Mgomo wa EFDs: Kilichopo nyuma ya pazia. Serikali isimame IMARA

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
EFD2.jpg
Jana wafanyabiashara wa Mwanza walianza kile wanachokiita Mgomo usio na Kikomo kugomea mashine za kutunza kumbukumbu za mauzo na kukadiria ushuru zijulikanazo kama EFD. Pia siku za nyuma tulisikia mgomo wa aina hiyo hiyo Dar na Mbeya. Sababu wanayotumia ni ya msingi sana kuwa hawawezi kununua mashine hizo kwa bei ya shilingi laki nane (800,000=) tena kwa makampuni maalum wakati mashine hizo China zinauzwa dola 50 tu (kama 80,000 za kitanzania) na Kenya ziko madukani kwa retail price ya 150,000Tshs. Hapo TRA inastahili lawama kwa kutumia mfumo CCM ambao kila kunapokuwa na bidhaa mpya watu wanakimbilia kupiga dili, ilitokea kwenye Speed Governer, Plate namba za magari na hata kwenye mikanda usalama ya mabasi. Hapa kuna makandokando yanaoonesha kuna dili inapigwa TRA ndo maana hawataki Biashara huria ya EFD wao kazi yao iwe Calibration tu ya mashine. Pia mashine hizi za bei mbaya pia zinaharibika haraka na wao wateule wanouza wamejipa na dili la kufanya maintenance kwa shilingi kuanzia elfu sitini (60,000) na kuendelea, wakati kiuasilia hizi mashine ni kama Calculator ya kawaida iliyoongezewa akili kidogo tu hivyo hazina gharama kubwa kihivyo kutengeneza. Kumbuka wengine tukipeleka gari garage za ushwahilini kufanya service huwa tunalipa elfu kumi, iweje mashine hizi service au maintenance iwe elfu sitini na kuendelea. Hapo TRA jitazameni, hiyo ni hoja ya wafanyabiashara

Ukweli halisi ni kuwa wafanyabiashara wanachogomea ni KULIPA KODI kwa kuwa hizi mashine zinatunza kumbukumbu vizuri na zinazuia kila aina ya Magumashi ambayo ndio msingi wa biashara nyingi Tanzania. Wakati wa uhamasishaji wa mgomo wa Mwanza, tulielezwa na wachochezi wa huo mgomo kuwa kama zikitumika hizi mashine wafanyabiashara wengi watafilisika kwa maana toka zimeanza kutumika hizi mashine wengi wanalipa kodi kubwa kuliko zamani. Kwa kuwa utamaduni wetu watanzania sio kulipa kodi na serikali haisimamii kisawasawa masuala ya ulipaji kodi (Sijawahi kusikia mtanzania amefungwa kwa kukwepa kodi) wafanyabiashara wameamua kusimama imara kuibabaisha serikali hadi ilegeze uzi tubakie na mfumo wa zamani wa kukwepa kodi. Pia jana simu za pongezi kutoka mikoa mingine zilipigwa kwa wafanyabiashara wa Mwanza kuwa wakaze uzi, wawe ngangari. Pia baadhi ya maafisa wa TRA walikuwa wanahamasisha kichinichini huu mgomo kwa vile matumizi ya hizi mashine yanawanyima ile dili yao iliwafanya wajenge magorofa ya KUKADIRIA KODI. Kwa hiyo kinachopingwa kwenye huu mgomo sio bei ya mashine za EFD, bali ni matumizi ya EFD ili kuendeleza utamaduni wa kukwepa kodi. Bei ni kisingizio tu, nashauri serikali iwanunulie iwape bure kwani itarudisha tu hela zake, ingawa huku Mwanza hata za bure hawataki kama picha hapo juu inavyoonesha

