima upate risiti za EFD, tena mara nyingine risiti mbili per transaction, but ukitoka tu humo kwa makaburu ukaingia kwenye duka lolote la mtanzania ndani ya compound ya Mlimani City haupewi risiti kabisa, au ukipewa ni za vitabu. Wakati umefika sasa serikali yetu ielimishe wafanyabiashara umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa
 
Nashukuru sana mtoa hoja ulianza vzur sana mwanzoni kwa kueleza bei halis ya Electronic Fiscal Divices (EFD) ni kwel kabsa znapatikana kwa bei hiyo ila mwishon epotosha uma kwa kusa ni njia ya kukwepa kulipa kodi sio sahihi bali wanachogomea wafanya biashara huku mby ilikua ni bei ghali ya hzo machine bad, ndug zangu wa jf hakuna anaekimbia kulipa kodi km hamuamin shaurin serikal yenu ipunguze bei au igawe bure...

Wewe bwana wewe, hivi unafkiri utawaongopea watu humu JF, wengi wanafanya biashara kama wewe, EFD ni mshipa kwa wafanyabiashara, ile mambo ya kuchana risiti na kuandikia pembeni HAKUNA, kuwa na vitabu double vyenye serial numbe hiyohiyo HAKUNA, ujanja wato kwenye EFD mwisho, mfanyabiashara akiskia hivyo roho inakwenda mbio! Na aliyewandanganya mashine sjui zinauzwa 60 dollar mpaka leo sijaona mfanyabiashara amekuja na sample moja na receipt inayoonesha dola 60 wakati kila siku mnaenda china...ukiuziwa mashine bei hiyo ujue utatumia miezi miwili imekwisha!!
 
uungane na serikali gani? serikali ya hovyo hivi?

kama wewe umeajiriwa na unalipishwa kodi kilazima kimpango wako.

serikali imaeshikwa pabaya, na hawana uwezo wa kwenda kinyume na matakwa ya wafanyabiashara.

viongozi wanafisadi, rasilimali zinachezewa halafu useme tulipe kodi ili baba mwanaasha aende nayo marekani kila kkicha?

kama ukitaka tukuunge mkono hakikisha misamaha ya kodi yote inafutwa na atleast hayo makampuni yaliosamehewa kodi wanalipa kuanzia 2000 had leo.
Kiongozi tunayo nafasi pia ya kudai uwajibikaji wa serikali na matumizi sahihi ya kodi zetu. Wakati huu tunagomea au hatutaki kulipa kodi, hata hicho kidogo kingechopatikana huenda kingeokoa maisha ya watanzania wenzetu kwa angalau kiasi kidogo cha dawa za kutibu magonjwa yao. Then ikifika 2015 tufanya maamuzi sahihi kwa kuweka serikali itakayojali matumizi ya kodi zetu. I understand your frustrations kiongozi...
 
Suala la kutotaka kulipa kodi hapa Tanzania ni la kimfumo zaidi. Watanzania tumezoea DEZO bila kuelewa kuwa kama hatutabadilika na kuanza kulipa kodi maendeleo kwenye nchi yetu tutayasikia bombani. Hata wakati tunatumia risiti za vitabu ambazo ni kazi ngumu zaidi kuliko kutumia hii machine bado kulikuwa na gharama za kununua vitabu vya risiti kwa wachapishaji. Wako wafanyabiashara wanatumia hadi vitabu 10 kwa siku ambayo gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko hata EFD. Mfano mzuri ukiwa pale Mlimani City, ukiingia duka la Game au Shoprite kila transaction lazima upate risiti za EFD, tena mara nyingine risiti mbili per transaction, but ukitoka tu humo kwa makaburu ukaingia kwenye duka lolote la mtanzania ndani ya compound ya Mlimani City haupewi risiti kabisa, au ukipewa ni za vitabu. Wakati umefika sasa serikali yetu ielimishe wafanyabiashara umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa

Uko sahihi Mkuu, Watanzania tumezidi kukwepa kodi!
 
