Mgombea ubunge wa UPDP Igunga

Mgombea ubunge wa UPDP Igunga

Nimemuona, jamaa amelewa chakali...duu! Bongo nomaaaaaaa

Pamoja na kucheka, nimesikitika sana kuona TV ya Taifa inatoa muda wote huo kwa huyu jamaa ambaye anafanya mzaha, na kushindwa kutoa walau muda kigogo tu kutujuza kuhusu maendeleo ya kampeni za vyama vingine! Aibu.
 
Pamoja na kucheka, nimesikitika sana kuona TV ya Taifa inatoa muda wote huo kwa huyu jamaa ambaye anafanya mzaha, na kushindwa kutoa walau muda kigogo tu kutujuza kuhusu maendeleo ya kampeni za vyama vingine! Aibu.

Anafanya mzaha wapi mkuu. Hiyo ndiyo picha ya na hali halisi ya avarage cizten wa wilayani na vijijini. We kama uko mjini na hujai kuspend some time wilayani na vijijini utashangaa. Huyo jamaa hajui tu kufanya maigizo yaani kawa himself na sincere . Kwa kuwa watu wamezoea siasa wanataka wadanganywe wanataka watu wa maigizo.

Huyu anaweza kuwa bora kuliko hata kuchagua wa CCM. Huyu ni aina ya mtu ambaye hata akiwa mbunge bado anaweza kutumia siku hata zaidi 150 kati ya 365 kwa mwaka kukaa jimboni kwake igunga.

Huyu ni aina ya wabunge anaweza asiwe na la kuongea kuhusu Afrika mashariki au kuhusu Mambo ya Nje au kuhusu internet au Viwanda lakini ni mtu ambaye anajua hasa wanaigunga wanataka nini. Sio wanasiasa wa mjini mara nyingi tunafundisha wapiga kura nini wanataka.....
 
Jamaa ni mkali,yaani Kama ni kuchekesha anaongoza teh teh bongo bwana!!!!
 
Hebu tuambizane ukweli,nani Kalewa sasa TBC-1 au Huyu jamaa?Maana anaonekana kabisa Katumwa na Magamba na TBC wakaamuliwa lazima warushe!!Na hata yule mtangazaji kumfananisha na Zecomedy nafikiri anataka kumfuata Tido yule,ile ni mission planned and accomplished!!Ile maana yake hata Dr.Kafumu gambaz hana sera kiasi kwamba kilichobaki sasa ni kuwapoteza wananchi.Taarifa ya habari ya TBC- imekuwa Vituko show zaidi ya Chanel-10!!!Aibu yao wenyewewalioonyesha uchafu ule.Na kesho nadai chenji ya kodi yangu iliyokwenda TBC kurusha vipindi leo kudadeki!!
 
Yaani ilikuwa full comedy kuliko hata akina masanja,kwa TBC zile ndio sera na aina za viongozi wanaotaka wananchi wawasikilize ,sio akina Tendwa mara alivyosema angekuwa na mamlaka angeufuta uchaguzi wakamkatiza kwani alikuwa anaingilia maslahi ya TBC na Wanaowatumikia,
 
hapo kwa solar panel ndo kumenivunja mbavu..
 
Kuna umuhimu wa kuwa serious na katika mambo ya msingi kama hili la uchaguzi, UPDP wanaanza kampeni kwa kutangaza biashara ya pombe na chipsi ambayo inaendeshwa na viongozi wao, viongozi wanacheza bolingo wakiwa wamelewa chakari lakini bado TBC wanatoa coverage kubwa kwa watu kama hawa hivi wanalenga kuelimisha au kuchekesha au ndio demokrasia yenyewe?
 
duh....mimi nilimuona nikashindwa kujua lengo lake hasa ni nini....tena mimi nilibahatika kumuona akicheza ndombolo huku yupo chicha.......tutaona mengi jamani....khaa

Khaaaaa!! Hivi huyo msajili huwa anawakagua wagombea kabla ya kuwapitisha?? Vyama vingine kweli KITUKO.....
 
Afadhari jamaa aliyeamua kutufurahisha hapa "kisiwa cha amani" kuliko yule "mwehu" aliyataka kututisha na kigobole chake.
 
Hii thread haina mvuto wala mashiko lakini nashangaa imeruhusiwa kuingia hapa wakati thread yangu iliyobeba ujumbe mzito ya ''TANZANIA INASHIKA KASI'' eti imepotezewa.
 
Jamaa ameamua kutumia haki yake ya msingi ya kikatiba ya kugombea kama raia,,hata hivyo uungwaji mkono ulikuwa si haba pia alipata watu kadhaa
 
Mi kanifurahisha alipowaambia vijana atawapa ajira na atawalipa kwa dola na pound, ajira ni ip ss? Huyu km magamba teh! Teh teh teh
 
Back
Top Bottom