Katika nchi ambayo zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wake hawalipi kodi, ni ndoto kuwa na miundombinu bora, elimu bora, afya bora na huduma zingine. Mama zetu wanalala wanne kitanda kimoja wakati wa kujifungua kwa kuwa pamoja na utawala mbovu wa CCM lakini pia wameshindwa kupata TAX BASE kubwa. Kama chini ya asilimia 20 ya wananchi ndio wanalipa kodi ina maana hao 80% wanatunzwa na hao 20%. Serikali inatakiwa kusimama imara kwenye huu mgogoro kwani matumizi ya EFD ndio future ya biashara Tanzania. Kwa sasa ukwepaji kodi ndio Competitive Advantage ya biashara nyingi, ili upate faida kubwa zaidi lazima uwakwepe/uwahonge TRA usilipe kodi ili uuze bei rahisi, wakati umefika serikali kuwa imara. Waacheni wafanyabiashara wafunge maduka hadi panya wamalize bidhaa za dukani, njaa zikiwauma watafungua tu. Pia ulinzi uimarishwe kwa wafanyabiashara walio tayari kulipa kodi na kutumia EFD kwa kuwa zinazuia kuibiwa pia.

EFD1.jpg
 
Kimilidzo

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
1,346
1,225
View attachment 129543

View attachment 129539

Serikali hii ya MIZIGO kamwe hawezi kununua EFD na kuwapa bure wafanyabiashara, hapo wameishika pabaya. Nasema wagome Tu, tumechoka
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Serikali hii ya MIZIGO kamwe hawezi kununua EFD na kuwapa bure wafanyabiashara, hapo wameishika pabaya. Nasema wagome Tu, tumechoka

Mkuu tuungane na serikali katika hili, hawa wafanyabiashara wanataka ku Blackmail serikali kwa maslahi yao binafsi. Lazima walipe kodi, mbona wafanyakazi wanakatwa juu kwa juu na hawajawahi kugoma na kodi wanayolipa ni kubwa kwa asilimia kuliko za wafanyabiashara
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,913
1,225
Wasituletee mambo yao ya ajabu walipe kodi hakuna cha bure hapa tumechoka kuibia taifa letu wenyewe.
 
Emanuel14

Member
Sep 7, 2013
32
0
View attachment 129543
Jana wafanyabiashara wa Mwanza walianza kile wanachokiita Mgomo usio na Kikomo kugomea mashine za kutunza kumbukumbu za mauzo na kukadiria ushuru zijulikanazo kama EFD. Pia siku za nyuma tulisikia mgomo wa aina hiyo hiyo Dar na Mbeya. Sababu wanayotumia ni ya msingi sana kuwa hawawezi kununua mashine hizo kwa bei ya shilingi laki nane (800,000=) tena kwa makampuni maalum wakati mashine hizo China zinauzwa dola 50 tu (kama 80,000 za kitanzania) na Kenya ziko madukani kwa retail price ya 150,000Tshs. Hapo TRA inastahili lawama kwa kutumia mfumo CCM ambao kila kunapokuwa na bidhaa mpya watu wanakimbilia kupiga dili, ilitokea kwenye Speed Governer, Plate namba za magari na hata kwenye mikanda usalama ya mabasi. Hapa kuna makandokando yanaoonesha kuna dili inapigwa TRA ndo maana hawataki Biashara huria ya EFD wao kazi yao iwe Calibration tu ya mashine. Pia mashine hizi za bei mbaya pia zinaharibika haraka na wao wateule wanouza wamejipa na dili la kufanya maintenance kwa shilingi kuanzia elfu sitini (60,000) na kuendelea, wakati kiuasilia hizi mashine ni kama Calculator ya kawaida iliyoongezewa akili kidogo tu hivyo hazina gharama kubwa kihivyo kutengeneza. Kumbuka wengine tukipeleka gari garage za ushwahilini kufanya service huwa tunalipa elfu kumi, iweje mashine hizi service au maintenance iwe elfu sitini na kuendelea. Hapo TRA jitazameni, hiyo ni hoja ya wafanyabiashara

