Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Hapa mkuu Paskali hukututendea haki members na hususani tunaofuatilia mabandiko yako.
Uweke hapa hizo sababu hata kama wewe kuziamini wacha tuzipime pia na sisi.
Ningependa kujua pia kama baada ya maono yako juu ya Magufuli uliyemuhofia ndiye huyu ama ala?
 
Ukimuendea chemba atakuambia kanisa katoliki ndo limeamua
 
Hapa mkuu Paskali hukututendea haki members na hususani tunaofuatilia mabandiko yako.
Uweke hapa hizo sababu hata kama wewe kuziamini wacha tuzipime pia na sisi.
Kuna vitu hata ukivijua hupaswi kuvisema kwa sababu once ukishavisema then the damage is irreversible!.

Mfano mmepata mgeni, wa kike mchumba wa mtoto wenu, akatayarishiwa chumba cha wageni, akalala. Asubuhi akadamka kwenda kuoga huku nyuma mawifi wakaja kumuamsha walipomkuta bafuni wakaamua kumtandikia kitanda. Wakakuta tandiko limeloa mkojo, wakaconclude wifi yao ni kikojozi. Taarifa ikafikishwa kwa mama mkwe, wakaamua uchumba uvunjwe hakuna tena ruhusa ya kijana wao kuoa kikojozi!.

Mtoto wa watu akafungashwa virago vyake akarudishwa kwao asubuhi hiyo hiyo, kosa ni kikojozi!.

Masikini mtoto wa watu aliangua kilio na alipofika kwao familia nzima waliangua kilio na mijitu ya miraba miine ilivamia zizi, na kuchukua ng'ombe wa mahari ili kurejesha mahari.

Baada ya hayo kufanyika. Jioni walipokuwa wanakula, kuna mtoto mdogo wa miaka mitano ambapo hapo ni kwa bibi akawa anamuulizia yule mgeni wa jana. Akaulizwa unamtafutia nini, ndipo mtoto akasema anamtafuta kumuomba msamaha usiku alipitiwa na usingizi hivyo kukojoa kitandani akaamka mapema na kuhamia chumba kwa dada!.

Vipi mtarejea ukweni kuomba msamaha na uchumba uendelee?. Kuna vitu ukivijua they are better kept close than let loose.

Paskali
 
Mkuu Paskali,kwa maslahi mapana ya taifa hakuna namna hata kama kutakuwa na damage ama imeshapatikana,ni kutuachia legacy ya kuwa alitokea mtu mmoja paskali maandishi yake yalikuwa ni ya weledi sana,pengine kwa muda ambao umebakiwa nao hapa duniani tuwe na tahadhari kubwa pale utakapoweka angalizo.
Ungetuwekea sababu ulizobaki nazo naamini ungeacha mafunzo kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Lakini sio mbaya,hili nalo limepita hakuna namna tena.
 

Uliona mbali.
 

Hauwezi kuvunja uchumba kwasababu ya kukojoa kitandani. Tafuta sababu nyingine ya kutufunga mdomo.
 
Katika vitu walivyokosea CCM ni kumpa huyu MTU uraisi watajuta sana.Siasa kwa sasa imebadilika ipo kwa vijana sana sasa kama unatengeneza mazingira mabovu kwa vijana kama anavyofanya huyu bwana ajira hakuna na mengineyo ur wrong way to go.
 
Mkuu Mpalakugenda, kwenye fani ya uandishi kuna kitu kinaitwa responsible journalism ambapo mwandishi yoyote makini anapaswa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwanza, hivyo kabla hujaandika taarifa fulani hata kama ni kweli, then unajiuliza jee nikiiripoti ina maslahi kwa taifa?!.

Mfano wakati wa Mwalimu Nyerere kulitolewa tip kuwa ni Mtutsi. Mkapa akatolewa tip ni Mmakonde wa Nchumbiji. Hata kama unampata mtu anayekupa uthibitisho kuwa tip hizo ni za kweli, a responsible journalist hawezi kuandika hayo kwa sababu sio habari za kujenga bali kubomoa.Hivyo unaachana nazo.

Natolea tuu mfano, ikitokea mimi mwandishi nimepewa a tip fulani kuwa wewe Mpalakugenda asili yako haswa ni Mhutu, au ni Banyamulenge, hukuzaliwa Tanzania na wala wazazi wako sio Watanzania, bali ulizaliwa huko ulikozaliwa, kisha wewe na wazazi wako mkahamia Tanzania ukiwa mdogo, ukakulia Tanzania, ukasomea Tanzania, ukazungumza lugha ya wenyeji wa hapo ulipokulia na ukahesabika ni Mtanzania. Ikitokea ukachaguliwa nafasi muhimu, jee ni busara kwa mimi kama mwandishi kuandika habari za asili yako wewe Mpalakugenda?.

Nikiiripoti story ya kuwa wewe ni Mhutu na sii Mtanzania asili, habari hiyo itakuwa ni ya kujenga au kubomoa?. Na nikiiripoti kuwa ni Mhutu, taarifa ya Uhutu wako ina maslahi kwa taifa?. Ukiishapima na kuiona haina maslahi kwa taifa, then unaachana nayo!.

Vivyo hivyo lets practice responsible journalism hii kitu tuachane nayo haina maslahi kwa taifa.

Paskali
 
Sawa Paskali,nakubaliana kutokukubaliana. Sasa naelewa ndio maana kuna wenzetu hawaoni shida kufanya mikataba ya kiujanja ujanja inayoligharimu taifa. Ingawa hii pia sio wote wanaweza kuwa hivyo.
 
Sawa Paskali,nakubaliana kutokukubaliana. Sasa naelewa ndio maana kuna wenzetu hawaoni shida kufanya mikataba ya kiujanja ujanja inayoligharimu taifa. Ingawa hii pia sio wote wanaweza kuwa hivyo.
Kukubaliana kutokubaliana ndio ustaarabu wa mijadala.

P.
 
angekuwa gwajima asingejali!
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…