Elections 2010 Mgombea wa Chadema ahongwa milioni 60

mbona hiyo habari kwenye mwananchi sijaiona? mwananchi ya leo sio?

Mkuu, ujaona kichwa cha habari "Mgombea ubunge Chadema arudi CCM" ? Kama umesoma majibu yangu vizuri kwa huyo mdau aliyetaka nifanyie upalelezi chanzo changu cha habari utakuwa umenielewa nacho sema hapa.
 
hawa sisi tuliwaambia wakabisha na kuja na nahau nyingi.

ooh mtu akihamia CHADEMA huwa makini jee mtu huyo huyo akitoka CHADEMA jee? mbona mnadouble standard

kwa nn isiwe ni kweli makini ila kaona chama hakiko makini kaamua kugura
 
Niliwahi kusema hapa kwamba KOSA ambalo chadema wanalifanya ni kuwaamini wanaojiunga na chama hicho ktk kipindi cha lala salama ya uchaguzi. Walipaswa kumpokea na kuanza kummezesha maji yenye sabuni za chadema awe msafi kisha apewe jimbo.
Tusikimbilie madaraka tukidhani ndo suluhisho la mwisho.
Dawa ni kujipanga na kuamini timu uliyo nayo haitakuangusha.
Poleni chadema
Msanii kuna ukweli fulani katika maelezo yako! Lakini kumbuka viongozi wa siasa karibu wote Afrika wako kwa ajili ya maslahi yao. Hata mtu akae miaka 20 kwenye chama sio qurantee kuwa anaamini falsafa na sera za chama. Mambo yalivyo sasa ni kama kurusha shilingi... hujui inaangukia wapi! Afrika itaendelea kuteseka hadi hapo sisi wenyewe tutakapokubali kubadilika!!
 
Kikwete amewaambia kwamba uchaguzi ni sawa na vita, kwenye vita kama inavyojulikana si lazima utumie mbinu halali hata mbinu haramu zinarushusiwa. Hiyo ndo Tz yetu
 
Kikwete amewaambia kwamba uchaguzi ni sawa na vita, kwenye vita kama inavyojulikana si lazima utumie mbinu halali hata mbinu haramu zinarushusiwa. Hiyo ndo Tz yetu

Watu walioendelea hata vitani wanapigana kwa sheria, ndiyo maana kuna Geneva Convention. Sasa kama unataka kutuambia Kikwete ni barbarian ambaye haelewi hili, sawa.
 
Watanzania, hatuna haja ya kushtushwa na hao mafisadi kwani mwishowaoo ni october 30, wananchi hawadanganyiki tumechoka wala hatutaki kusikia ccm iko madarakani. Kama wataendelea kutawala basi watakuwa wanataka kutuingiza kwenye matatizo zaidi na kutakuwa na vuguvugu la hali ya hatari muda wote.

We all need the changes whether you are in CCM or Chadema au CUF or whatever. Hakuna anayependa kuona mama zetu wakilala chini pale mwananyamara hospitali wakati tatizo ni watu tuliowapa dhamana siwabunifu, yule sawa kakimbia bora kawahi mapema. Tunasonga mbele haturudi nyuma. PEOPLES POWER ina ari kubwa na inatisha kila sehemu.

Tunahitaji kubwa la mabadiriko na mambo mafanikio hayaji kirahisi, ndo kama hivi wenye kushindwa kuvumilia wanaachia kasi ipite.

Watu
 
Watu walioendelea hata vitani wanapigana kwa sheria, ndiyo maana kuna Geneva Convention. Sasa kama unataka kutuambia Kikwete ni barbarian ambaye haelewi hili, sawa.

Great Post!

Kama, na kama habari hii yote ni ya kweli, basi sheria ya uchaguzi iangaliwe upya. Kwani jambo hili kutokea linaonesha mapungufu mengi katika kusimamia demokrasia ya kweli.

Kuhama chama ni jambo la kawaida, maana watu hubadilisha misimano na malengo yao kulingana na yale wanayoamini, misimamo yao na yale wanayo kukutana nayo ndani ya chama. Lakini si hoja kubwa kulinganisha na uvurugaji wa sheria kama zipo kulinda uhamiaji wa kiholela wa wagombea. Ni mithili ya transfer window kwenye league za ulaya; wachezaji wanaweza kuhama wapendavyo ndani ya kipindi kilicho idhinishwa, muda ukipita transfer zote zinasimamishwa.

Katika hili, mimi nadhani sheria iweke ku-limit kipindi ambacho mgombea anaweza kuhama toka chama kimoja hadi kingine pale kampeni zinapoanza. Na pale zinapoisha, mgombea huyo kama amesha utwaa ubunge akihama, uchaguzi mdogo wa jimbo unafatia. Ili kuruhusu watu kuchagua mtu na chama wapendacho kulingana na sera zilizopo na maono yao.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba, sheria zetu bado haziruhusu wagombea binafsi, na mgombea mmoja kuhama wakati wa kipindi cha kampeni ambapo kura za maoni zimeshapita na kipindi cha kupitisha wa wakilishaji wa chama kimefungwa, kunaweka disadvantage kwa chama pinzani na demokrasia kiujumla.