Ukweli halisi ni kuwa wafanyabiashara wanachogomea ni KULIPA KODI kwa kuwa hizi mashine zinatunza kumbukumbu vizuri na zinazuia kila aina ya Magumashi ambayo ndio msingi wa biashara nyingi Tanzania. Wakati wa uhamasishaji wa mgomo wa Mwanza, tulielezwa na wachochezi wa huo mgomo kuwa kama zikitumika hizi mashine wafanyabiashara wengi watafilisika kwa maana toka zimeanza kutumika hizi mashine wengi wanalipa kodi kubwa kuliko zamani. Kwa kuwa utamaduni wetu watanzania sio kulipa kodi na serikali haisimamii kisawasawa masuala ya ulipaji kodi (Sijawahi kusikia mtanzania amefungwa kwa kukwepa kodi) wafanyabiashara wameamua kusimama imara kuibabaisha serikali hadi ilegeze uzi tubakie na mfumo wa zamani wa kukwepa kodi. Pia jana simu za pongezi kutoka mikoa mingine zilipigwa kwa wafanyabiashara wa Mwanza kuwa wakaze uzi, wawe ngangari. Pia baadhi ya maafisa wa TRA walikuwa wanahamasisha kichinichini huu mgomo kwa vile matumizi ya hizi mashine yanawanyima ile dili yao iliwafanya wajenge magorofa ya KUKADIRIA KODI. Kwa hiyo kinachopingwa kwenye huu mgomo sio bei ya mashine za EFD, bali ni matumizi ya EFD ili kuendeleza utamaduni wa kukwepa kodi. Bei ni kisingizio tu, nashauri serikali iwanunulie iwape bure kwani itarudisha tu hela zake, ingawa huku Mwanza hata za bure hawataki kama picha hapo juu inavyoonesha

Katika nchi ambayo zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wake hawalipi kodi, ni ndoto kuwa na miundombinu bora, elimu bora, afya bora na huduma zingine. Mama zetu wanalala wanne kitanda kimoja wakati wa kujifungua kwa kuwa pamoja na utawala mbovu wa CCM lakini pia wameshindwa kupata TAX BASE kubwa. Kama chini ya asilimia 20 ya wananchi ndio wanalipa kodi ina maana hao 80% wanatunzwa na hao 20%. Serikali inatakiwa kusimama imara kwenye huu mgogoro kwani matumizi ya EFD ndio future ya biashara Tanzania. Kwa sasa ukwepaji kodi ndio Competitive Advantage ya biashara nyingi, ili upate faida kubwa zaidi lazima uwakwepe/uwahonge TRA usilipe kodi ili uuze bei rahisi, wakati umefika serikali kuwa imara. Waacheni wafanyabiashara wafunge maduka hadi panya wamalize bidhaa za dukani, njaa zikiwauma watafungua tu. Pia ulinzi uimarishwe kwa wafanyabiashara walio tayari kulipa kodi na kutumia EFD kwa kuwa zinazuia kuibiwa pia.

View attachment 129539

Acha wagome tu maana hata hiyo kodi kidogo wanayopata hawaitumii ipasavyo. Hopitali hazina dawa, umeme sio wa uhakika, barabara mbovu basi taabu tu, wao kila siku tuongeze kodi kwa manufaa yao na familia zao. Mgomo uendeleee,
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,913
1,225
Mkuu tuungane na serikali katika hili, hawa wafanyabiashara wanataka ku Blackmail serikali kwa maslahi yao binafsi. Lazima walipe kodi, mbona wafanyakazi wanakatwa juu kwa juu na hawajawahi kugoma na kodi wanayolipa ni kubwa kwa asilimia kuliko za wafanyabiashara
Ni kweli mkuu hili ndiyo tatizo la wafanyabiashara wetu huu ni wakati wa kulipa kodi udanganyifu basi tena.
 
Ungekuwa mzima usingeongea haya lakini kwa vile unaumwa endelea lakini fahamu maendeleo ya nchi hayaji kwa migomo na kukwepa kulipa kodi.
 
bategereza

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
3,316
0
Ni kweli mkuu hili ndiyo tatizo la wafanyabiashara wetu huu ni wakati wa kulipa kodi udanganyifu basi tena.

