Elections 2010 Mgombea CHADEMA Nkenge ajiondoa kugombea Ubunge

sababu kubwa ya kujitoa ni kuwa chama makao makuu kimeshindwa kutoa fungu la kumwezesha kufanya kampeini badala yake amekuwa akitumia fedha zake

baada ya kupata habari kuwa undp itatoa fedha za kwa ajili ya gharama mbali mbali za vyama kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ndipo baaadhi ya vyama vikajitutumua kusimamisha wagombea katika nafasi mbali mbali; na baadhi ya wagombe nao wakajitokeza kugombea kupitia vyama mbali mbali. Lengo ikiwa ni kupata fedha zitakazotolewa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2010. Ndio maana mwaka huu kama vile kuna utitiri wa wagombea.

Kutokana na malalamiko makubwa kutoka kwa mawakalawa vyama mbali mbali katika chaguzi zilizopita ya kutolipwa baada ya matokeo kutangazwa, tume ya uchaguzi imeamua kuwa itawalipa mawakala yenyewe kwa kutumia fedha zitakazotolewa.

Hivyo vyama vilivyofuata fedha na wagombea waliofuata fedha baada ya kusikia hivyo wameishia nguvu na kukata tamaa. Baadhi ya vyama tayari vimeanza kupigia debe vyama vingine, wagombea kujitoa n.k.

Mapambanouya ukombozi hayataki watu wenye chembe chembe za ufisadi mioyoni mwao.

Tukaze buti wachache watakaobakia!!!!! Mabadiliko yoyote hufanikishwa na wachache kwa maslahi ya wengi
.
 
Nipo kwenye hiyo press cof,ingawa imekwishasoma magazeti ya kesho,hasa gazeti la Uhuru kwani naomba mwandishi wao kama vile anaripoti live,kwani kila wakati anapiga simukazi kweli kweli mwaka huu
Naanza kuwa na wasiwasi na habari yenyewe kama bado mwandishi tena wa Uhuru ana negotiate seem like a fishy to me, but lets wait.
 
Hivi huyu kanunuliwa kwa bei gani? Maana kila mtu ana bei yake, hata JK alikuwa na bei yake pale aliponunuliwa na akina Rostam.
 
Nkenge iko mkoa gani?

Mkoa KageraAwali jimbo hilo lilikuwa likiwakilishwa na Dk Diodorus Kamala ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,alishindwa katika kura za maoni na Bi Asumpta Mshama
 
Taarifa za sasa hivi ni kuwa mgombea ubunge kupitia CHADEMA Bw Focas amejiondoa katika kinyanganyiro hicho hivyo kuwacha wagombea wa CCM na CUFAwali ilidaiwa kuwa focas ambaye anamiliki vifaa vya mziki alidaiwa kupandikizwa na Dk Kamala aliyebwaga na Asumpta mshama katika kura za maoni.sababu za kujiondoa nitaweka hapa muda mfupi ngoja amalize kulonga na medianatumia simu

Kama kuna ukweli basi Kamala amefanya kazi yake na tegemea kulipwa fadhila kwa ubunge wa viti maalumu, sorry ubunge wa kuteuliwa!
 
Sababu kubwa ya kujitoa ni kuwa Chama makao makuu kimeshindwa kutoa fungu la kumwezesha kufanya kampeini badala yake amekuwa akitumia fedha zake

Kwa wagombea ubunge anayepeleka taarifa ya gharama za uchaguzi ni chama au mgombea? Imeandikiwa ukitaka kujenga ghorofa lazima ufanye tathmini ya gharama usije ukaishia kwenye msingi
 
poa tu wacha aende, hakua na dalili ya kushinda... nashauri hata wale wa ccm wenye hali mbaya wajitoe... bora lawama kuliko fedheha
 
Ameshakula vya watu na sasa amekubali na yeye aliwe kidogo.

Maadamu mwaka huu Dr. Slaa anashinda, jamaa ndiyo wiiiii (ile ya JKT).



Kama kuna ukweli basi Kamala amefanya kazi yake na tegemea kulipwa fadhila kwa ubunge wa viti maalumu, sorry ubunge wa kuteuliwa!
 
Last edited by a moderator:
Nipo kwenye hiyo press cof,ingawa imekwishasoma magazeti ya kesho,hasa gazeti la Uhuru kwani naomba mwandishi wao kama vile anaripoti live,kwani kila wakati anapiga simukazi kweli kweli mwaka huu

NIna wasi wasi na wewe RM; umekaa kama kikazi zaidi!!!
 
Hivi huyu kanunuliwa kwa bei gani? Maana kila mtu ana bei yake, hata JK alikuwa na bei yake pale aliponunuliwa na akina Rostam.

Bei ya JK ilikuwa Sh 40 bilioni za kagoda! hapo mdosi haguswi na JK ataenda kule Igunga kumwagia sifa kemkem. This is a bloody f****** phase of CCM administration!!!!
 


Mgombea ubunge wa jimbo la Nkenge kwa tiketi ya CHADEMA,Focus Rwegasira ambaye ni mpiga Disco maarufu mkoani Kagera, akijinadi wakati wa uzinduzi rasmi wa mikutano ya Kampeni ya chama hicho uliofanyika maeneo ya mafumbo ndani ya manispaa ya Bukoba.






umati mkubwa ukimsikiliza mgombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo la Bukoba mjini kupitia tiketi ya CHADEMA,Wilfred Lwakatare alipokuwa akiongea na wananchi kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho.
 
Hivi jamani mgombea wa Nkenge kupitia CHADEMA Bw. Focus au ni Walter Nyahoza nijuzeni.
 
Yale yale ya Nakaaya Sumari............hayo ni mavuvuzela tu ila mwaka huu lazima CHADEMA wawatoe kamasi CCM.
 
Kwani kuna shida gani? Kama huyu wa chadema kajitoa sababu anazijuwa yeye! Bado yuko wa cuf huyu kama wapinzani wanataka mabadiliko basi wampe huyu na kama wafuasi wa chadema hawataki upinzani ushinde sababu ya ubinafsi wao basi nawashauri wapige kura za maruhani kama walivyopiga wana cuf wa pemba! Vinginevyo wampe kura zao mgombea wa cuf kwani huyu anaonekana amekataa kurubuniwa!

Chadema munataka kupewa ridhaa ya kuongoza nchi wakati viongozi wenu ndio kama hao ambao wanijitoa mmoja mmoja hata uchaguzi haujafanyika? Labda mujitayarishe tena kwa uchaguzi wa 2015!
 
Back
Top Bottom