Mgomo UDSM wafanyakweli

AK-47

JF-Expert Member
Nov 12, 2009
1,373
199
Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha DSM wameamua kuanza mgomo usiokua na kikomo kupinga mafao duni pamoja na madai mengine. Kazi imebaki kwetu wafanyakazi ifikapo Mei tano kumfunga paka kengele.
 
"....Silaha ya Mnyonge ni umoja...!
 
hivi tusio na vyama vya wafanyakazi kulingana na saizi ya mashirika tufanye aje ili tugome??????????
 
Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha DSM wameamua kuanza mgomo usiokua na kikomo kupinga mafao duni pamoja na madai mengine. Kazi imebaki kwetu wafanyakazi ifikapo Mei tano kumfunga paka kengele.

Nilkuwa napenda sana migomo.....nawapongeza sana ! Vipi jamaa wa MUHAS, SUA na Mzumbe?
 
Kazi sana hii Tanzania yetu, kama Mhadhiri anagoma eti mshahara mdogo je yule Karani masjala pale Wizara ya Uvuvi si itakuwa balaa. Mungu ibariki Tazania.
 
Hongera UDSM, vipi wengine I hope na wao wameunga mkono. Serikali imezidi siasa bila matendo!!
 
Kazi sana hii Tanzania yetu, kama Mhadhiri anagoma eti mshahara mdogo je yule Karani masjala pale Wizara ya Uvuvi si itakuwa balaa. Mungu ibariki Tazania.

Mkuu sina uhakika umetumia vigezo gani ili kuweza kuwalinganisha mwenye haki ya kugoma kati ya mhadhiri na karani wa masijala. Ungewatendea haki iwapo ungetumia vigezo mfano muda wa kufanya kazi, aina ya kazi, ukubwa wa kazi, kiasi cha mshahara na vigezo vingine ili uweze kufikia hitimisho ya yupi anastahili au asiyestahili kugoma.
 
Umesahau muda aliohangaika kutafuta hiyo shule iliyomwezesha kupata hicho kibarua. Mtu aliepiga shule kwa miaka 4 na labda akaambulia "D" 2 au 3 huwezi kumlinganisha na mtu aliyesoma hadi wajukuuu wakamkuta shule. Na bado anaendelea kukata shule kila siku ili kuwapatia maarifa vijana. Hawa watu hawawezi kulinganishwa kwa kitu chochote (ni kama maji na mafuta). Ni upuuzi wa nchi yetu unaowafanya waonekane kama wa hovyo hovyo wakati nchi zenye akili hawa wataalamu ndio injini ya uchumi!
 
Back
Top Bottom