Serikali ianze kwa kurekebisha wafanyakazi wa mamlaka ya mapato . tuanze kwa kumwondoa Kamishna jerero. huyu mtu ana zaidi ya miaka stini. unakaa pale TRA kwa manufaa ya nani. kubebabeba vibabu kazini kunawanyima vijana ajiraaaa
 
mikogo

Senior Member
Jul 24, 2011
175
225
Hii ni dunia ya digital hakuna magumashi. Wafilisike ili kila mwenye bishara aonyeshe uwezo wake halisi. Na sio kukwepa kwepa kodi.
Funga duka kalime
 
Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,564
2,000
UKWELI NI KWAMBA MASHINE HIZO WANAPEWA BIRE KWANI FEDHA AMBAZO WAFANYABIASHARA WATATUMIA KUNUNULIA HIZO HIZO MASHINE ZINARUDISHWA WAKATI WAKIWA WANAFANYA MAREJESHO YAO YA KODI YA KILZ MWEZI. Sasa hapo tatizo ni nini. Labla ninalolionamimi ni kuwa wanasiasa wetu wana politisize kila jambo. Mashine hizo zina faida kubwa sana kwa upande wa uboreshaji wa sector ya kodi. Ni mfanya biashara zsiye makkini pekke ndiye atakayekataa kutumia mashine hizo. Kwawaliomakini huwasaidia ktk kutunza kumbukumbu za biashara zao.
 
bluecolour

JF-Expert Member
May 20, 2013
202
225
Mtoa Mada Tafadhali UCPOTOSHE UMMA: Kama Hujui Sababu Ya Mgomo Ni Bora Ukanyamaza... Nianze Na Hili La Bei Umesema Katika Post Yako Dubai Ni US50/TSH ELEU 80 TU. Ukatoatoa Mfano Kenya Ni Tsh 150,000= Pamoja Na Kutokuwa Sahihi Bei Zako Je Wewe Unaweza Nunua Kitu Cha Elf 80 Kwa Laki Nane?? Na Kama Tatizo Ni Mashne Kwann Wasiruhusu Wafanyabiashara Waagize/wanunue Wenyewe Sehemu Wanayotaka??? Je Ni Kwann Walazimishe Service Ya Mashine Iwe Elf 60 Hata Kama Ni Kubadilisha Karatasi Zikiisha??? Hv Mazingra Kama Haya Ndg Yangu Wewe Unayaona Ni Sahih Mpaka Wafanyabiashara Wakubali Wizi Huu Wa Kimachomacho Wanaofanyiwa Na Serikali Yao Kumbuka Kuna Wegne Wamekopa Kwa Wizi Huu Lazima Watafungwa LAKIN Kubwa Kumbuka Mfanyabiashara Hana Hasara Maumivu Ya EFDs Atakaye Yabeba Ni Mimi Na Wewe Mimi Nilifikiri Tunawasaidia Wafanyabiasha Kudai Hili Ili Unafuu Upatikane Kwetu WALAJI.. Msimamo Huo Ungeiambia Serikali Na Misamaha Ya Kodi Kwa Makampuni Makubwa Na Ya Nje Wewe Unashadadia Walalahoi Wenzako... Buushit
 
sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,284
1,195

wanamjua Blandina Nyoni wanamsikia?

Hahah! na yeye anaijua Blinded Nyomi au anaisikia?

Nway,
ishu sio EFD mashine au kulipa/kutolipa kodi.. Ishu ni dhamira ya kufanya lolote kati ya hayo haipo..

Tabaka kubwa la walionacho na wasionacho ndio tatizo. Na hili tabaka limesababishwa na rushwa, wizi na ufisadi uliotamalaki, miongoni mwa viongozi wenye dhaman!

So ni ngumu kumshawishi mfanyabiashara asikwepe kodi wakati anamuona kiongozi wake (kisiasa au kiserikali) ndani ya miaka miwili ana majumba mengi ya gharama na mali nyingi, wakati mshahara hauzidi milioni.. Hapo hapo anasikia pamoja na kujikusanyia zaidi ya milioni 12 na marupurupu kibao kwa mwezi, bado mbunge halipi kodi.. Hujamtaja rais na wakubwa wengine..

So, serikali isipotibu the root cause, hakuna kitakachofanyika. Sana sana ni kuchochea vurugu tu.. Mind u chadema wameshapata hoja nying za kuingia ikulu!
 
Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,797

HUyo mama Blinded Nyomi (lol) Blandina Nyoni ni hatare kwa afya ya taifa hili..kila mahala anapokua lazima akinukishe!

Serikali imewasafisha aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo huku ikimpandisha cheo aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali Deo Mtasiwa.

Nyoni alisimamishwa kazi pamoja na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa na wote kwa pamoja walikuwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao wakiwa watumishi wa umma.