Kama sio biashara ya kiongozi moja wa serikali basi tra iruhusu wafanyabiashara waagize wenyewe wanaojua iwe china uarabuni au hara mbinguni haafu serikali isajili tu na kuzipa namba au laa serikali iagize popote na kuwapa bure wafanyabiashara maana hawa ni vitegauchumi (sehemu ya kukusanyia kodi serikali hivyo ni muhimu kuwakopesha au kuwapa bure
 
HUyo mama Blinded Nyomi (lol) Blandina Nyoni ni hatare kwa afya ya taifa hili..kila mahala anapokua lazima akinukishe!

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyoni kwa sasa amerejea kwa mwajiri wake wa awali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akishikilia nafasi ya mmoja wa wakuu wa idara, huku Dk Mtasiwa akiwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Katibu Mkuu Kiongozi
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amelithibitishia gazeti hili kuhusu watumishi hao na kwamba taratibu zimefuatwa.

“Mimi ninachojua ni kwamba Blandina alikuwa mwajiriwa wa TRA na mkataba wake ulikuwa haujaisha… Siyo kwamba alikuwa na mikataba miwili, kwenye utumishi wa umma huwa kuna utaratibu wa kuazima watumishi wa umma.
Ndiyo maana unaweza kukuta mwanajeshi anatolewa jeshini na kupelekwa uraiani au mtumishi kutoka idara moja kwenda nyingine. Kwa upande wetu sisi tulishamwondoa kwenye ukatibu mkuu na kule TRA hakuwa na tatizo,” alisema Balozi Sefue.

Hili li nchi kwa kweli limelaaniwa, haiyumkiniki jitu jizi kama Blandina Nyoni ambalo lilikuwa sehemu yenye fursa hafifu lakini likawa linaiba na kujipatia tenda. Then leo hii limehamishiwa kwenye Mamlaka ya Mapato, amboko ndio ROHO ya serikali. Hii serikali ya CCM ina dharau sana na suala zima la ukusanyaji kodi, hii ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi. Blandina Nyoni alishafikia ufisadi wa kiwango cha kidunia, inakuwaje leo anapewa nafasi akaibe hata kodi zetu??

Back to topic, EFDs ni lazima kwa maendeleo ya Taifa
 
Watu wanakula vumbi k koo harafu wanunue EFDs sio rahisi kihivyo mgomo mpaka kieleweke.
 
View attachment 129543
Jana wafanyabiashara wa Mwanza walianza kile wanachokiita Mgomo usio na Kikomo kugomea mashine za kutunza kumbukumbu za mauzo na kukadiria ushuru zijulikanazo kama EFD. Pia siku za nyuma tulisikia mgomo wa aina hiyo hiyo Dar na Mbeya. Sababu wanayotumia ni ya msingi sana kuwa hawawezi kununua mashine hizo kwa bei ya shilingi laki nane (800,000=) tena kwa makampuni maalum wakati mashine hizo China zinauzwa dola 50 tu (kama 80,000 za kitanzania) na Kenya ziko madukani kwa retail price ya 150,000Tshs. Hapo TRA inastahili lawama kwa kutumia mfumo CCM ambao kila kunapokuwa na bidhaa mpya watu wanakimbilia kupiga dili, ilitokea kwenye Speed Governer, Plate namba za magari na hata kwenye mikanda usalama ya mabasi. Hapa kuna makandokando yanaoonesha kuna dili inapigwa TRA ndo maana hawataki Biashara huria ya EFD wao kazi yao iwe Calibration tu ya mashine. Pia mashine hizi za bei mbaya pia zinaharibika haraka na wao wateule wanouza wamejipa na dili la kufanya maintenance kwa shilingi kuanzia elfu sitini (60,000) na kuendelea, wakati kiuasilia hizi mashine ni kama Calculator ya kawaida iliyoongezewa akili kidogo tu hivyo hazina gharama kubwa kihivyo kutengeneza. Kumbuka wengine tukipeleka gari garage za ushwahilini kufanya service huwa tunalipa elfu kumi, iweje mashine hizi service au maintenance iwe elfu sitini na kuendelea. Hapo TRA jitazameni, hiyo ni hoja ya wafanyabiashara

