Mgogoro mkubwa Arusha Chadema waendelea kufukuzana

Naona tofauti ya CDM na CCM kwenye kuwashughulikia wasaliti, CDM inawaachia uhai wao na kuwaambia enendeni kwa amani ila CCM wanalia na uhai wako mifano mizuri ni kina Kolimba (RIP), Mwakyembe,Mwandosya nk. Iliyobaki tujadili njia ipi ni bora ambayo vyama vidogo kama CCK vinaweza vikaiga na watanzania tukaridhika na maamuzi?????
 
Mkuu Nanyaro mleta hoja katoa maelezo yanayojitosheleza kata majina na nyazifa wanazoshikilia,eneo na nk wewe unakanusha bila kutoa maelezo ya kina yatakayojitosheleza.Kwahiyo unataka kutuambia Dominick Mboya bado ni mweyekiti wa Elerai na Joseph Warioba I hope si waziri mkuu mstaafu bado ni Katibu ?.
Kasha jibu hilo soma mabandiko yake...
 
Nimejibu kwa kirefu,kwanza CHADEMA hakuna mgogoro,kwa kuwa huyo anayetajwa kuwa mwenyekiti si mwanachama wa CHADEMA,Dominik Mboya si mwanachama,Joseph Warioba ni mwanachama ila hana cheo/nafasi yoyote kwenye chama.
Mboya alifutwa uanachama kutokana na kukiuka maadili ya chama,ikiwa ni pamoja na kukataa maagizo mbalimbali ya viongozi,kufanya vitendo vya kugawa chama,pamoja na jaribio la kutaka kufunga ofisi ya chama.
Nimeongea na wanachama wote walioandikwa kwenye gazeti la Mwananchi(Si Dominik Mboya) wamekana kuzungumza na gazeti
 
Huwezi kukubali wakati wewe ndio ulikuwa Mwenyekiti kwenye kikao cha kuwafukuza wenzako!

Yaelekea umelipwa na mafisadi cash nzuri sana kuangusha mataputapu ya hapa jamvini!

Kawaambie CDM iko imara tofauti na watakavyo hao wachumia matumbo yao!

tuna hasara sana na chichiem!
 
hata mimi nipo Arusha sijaona mgogoro wowote, labda mwandishi ana undugu na wale madiwani waliofukuzwa, ni kweli ndugu yako akifukuzwa inatia uchungu lakini naamini ulafi wao umewaponza. Pooleni
 
kwa hadhi yako hayo hayo ni majibu ya kihuni.toa ufafanuzi wa kilichotokea ili jamii iseme.wewe unaanza kujitetea.

Mkuu ana HADHI ipi??? Mi nafkiri ungetumia neno "nafasi uliyonayo" manake hilo neno hadhi kwanza kwa majibu yake hata kutumia hilo neno bado ni kumpa nafasi kubwa! In short Elerai mgogoro upo na jinsi ya kukanusha si kukataa bali kutolea jambo hilo maelezo ya kutosha na hili vile vile lifanyike kwa umakini kwa kuwa kuna uwezekano wa kutoweza kupata maelezo ya upande wa pili. Muhusika aache kutoa majibu ya jazba na kutuhumu watu eti wametumwa kukichafua chama.
 
mgogoro wa CHADEMA na mgogoro wa serikali upi wenye madhara hapa tujadili mambo ya kitaifa usilete ukada hapa ongelea mgogoro wa madaktari tukuelewe
 
Yaelekea umelipwa na mafisadi cash nzuri sana kuangusha mataputapu ya hapa jamvini!

Kawaambie CDM iko imara tofauti na watakavyo hao wachumia matumbo yao!

tuna hasara sana na chichiem!
tatizo la hawa vigamba wadogo wakilipwa wako tayari kuuza hata familia arusha kuna mgogoro ok itisheni uchaguzi na policcm wawepo wa kutosha muone atayeshinda
 
Wanabodi.
Baadhi ya viongozi wa Chadema kata ya Elereai, wamepinga kufukuzwa kwao madarakani na kuhishutumu kamati ya utendaji ya wilaya chini ya Mwenyekiti wake, Efatha Nanyaro.

Viongozi wanaopinga kufukuzwa madarakani ndani ya kata hiyo ni pamoja na Mwenyeketi wa Kata ya Elerai, Dominick Mboya na Katibu wake Joseph Warioba.

Wengine Mwenyekiti wa Wazee, Bakari Kasembe, Mwenyekiti wa Vijana, Paul Maganga, na Katibu wake, Sia Temu, Mwenyekiti wa Wanawake, Mariam Suleman pamoja na mweka hazina. Baraka.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa viongozi hao, Dominick Mboya alisema kwa mujibu wa katiba ya Chadema kamati tendaji ya wilaya haina mamlaka ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi uliowaingiza madarakani, kilichofanyika ni uhuni na ubabe tu.

Hizo ndio siasa za Chadema Arusha.

Hivi lini umewahi kuandika positive impact kwa CDM? Kwa taarifa yako CDM Arusha hakuna mgogoro, na likitokea kundi au magugu ndani ya chama yanang'olewa haraka sana. CDM wapo makini kupita maelezo!
 
Wanabodi.
Baadhi ya viongozi wa Chadema kata ya Elereai, wamepinga kufukuzwa kwao madarakani na kuhishutumu kamati ya utendaji ya wilaya chini ya Mwenyekiti wake, Efatha Nanyaro.

Viongozi wanaopinga kufukuzwa madarakani ndani ya kata hiyo ni pamoja na Mwenyeketi wa Kata ya Elerai, Dominick Mboya na Katibu wake Joseph Warioba.