Jairo kwa upande wake alisimamishwa kazi kutokana na kuchangisha fedha kinyume cha sheria kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha bajeti ya wizara yake, katika mwaka wa fedha 2011/2012 na sasa ameondolewa kwenye utumishi wa umma, huku Bunge likiwa bado halijapata taarifa ya utekelezaji wa maazimio yanayomuhusu.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyoni kwa sasa amerejea kwa mwajiri wake wa awali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akishikilia nafasi ya mmoja wa wakuu wa idara, huku Dk Mtasiwa akiwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Katibu Mkuu Kiongozi
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amelithibitishia gazeti hili kuhusu watumishi hao na kwamba taratibu zimefuatwa.

"Mimi ninachojua ni kwamba Blandina alikuwa mwajiriwa wa TRA na mkataba wake ulikuwa haujaisha… Siyo kwamba alikuwa na mikataba miwili, kwenye utumishi wa umma huwa kuna utaratibu wa kuazima watumishi wa umma.
Ndiyo maana unaweza kukuta mwanajeshi anatolewa jeshini na kupelekwa uraiani au mtumishi kutoka idara moja kwenda nyingine. Kwa upande wetu sisi tulishamwondoa kwenye ukatibu mkuu na kule TRA hakuwa na tatizo," alisema Balozi Sefue.

Kuhusu Dk Mtasiwa alisema: Uteuzi wa Dk Mtasiwa ulikuwa wazi na hata alipoapishwa mambo yote yalitangazwa hadharani." Aliendelea kufafanua kuhusu Jairo akisema: "Jairo alishaondolewa kwenye ukatibu mkuu, siyo mtumishi tena wa umma." Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alimtetea Nyoni akisema kuwa amerudi kwenye ajira yake ya awali.

"Siyo kwamba ameajiriwa TRA, amerudi tu kwenye ajira yake ya zamani, alikuwa akifanya kazi hapa akaazimwa na sasa amerudi," alisema Kayombo na kuongeza: "Kwani amefanya kosa gani? Kuna mashtaka yoyote aliyofanya unaweza kuyathibitisha?"

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Bernard Mchomvu ambaye alisema Nyoni alishasafishwa na Serikali ndiyo maana wamempokea. "Yule aliazimwa tu na Serikali…Sasa kama Serikali imesham-clear sisi tutamkataaje?" alihoji na kuongeza:

"Kwa sababu sikumwomba huyo mtu, nimeambiwa kwamba huyo yuko safi mimi nifanyeje? Unajua watu wanafurahia wengine wakipata matatizo, hata kama mtu ameua, basi walete ushahidi. Hata unaposema nchi imejaa rushwa, ulete ushahidi… kama Serikali imeshamsafisha, ningemkataa ningekuwa mtu wa ajabu."

Jitihada za kumpata Nyoni kupitia simu yake ya mkononi hazikuzaa matunda, baada ya simu yake kupokelewa na sauti ya kiume iliyosema kuwa namba imekosewa.

Hata alipotafutwa kwa namba nyingine, simu ilipokelewa na mwanamke aliyejitambulisha kama mfanyakazi wa Wizara ya Afya na kwamba namba hiyo kwa sasa haitumii tena. Alipotafutwa kwa njia ya simu, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah, alisema suala hilo aulizwe msemaji wa Serikali juu ya Bunge.

"Ongea na msemaji wa Serikali juu ya mambo ya Bunge," alijibu kwa njia ya ujumbe wa simu.
Lukuvi

Naye Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hayuko ofisini.

"Niko ‘airport' nasafiri kwenda South Africa, msinipigie simu, siko ofisini hadi mwezi ujao (Januari)," alisema Lukuvi na kukata simu yake.
Awali alipoulizwa kwa njia ya simu baada ya mwandishi kuelezea suala hilo alisema ana kazi nyingi na kwamba apigiwe baadaye.