Ukweli halisi ni kuwa wafanyabiashara wanachogomea ni KULIPA KODI kwa kuwa hizi mashine zinatunza kumbukumbu vizuri na zinazuia kila aina ya Magumashi ambayo ndio msingi wa biashara nyingi Tanzania. Wakati wa uhamasishaji wa mgomo wa Mwanza, tulielezwa na wachochezi wa huo mgomo kuwa kama zikitumika hizi mashine wafanyabiashara wengi watafilisika kwa maana toka zimeanza kutumika hizi mashine wengi wanalipa kodi kubwa kuliko zamani. Kwa kuwa utamaduni wetu watanzania sio kulipa kodi na serikali haisimamii kisawasawa masuala ya ulipaji kodi (Sijawahi kusikia mtanzania amefungwa kwa kukwepa kodi) wafanyabiashara wameamua kusimama imara kuibabaisha serikali hadi ilegeze uzi tubakie na mfumo wa zamani wa kukwepa kodi. Pia jana simu za pongezi kutoka mikoa mingine zilipigwa kwa wafanyabiashara wa Mwanza kuwa wakaze uzi, wawe ngangari. Pia baadhi ya maafisa wa TRA walikuwa wanahamasisha kichinichini huu mgomo kwa vile matumizi ya hizi mashine yanawanyima ile dili yao iliwafanya wajenge magorofa ya KUKADIRIA KODI. Kwa hiyo kinachopingwa kwenye huu mgomo sio bei ya mashine za EFD, bali ni matumizi ya EFD ili kuendeleza utamaduni wa kukwepa kodi. Bei ni kisingizio tu, nashauri serikali iwanunulie iwape bure kwani itarudisha tu hela zake, ingawa huku Mwanza hata za bure hawataki kama picha hapo juu inavyoonesha

Katika nchi ambayo zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wake hawalipi kodi, ni ndoto kuwa na miundombinu bora, elimu bora, afya bora na huduma zingine. Mama zetu wanalala wanne kitanda kimoja wakati wa kujifungua kwa kuwa pamoja na utawala mbovu wa CCM lakini pia wameshindwa kupata TAX BASE kubwa. Kama chini ya asilimia 20 ya wananchi ndio wanalipa kodi ina maana hao 80% wanatunzwa na hao 20%. Serikali inatakiwa kusimama imara kwenye huu mgogoro kwani matumizi ya EFD ndio future ya biashara Tanzania. Kwa sasa ukwepaji kodi ndio Competitive Advantage ya biashara nyingi, ili upate faida kubwa zaidi lazima uwakwepe/uwahonge TRA usilipe kodi ili uuze bei rahisi, wakati umefika serikali kuwa imara. Waacheni wafanyabiashara wafunge maduka hadi panya wamalize bidhaa za dukani, njaa zikiwauma watafungua tu. Pia ulinzi uimarishwe kwa wafanyabiashara walio tayari kulipa kodi na kutumia EFD kwa kuwa zinazuia kuibiwa pia.

View attachment 129539
Njia mpya ya taasisi kujibu mapigo, safi sana.
 
watanzania bwana kwa kutoelewa alokwambia wenye maduka hawalipi kodi kakudanganya hiyo ni mojatu kati ya milolongo ya kodi wanazolipa, kodi ni nyingi mno nchi hii.
 
jamani sisi watumishi wa umma tunalipa kodi mara mbili. ile kwa mshahara na ile kwa dukani.me ntaungana na serikari kuhusu EFDs kama itatufutia kodi mmoja kati ya hizo mbili.

Dawa ni kuwa mfanyabiashara kuepuka kulipa kodi kubwa
 
Back
Top Bottom