Mgogoro wa Wabunge 19 wa CHADEMA ni wa kimaslahi zaidi kuliko Kisiasa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,310
12,607
Tangu chaguzi za vyama vingi zianze mwaka 1995 vyama vya upinzani vimekuwa na malalamiko na madai hayohayo ya kuibiwa kura na tume isiyokuwa huru, lakini vyama vya upinzani havijaacha kuhudhuria vikao vya bunge wala kuteua Wabunge wa viti maalamu kwenda kuapa na kuhudhuria vikao vya Bunge.

Mara hii kulikoni? Uchaguzi wa safari hii umetoa matokeo tofauti kabisa tofauti na chaguzi nyingine za vyama vingi zilizopita. tofauti hizo ni pamoja na:

1. Hakuna hata Mwanaume mmoja wa CHADEMA aliyeshinda kiti cha ubunge
2. Hakuna kiongozi mkuu wa chama aliyeshinda Ubunge
3. Viongozi wa chama wanadai hawakuhusika na uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum.

Kwahiyo, kwa hali hii inawezekana kinachotokea kwa Wabunge hawa 19 wa Viti Maalum ni matokeo ya matokeo haya tofauti ya uchaguzi wa mwaka huu.

Hivyo, inawezekana yafuatayo yanasababisha haya tunayoyaona sasa.

1. Wanaume tumekosa basi tukose wote
2. Viongozi wakuu tumekosa basi kwa hasira tukose wote kama shinikizo
3. Walioteuliwa viti maalum walioapa safari hii kuna ambao walioachwa nje.
4. Walioteuliwa sio chaguo la viongozi wa chama.
5. Wanawake ambao hawakuchaguliwa ndio chanzo cha tatizo, wivu
6. CHADEMA kushiriki bungeni kunavuruga juhudi za kuibana serikali kupitia wahisani
7. Kushiriki Bunge kunaleta dhana kuwa hawajali kilio cha Lissu
8. Wabunge walioteuliwa wamehongwa kwenda kuunga juhudi
 
Back
Top Bottom