Nionavyo hili ni sawasawa na swala lile la kupita bila kupingwa. Kwani itatokea watu wanafanya makusudi kuhamia chama kimoja wakati wakiwa wamekula njama na chama fulani, ili pale kipindi cha kuteua wawakilishi wa chama kinapofungwa, basi mgombea huyo anahama chama kwenda kingine na kukiacha kingine bila mwakilishi.
 
Steve-Dii

hivi vyama vya upinzani vilitakiwa vizingatie suala hilo mapema sana. Vili gamble na imeanza kula kwao.

tunaambiwa kuwa zitto kabwe yeye binafsi alienda kuwaomba hao 'walio onewa' kwenye ccm, kujiunga na chadema na baadae kuwapa nafasi ya kugombea majimbo.

Hii mimi inanionyesha dhahiri kuwa hao wahamiaji kwenye vyama vya upinzani hawajahamia kwa kupenda sera au muongozo wa upinzani bali kama njia ya kuikomoa ccm.
Wakipewa pesa ndio haooo wanaondoka bila ya kutizama nyuma kwa kuwa mapenzi tokea hapo mwanzo hayapo.
 
Steve,

Ingawa natetea utawala wa sheria kwa jumla, nisingependa kuona demokrasia inakabwa koo na sheria.Nisingependa kwa mfano, kuwe na minimum qualification ya kuwa mbunge iliyokuwa based on formal education. Ningependa vyama vyenyewe vituonyeshe vinathamini formal education kiasi gani, na nisingependa watu wenye exceptional talents lakini wasio na formal education wafungiwe mlango wa uongozi.

Binafsi nisingependa sheria ziingilie sana demokrasia, sheria zikiingilia sana demokrasia tunaanza kuipooza demokrasia.

Mimi nisingetaka kuwe na sheria ya nchi kuwazuia watu kuhama vyama, ningependa watu wawe na uhuru wa kuhama vyama.Ningependa kuona vyama vyenyewe kwa utashi wavyo tu vinaamua kuwachuja hawa watu wanaohama vyama.

Tukifuata utaratibu huu, sio tu tutaimarisha demokrasia, bali pia tutakomaza vyama viimarike zaidi kwa kufuata Darwinian evolution.

Na tutaweza kujua kirahisi chama kipi ni imara na kinaweza kutoa viongozi miongoni mwa wanachama wake wa siku nyingi, na kipi ni chama bomu kisicho na viongozi kinachosubiri makapi ya CCM.

Kama kungekuwa na sheria hiyo unayoipendekeza inawezekana tusingejua udhaifu wa CHADEMA leo.
 
Nilisema hapa CHADEMA wasichukue makapi ya CCM, yatawatokea puani. Watu wakasema ooooh, aaaah.

Sasa mnayaona. Na bora hata huyu karudi CCM kabla ya uchaguzi, kuna wengine watabaki upinzani na kuuhujumu upinzani huu huu bungeni.
you can say that again... its not over yet!!! watu walimshukia rev. lakini relevance iko palepale
 
Steve-Dii

hivi vyama vya upinzani vilitakiwa vizingatie suala hilo mapema sana. Vili gamble na imeanza kula kwao.

tunaambiwa kuwa zitto kabwe yeye binafsi alienda kuwaomba hao 'walio onewa' kwenye ccm, kujiunga na chadema na baadae kuwapa nafasi ya kugombea majimbo.

Hii mimi inanionyesha dhahiri kuwa hao wahamiaji kwenye vyama vya upinzani hawajahamia kwa kupenda sera au muongozo wa upinzani bali kama njia ya kuikomoa ccm.
Wakipewa pesa ndio haooo wanaondoka bila ya kutizama nyuma kwa kuwa mapenzi tokea hapo mwanzo hayapo.

Gaijin,

Hicho ndicho ninachotaka kukisema mimi, kuhama kuhama chama kimoja hadi kingine isiwe hoja kubwa saaana, maana watu hubadilisha misimamo juu ya vyama vyao. Namna hilo linavyofanyika ndilo la kuangalia na kuwekewa umakini. Watu wenye pesa leo wakiwa CCM, haizuii watu wengine kuwa na pesa za kuhonga wagombea kwenye vyama vya upinzani. Kwa mfano huu uliopo, na kama jambo hili limetokea kweli; hatuchelewi kusikia hili jambo linakuwa common practice kwenye chaguzi mbeleni, si kwa chama tawala pekee bali hata kwa upinzani. Maana ku-hog position ya mgombea wa chama ni jambo linalowezekana kotekote.