Makani azungumza
Mwenye wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza tuhuma hizo, Ramo Makani, ambaye pia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, akizungumza na gazeti hili kuwa: "Ni kweli mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza suala hilo, kwa utaratibu kamati kama hiyo huundwa kwa kanuni za Bunge kwa kupewa majukumu maalumu… Kama mbunge tu ningefurahi kusikia taarifa ya Serikali bungeni baada ya kupata taarifa ya Bunge," alisema Makani na kuongeza:

"
Serikali iliahidi kuleta taarifa bungeni ya utekelezaji wa maagizo ya Bunge. Mimi sikumbuki kama taarifa hiyo imeshasomwa bungeni, labda wewe mwenzangu umebahatika kuisikia. Kwa hiyo bado tunasubiri… Kama Serikali imechukua hatua, mimi sijui."

Tuhuma za Nyoni

Nyoni alituhumiwa kutenda makosa saba ambayo yaliainishwa wakati wa mgomo wa madaktari ulioanza Januari mwaka jana, hali iliyomlazimisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kutangaza kumsimamisha kazi ili uchunguzi uweze kufanyika.

Baadhi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili ni pamoja na kujilipa mshahara wa ziada kupitia Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) nje ya mshahara aliokuwa akilipwa na Serikali, kutengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na ofisa ununuzi wake kwa kujiweka yeye mwenyewe.

Tuhuma nyingine zilikuwa kulazimisha Wizara ya Afya kununua sare za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za ununuzi.

Katika mikutano yote inayofanyika wizarani, alikuwa akilazimisha Kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa zabuni ya kutoa huduma ya chakula kwa washiriki tangu alipotua wizarani kama Katibu Mkuu.

Sakata la Jairo

Hatua ya kumwondoa Jairo katika utumishi wa umma nayo imefanyika kimyakimya kwani Serikali hadi sasa haijawasilisha bungeni majibu ya maazimio ya Bunge kuhusu sakata hilo ambalo pia liliwagusa watumishi wengine wa Wizara ya Nishati na Madini. Maazimio hayo ni yale yaliyotokana na matokeo ya uchunguzi wa Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Makani na kubainisha kuwapo kwa makosa ya kiutumishi na kijinai ambayo yangewafikisha baadhi ya watumishi hao katika vyombo vya sheria.

Mbali na Jairo, kamati hiyo ilipendekeza kuwajibishwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

Hata hivyo, ni Jairo pekee kati ya hao aliyewajibishwa kwa kusimamishwa kazi na baadaye kuondolewa katika wadhifa wake. Luhanjo alistaafu utumishi wa umma bila kuchukuliwa hatua zozote wakati Utouh anaendelea na wadhifa wake.
Pia katika taarifa yake, Kamati Teule ilisema utaratibu wa uchangishaji wa fedha Sh418.081 milioni uliofanyika katika Wizara ya Nishati na Madini haukuwa na uhalali kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni za Fedha za Umma.

Pamoja na mambo mengine, Bunge liliazimia kwamba ufanyike ukaguzi wa kiuchunguzi (forensic audit) kwa matumizi ya Sh214 milioni, ambazo kati ya hizo Sh126 milioni Kamati Teule ilikataa maelezo ya matumizi yake na Sh88 milioni ni zile zinaotajwa kwamba zilitumika katika kugharimia semina kwa wabunge.

Azimio jingine ni lile lililoitaka Serikali iviagize vyombo vya dola kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za kughushi na ubadhirifu zilizoelezwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kama ilivyoelekezwa.
Baada ya kufikiwa kwa maazimio hayo, Serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe iliahidi kuyafanyia kazi na kuwasilisha majibu bungeni.

"Kwa sababu ya ukubwa na uzito wa taarifa hii, ni vigumu kuitolea majibu yote hapa hapa, ninachoweza kufanya ni kuipokea pia tutakapokuja katika Mkutano wa Sita, tunatarajia kuleta majibu ya hoja zilizomo kwenye taarifa hii," alisema Chakawe ambaye sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria.
 
Kozo Okamoto

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
3,397
2,000
Mkuu tuungane na serikali katika hili, hawa wafanyabiashara wanataka ku Blackmail serikali kwa maslahi yao binafsi. Lazima walipe kodi, mbona wafanyakazi wanakatwa juu kwa juu na hawajawahi kugoma na kodi wanayolipa ni kubwa kwa asilimia kuliko za wafanyabiashara

samahani mkuu uko sober kweli?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom