Mgomo wa Dalala Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Dalala Morogoro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, May 20, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wana JF inasemekana kuna mgomo wa Daladala yaani yale magari yanayotumika kusafirishia abiria ndani ya Manispaa ya morogoro,mgomo huo ni wa siku mbili

  kwa aliye morogoro anaweza kutujuza nini chanzo ama sababu za mgomo huo?
   
 2. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Manispaa wanataka kuchukua ushuru wa shs 300.00 kwa kila tripu ya daladala. (average ya Shs 2400.00 kwa kila daladala inayoingia kituoni kubeba abiria. Madereva wanadai hii inawapunguzia posho yao kwa vile wenye magari yao wanataka kipande kilekile na wakati bei ya mafuta imepanda kwa hiyo mwisho wa siku hawaondoki na kitu.
  My take: Uongozi wa manispaa ubuni vyanzo vingine vya mapato siyo kwa magari kwa wakati huu gharama za mafuta na vipuru viko juu sana ama sivyo Wananchi ndio watakaoteseka na wawachukulie Wenye daladala kama ni washirika wenzao wa kutoa huduma muhimu kwa jamii badala ya kuwachukulia kama njia ya kuwakamua na kuwatafutia fedha za matumizi ya kuendesha gharama za Manispaa.
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Uvivu wa kufikiria kwenye halmashauri zetu. Hivi hawana vyanzo vingine kweli..... Sasa utashangaa bei za kupangisha vibanda zilivyochini wakati middle men wanafaidika wao wanang'ang'ana na kuongeza ushuru wa magari!!! Serikali hii ya Kikwete imechoka kila Idara kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa.
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280

  Kaka MAGAFU,kumbuka kuna halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA...na hali ni kama au zaidi ya halmashauri ya morogoro....!
  Ila ni kweli kuwa halmashauri zetu zote (PASIPO KUJALI ZINAONGOZWA NA CHAMA GANI) zibuni vyanzo vya mapato ambavyo haviumizi
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Engineer sio kama vyanzo vya mapato havipo,vipo lakini mapato hayo yanakwenda mifukoni mwa watu na sio ktk Acc za halimashauri,kwa mfano hizo stand zote tatu pale morogoro ni vyanzo vizuri sana vya mapato,ukianzia ile ya soko kuu,ile ya mjini na msavu,lakini siku mvua zikinyesha kunastand huwezi kupita ni matope kama vile ziko vijijini,je hizo pesa wanazochukuwa ktk maegesho ya magari zinakwenda wapi?

  Nadhani uwajibikaji haupo,kila mtu anafikilia mfuko wake tu,pasipo kuangalia jamii kwa ujumla na Taifa
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  wamefuta kodi kwenye madini halafu wanazidisha kodi kwenye wananchi, kwanza hiyo pesa wakiipata wanaipeleka wapi kama sio kuila,
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  MTAKATIIFU IVUGA....! NYERERE aliwahi sema (MIMI HUSIKILIZA HOTUBA ZA HUYU MZEE MARA KWA MARA TBC SAA MBILI NA ROBO USIKU)
  Serikali corrupt haikusanyi kodi...inaishia kukimbizana na watu wadogowadogo.....! KODI KWENYE MADINI ...AMBAPO WAMILIKI WA MACHIMBO NI MABILIONEA INAACHA ....halafu inakusanywa ya vijitu ambavyo mtaji wake haufiki TSH 3,500 ni fedheha
  HALAFU WAKTU WAKIANDAMANA TUNAWAITA WALETA FUJO........?! SHAME ON LAW MAKERS....SHAME ON LAWS...SHAME ON LAWYERS....! SHAME ON YOUUUU
   
 8. k

  kituro Senior Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  pamoja na ushuru wa shilingi mia tatu pia wanalalamikia matumizi ya hiyo pesa mfano daladala ziendazo chamwino, mzinga, SUA na maeneo jirani na hayo niliyoyataja huwa zinapaki sokoni ambako wakati wa mvua huwa kunakuwa na tope mpaka abiria kuingia standi hiyo ya sokoni inakuwa shida. stendi inakuwa matope matupu utazani unafyatua matofari kama siyo kupanda mpunga wa majarubani.
   
Loading...