Kwamfano, kwa hela hizo hizo ni kwamba mtu wa Chadema anatayarishwa tu mapema kama valid candidate wa CUF au CCM au TLP, kisha kura za maoni zinafatia, jamaa anashinda kura za maoni za CUF, CCM au TLP. Baada ya kipindi cha kura za maoni kuchagua wawakilishi wa jimbo kwa vyama husika kupita, jamaa anatangaza kuhamia Chadema. Hivyo chama alichokuwa amepatia uwakilishi kinaachwa na nafasi tupu. Hili ndilo ninaloliongelea mimi na kuhimiza liangaliwe ili kuweza kuleta demokrasia ya kweli kwa kuzuia movement kiholela.
 
Hili ni jambo ambalo lazima litokee, hata chadema ikifanya vetting ya aina gani.
Bado watu wengi wanaamini bila ccm haiwezekani.
Ni afadhali huyu jamaa ameonyesha rangi yake mapema
chadema ni chama huru na akiwezi kuwazui watu wanaoonyesha moyo wa dhati kutaka kupigania nchi hii, tatizo siyo kila anayeonyesha moyo wa dhati ana moyo wa dhati.

Kwa hali ilivyo tz wanachama wengi wa vyama vya upinzani walishawahi kuwa wanachama wa ccm katika maisha yao. Hata waasisi wa chadema walishawahi kuwa wanachama wa ccm. Kizazi kipya ndio kina watu ambao hawajawahi kuwa wanachama wa ccm.

Kupata watu kugombea upinzani ni shida sana sio sawasawa na ccm. Wengi mnalalmika chadema wasichukuwe watu wa ccm lakini kujitokeza kwenda kugombea chadema hamtaki
 
Kabonde
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
  • email.png
    Send Email
user-offline.png
JF Senior Expert Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

Join DateTue Aug 2008Posts270Thanks : 162
Thanked 76 Times in 42 Posts
Rep Power23
 
Good riddance, maana asingewafaa wananchi wa Singida huyu! Sasa CCM si lazima washitakiwe kwa kutoa rushwa na huyu naye, au Takukuru watasubiri Mtikila ashitaki! Maskini hivi Mtikila yuko Huru au anakula dona jela!
 
CCM imejaa waroho wa madaraka ambao wakikosa huko wanakimbilia upinzani kutumia link hiyo kuyatwaa hayo madaraka.
Dawa ni kujenga chama kuanzia chini no matter what.
Kama CHADEMA wakinihitaji niwape ushauri am available.
 
Wanasheria Mnashauri nini kuhusus utapeli huu na nini kifanyike kuhakikisha kwamba sheria inachukua mkondo wake na tabia kama hizi zinakomeshwa?
 
Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, kwa tiketi ya Chadema Elisha Nkhambaku amerudi tena CCM baada ya kufatwa na uongozi wa juu wa CCM ukimsihi arudi CCM ambako alijiengua baada ya kushinda kwenye kura za maoni na NEC kumuengua kwenye kinyanganyiro hicho.Elisha ambaye alikuwa amejiunga na Chadema ili kugombea kwenye Jimbo hilo la Singida Magharibi amejitoa Chadema baada ya kupewa million 60 na kuahidiwa u-DC kwenye jimbo jipya...

Source: Zimetoka kwa mtu wakaribu sana ambaye alikuwa ni mmoja ya watu waliomfuata Elisha.

inasikitisha inaniuma sana inaniambia je watu wote ambao walihama ccm wanatafuta ubunge kama siasa ya kujinufaisha wao na siyo kwenda kutetea wananchi kwa kuwa je ndiyo mfumo wetu kwa kuwa kama huyo mmoja yupo hivi je ni kweli hao wengine watakuwa vipi jamani tuwe macho watu kama hawa na wezi wale wa kuchomwa moto hawana tofauti huyu katumia wizi wa busara na yule wa nguvu wote ni wezi takukuru inakamata wale walio na mwelekeo tofatuti na cCM na siyo wenye kuelekea kule kule kwa jana na juzi hizi siasa za ccm za juzi jana na leo kwenye waliopo sidhani kama zinaweza kutufikisha mbali tuwe macho ndugu zangu
 
Hii kali kweli... ukisikia chama tawala ndio hicho bana, kwao gharama si kitu ... kununua magazeti ya kumchafua mtu hata kwa milions, kumpa mtu milions ati aseme ungo kwa kumponda mpinzani, kuwafunga midogo wenye haki zao ili wasifike kwenye vyombo vya sheria... duh.... utawala bana, ni silaha nzuri sana... ila huu ni mwanzo, hata ROMA haikujengwa kwa siku 2... ipo siku chumvi itayeyuka tu kwenye maji hakuna msalie mtume.
 
Back
Top Bottom