Elections 2010 Mgombea wa Chadema ahongwa milioni 60

Namfahamu sana Elisha, atakuwa amejimaliza kwa kufanya hivyo. Alikuwa na mtaji mzuri wa kushinda baada ya NGO yake kufanya vizuri katika masuala ya maendeleo jimboni humo. Kukosa msimamo ni hatari.

mimi naona hajakosa msimamo karudi chama chake cha zamani. Eti alipotoka CCM kwenda chadema hakununuliwa lakini alipoamua kurudi kwenye chama chake cha Zamani CCM amenunuliwa. acha longo longo hapa
 
Nilisema hapa CHADEMA wasichukue makapi ya CCM, yatawatokea puani. Watu wakasema ooooh, aaaah.

Sasa mnayaona. Na bora hata huyu karudi CCM kabla ya uchaguzi, kuna wengine watabaki upinzani na kuuhujumu upinzani huu huu bungeni.
.

Na wengine watarudi CCM baada ya uchaguzi mkuu hasa watapokuwa wameshindwa kwenye nafasi za ubunge na udiwani. Hawa wanaohamahama kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wamefuata madaraka Chadema watakapokosa tu ni wa CCM baada ya uchaguzi.
 
Kapata alichokuwa anatafuta,hapa TZ wanaogombea ubunge wanatafuta ngawira na sio kwa ajili ya kuwatumikia wananchi,ndio maana kwa sisi wengine siasa ni "taaluma ya kihuni''abadani siwezi nikawa mwanasiasa hasa wa pande hii ya TZ

Ni kweli mkuu. Kwa walio wengi mbio za kuelekea kule mjengoni ni kutafuta maisha ya nyumbani kwao na si kwa maendeleo ya taifa.
 
Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, kwa tiketi ya Chadema Elisha Nkhambaku amerudi tena CCM baada ya kufatwa na uongozi wa juu wa CCM ukimsihi arudi CCM ambako alijiengua baada ya kushinda kwenye kura za maoni na NEC kumuengua kwenye kinyanganyiro hicho.Elisha ambaye alikuwa amejiunga na Chadema ili kugombea kwenye Jimbo hilo la Singida Magharibi amejitoa Chadema baada ya kupewa million 60 na kuahidiwa u-DC kwenye jimbo jipya...

Source: Zimetoka kwa mtu wakaribu sana ambaye alikuwa ni mmoja ya watu waliomfuata Elisha.

Hiyo kwenye nyekundu ngoja niiweke kwenye "reminder" ya simu yangu kujua kitakachojiri hapo baadae
 
Huyo hajaona mbali kabisa. Kachukua mil. 60 wakati angekaa bungeni angelamba zaidi ya hizo. Sio lengo kupata hela lakini huyo ni mwananjaa tu
 
Yawezekana huu ni mchezo uliokuwa umepangwa tangu mwanzo. Jamaa alitumiwa tu na alikuwa anajua atakachofanya baadae. Dirty politics, thats it.
 
Huyu ndugu Elisha ana record chafu sana na ni mtu hasiye na msimamo kabisa, anasumbuliwa na tamaa.Mwaka 2005 alitaka kugombea ubunge kwa kwa tiketi ya CCM na kwenye kura za maoni alikuwa apambanishwa na Muhamed Missanga ambaye sasa ni katibu wa miundombinu wa Bunge, Ambaye mwaka 2005 alimpatia bwana Elisha Tsh millioni tano akimtaka amuhashie hiyo nafasi ya ubunge akimuahidi kuwa mwaka 2010 hatogombea hivyo atamuashia hiyo nafasi. kinyume chake ndio haya ya yalio tokea sasa hivi. Mpaka hapo unaweza kupata picha Elisha ni mtu wa aina gani. http://www.facebook.com/ajax/intl/l...acebook.com/?compose&id=660477358&sk=messages
 
Hiyo kwenye nyekundu ngoja niiweke kwenye "reminder" ya simu yangu kujua kitakachojiri hapo baadae
We subiria utakuja kuniambia....Japo kuwa wanaweza kufanya kinyume chake, Kama alivyo fanyiwa na Muhamed Missanga.
 
Nchi ikienda kwa misingi ya namna hii kweli tutafika?............laana hii nyie akina elisha.....unajua kabisa njia ya kweli lakini unaikataa......nyie ccm mtanunua watu mpaka lini........??????
 
chadema poleni, na kama kuna mtu mwenye akili zake na kuamua kuandama na chadema pia anasthili kupewa pole tena ile ya samaki poole wanavyomfanya.


nani asiejua kuwa chadema haina dhamira ya dhat i ya kuwatumikia watanzania.

ukirudia waraka wa chacha wangwe utawajua ni nani akina chadema?

Zitto anajikaza tu yakimshinda atakuja kutueleza kuna nn huko ndani, yeye yaliomkuta alipotaka kugombea uwenyikiti anayajua hao ndio chadema.


na safari hii ndio komesha maana wananchi watafanya kufuru na kuwahakikishia chadema kuwa watanzania wanalaani kiudhati, ukabila, udini, umajimbo na majisifu yasio na faida?


hivi waulizane chadema msimamo wao au wanafata siasa za mlengo gani ndio utachoka, hawajulikani kama ni maliberali, demokrati, au masoshalisti, au maccomunist/


hawa popo tu, kila kwenye maslahi wanapafata wameishiwa
 
source wako ni mtu aliyefuata Elisha na kumpa kiasi hicho cha fedha kisha akatoa siri kwako..... imekaa kama propaganda ya kisiasa vile
Mkuu, Hizo unazo sema wewe ndizo propaganda zenyewe. Unijui sikujui hivyo usidhani unavyo fikiri wewe na wezako ni hivyo hivyo... Swala la mimi kupata hizi habari lisikupe taabu kabisa. hii ni post yangu ya kwanza hapa JF inayohusu maswala ya siasa,

Kama umesoma maelezo yangu ya Page ya tatu nafanya utaratibu wa kuwasiliana na Melo kama unauwezekano wakuweka clip kaadha za ili sakata.
 
Back
Top Bottom