Wengine Mwenyekiti wa Wazee, Bakari Kasembe, Mwenyekiti wa Vijana, Paul Maganga, na Katibu wake, Sia Temu, Mwenyekiti wa Wanawake, Mariam Suleman pamoja na mweka hazina. Baraka.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa viongozi hao, Dominick Mboya alisema kwa mujibu wa katiba ya Chadema kamati tendaji ya wilaya haina mamlaka ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi uliowaingiza madarakani, kilichofanyika ni uhuni na ubabe tu.

Hizo ndio siasa za Chadema Arusha.

Nipongeze hatua zilizochukuliwa zilikuwa za msingi sana..... kama kunakiongozi ambaye haendani na speed ya chama ni bora aondolewe ilikupisha wenye kasi na chama washike ngazi, ilikuharakisha maendeleo kwa wananchi, unayedai kuwa katiba ya chama haikufuatwa huijui katiba ya chadema( Ngazi ya juu itakuwa na mamlaka ya kuwajibisha ngazi ya chini yake kupitia vikao halali) hapo inatosha.*
 
ni heri wanaofukuzana kuliko wanaouana; Sokoine, Kolimba, Kombe, Kigoma Malima na mnusurika Mwakyembe:
uzandiki mzigo jamani!
 
Jamii ielewe kuwa CHADEMA haina mgogoro,unataka jibu gani zaidi ya hilo?sijibu unavyotaka wewe najibu ukweli,na ukweli ni kuwa hakuna mgogoro.
mkuu,tunaomba utujuze kuhusu hao wanachama na viongozi uliowafukuza.nini hasa kilitokea.wewe ni kiongozi tunategemea uwe ndio dira na utoe taarifa muhimu zinazokihusu chama.
 
kwa nini cdm inataka kujiimarisha katika fukuza fukuza ya wanachama na viongozi wake?????????????
chama kinajengwa kwa kuvumiliana ankukosoana sasa huu umwamba unatoka wapi??????????????

Mkuu we umeona wapi Magugu yanapaliliwa? Akina Mboya ni Magugu mbaya katikati ya Ngano safi. Lazima wang'olewe kabla hawajaleta madhara. Isitoshe CDM Arusha tuna evidence kuwa Mboya alikuwa financed na magamba kuigawa chadema. Mbinu yao imeyeyuka, CDM wapo makini, na zoezi hili haliishii kwa akina Mboya, itaendelea kuwakumba wale wote wenye nia mbaya na chama. Nitashangaa kama mtu mzima tena msomi anashauri eti siasa ni kuvumiliana. Ndiyo, siasa nikuvumiliana lakini siyo kwa watu wanaokisaliti chama.
 
Nimejibu kwa kirefu,kwanza CHADEMA hakuna mgogoro,kwa kuwa huyo anayetajwa kuwa mwenyekiti si mwanachama wa CHADEMA,Dominik Mboya si mwanachama,Joseph Warioba ni mwanachama ila hana cheo/nafasi yoyote kwenye chama.
Mboya alifutwa uanachama kutokana na kukiuka maadili ya chama,ikiwa ni pamoja na kukataa maagizo mbalimbali ya viongozi,kufanya vitendo vya kugawa chama,pamoja na jaribio la kutaka kufunga ofisi ya chama.
Nimeongea na wanachama wote walioandikwa kwenye gazeti la Mwananchi(Si Dominik Mboya) wamekana kuzungumza na gazeti

Mkuu naona unakubali taratibu kama kuna mgogoro! Unaweza kutuambia kwa nini mmewafukuza chama baadhi ya wanachama wenu? Na zile barua ulizowapa zilikuwa ni za nini?
 
Yaelekea umelipwa na mafisadi cash nzuri sana kuangusha mataputapu ya hapa jamvini!

Kawaambie CDM iko imara tofauti na watakavyo hao wachumia matumbo yao!

tuna hasara sana na chichiem!

Wewe unalipwa na Mbowe kiasi gani?
 
hata mimi nipo Arusha sijaona mgogoro wowote, labda mwandishi ana undugu na wale madiwani waliofukuzwa, ni kweli ndugu yako akifukuzwa inatia uchungu lakini naamini ulafi wao umewaponza. Pooleni

Wewe ni Chadema-Kata huwezi kujua kinachoendelea wewe subiri maandamano!
 
Mkuu Nanyaro mleta hoja katoa maelezo yanayojitosheleza kata majina na nyazifa wanazoshikilia,eneo na nk wewe unakanusha bila kutoa maelezo ya kina yatakayojitosheleza.Kwahiyo unataka kutuambia Dominick Mboya bado ni mweyekiti wa Elerai na Joseph Warioba I hope si waziri mkuu mstaafu bado ni Katibu ?.

Mkuu Ngogo,
Nimejaribu kuwawekea orodha ya viongozi wao waliofukuzwa lakini Chadema-kata bado wanabisha tu.
 
Nipongeze hatua zilizochukuliwa zilikuwa za msingi sana..... kama kunakiongozi ambaye haendani na speed ya chama ni bora aondolewe ilikupisha wenye kasi na chama washike ngazi, ilikuharakisha maendeleo kwa wananchi, unayedai kuwa katiba ya chama haikufuatwa huijui katiba ya chadema( Ngazi ya juu itakuwa na mamlaka ya kuwajibisha ngazi ya chini yake kupitia vikao halali) hapo inatosha.*

Kwa hiyo unakubali kuna mgogoro na wanachama wengine mmewafukuza?
 
Back
Top Bottom