Mgogoro mkubwa Arusha Chadema waendelea kufukuzana

Mgogoro mkubwa Arusha Chadema waendelea kufukuzana

CHADEMA Arusha,hakuna mgogoro,chama kipo IMARA,kuliko kipindi kingine chochote,
ndg yangu nanyora natambua uwajibikaji wako ktk kuimarisha chama chetu. Nimeshashauri na sasa nashaur tena eneo lamorombo msiliache bila kufungua matawi nieneo muhmu sana kwan ongezeko la watu nikubwa sana karibu morombo tukijenge chama Kazinjema nsuri!
 
Wanabodi.
Baadhi ya viongozi wa Chadema kata ya Elereai, wamepinga kufukuzwa kwao madarakani na kuhishutumu kamati ya utendaji ya wilaya chini ya Mwenyekiti wake, Efatha Nanyaro.

Viongozi wanaopinga kufukuzwa madarakani ndani ya kata hiyo ni pamoja na Mwenyeketi wa Kata ya Elerai, Dominick Mboya na Katibu wake Joseph Warioba.

Wengine Mwenyekiti wa Wazee, Bakari Kasembe, Mwenyekiti wa Vijana, Paul Maganga, na Katibu wake, Sia Temu, Mwenyekiti wa Wanawake, Mariam Suleman pamoja na mweka hazina. Baraka.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa viongozi hao, Dominick Mboya alisema kwa mujibu wa katiba ya Chadema kamati tendaji ya wilaya haina mamlaka ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi uliowaingiza madarakani, kilichofanyika ni uhuni na ubabe tu.

Hizo ndio siasa za Chadema Arusha.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...vijijini-kuwaleta-kwenye-maadhimisho-yao.html
 
Ni kweli MJINGA inatakiwa uheshimiwe ili watu waepukane na balaa!

Sasa nyie Chadema-Kata mnapinga hakuna mgogoro Arusha, wakati wenye chama kina Slaa, wanautambua huu mgororo ingekuwa uzushi hii thread wangeifuta.
 
Ndio Mkuu maake majuzi nilionana na Lema pale SELENA HOTEL jamaa hakuwa na nyuso ya amani. Maake aliandamana na jamaa wawili ambo nilihisi ni ndugu zake kwani walikuwa wakifanana.

Du hii itakuwa vita mbaya.

Itakuwa alikuwa na mjomba {Mboya} naye kesha zoezwa kukutana nakuzungumzia bar,Mh.Lema keshaona kinachotaka kutokea kwahiyo anajaribu kupanga safu ya watu wake kwa lazima,siri tunazijua,na anachokikosea ni kumpanga kama huyu muuza ndizi na chips mayai,asiye jua siasa ni nini,hajawahi hata kuwa balozi,au hata kiongozi wa kikoba.kinachonishangaza pia anajiita mwekiti,wakati mwenyekiti yupo,haya anajiita na kujitapa ye diwani kachaguliwa na nani japo mpaka sasa hatujui hatma ya hao madiwani na uchagizi bado.
Mboya ni mmoja kati ya wachochezi wa vurugu zote za Arusha.
 
Huyo anaye jiita Mboya mkaanga ndizi Elerai chini pale,hana lolote kwenye chama hususan siasa haziwezi ni kelele tupu na kuchochea vurugu,lengo lake sie tuna lijua na matarajio yake ni kugombea udiwani kata ya Elerai na ukweli ni kuwa hata akigombea hakuna wa kumpa,kama huamini ingia elerai uliza utaambiwa ye ni mtu wa aina gani,akipitishwa kugombea udiwani basi atambulia kura ya mke wake na wapembe wake wasio zidi 10,hana lolote kwenye siasa,kinacho nishangaza ashajitangaza kuwa ye ndo diwani mtarajiwa wakat ndo kwanza yuko chini ya ungalizi kwa mwaka mzima,
Anacho jivunia kisa Lema mjomba wake,kwani chama ni cha kina lema,
We mboya kila ulicho jaribu kukifanya kina kushinda sasa unakimbilia siasa ni nadhani ni wakati wewe kujipanga upya hujui undako.

Kamanda hapa umemaliza kabisa na sina cha kuongezea kwa leo huyo jamaa na wapambe wake wakalale kwa afya zao za baadaye wakuja kufa na shinikizo la damu maana CDM. Wahuni hawana nafasi tena.
 
Nanyaro,
usiishie hapo weka maelezo huyo Mboya ni nani na nini kilifanyika mpaka Kamati Tendaji ikafikia maamuzi yaliyofikiwa.

Asante Rais wangu wa moyoni kwa maelekezo sahihi maana huyu Mboya aliwatishia makada wa CDM. Na kutaka hata kumgonga na gari mmoja wao aliposhindwa alimtishia kumuua kwa gharama yoyote na mashahidi wapo waliona tukio hilo na anachunguzwa na Polisi na kama ataendelea kuleta siasa chafu ndani ya chama atajimaliza na kupotea kabisa kwenye wigo wa siasa.
 
Kichenchede!!!
5.jpg
kwa style hii chama sikiachi ng'o mseme msemavyo!!!!! nitakufwa na CCM yangu!!!
 
nanyaro tuna shida hapa arusha..hayo majibu unayotoa ni ya mkama ya kusema ccm ipo imara wakati inachechemea..hatutaki kufika huko..chadema sio chama chako..tatizo lipo..huyo mboya mi simfahamu ila nimepata jana hizi taarifa..otherwise utuambie chama kinashughulikia hili suala..kama unaona huwezi achia kiti waje wengine..
 
Sasa nyie Chadema-Kata mnapinga hakuna mgogoro Arusha, wakati wenye chama kina Slaa, wanautambua huu mgororo ingekuwa uzushi hii thread wangeifuta.

Jaribu kuwa mwelewa magamba aliyeleta hoja amesema kuwa kuna mgogoro wa viongozi kufukuzwa na kama ulisoma awali nilijaribu kuelezea vizuri sana kuhusu Mboya ni kwamba siyo kiongozi wa chama kwa zaidi ya mwaka na na alikuwa anachunguzwa na hakutakiwa kugombea nafasi yoyote ile mpaka tamko litoke kamati kuu lakini yeye kwa uhuni wake wakati sisi tumekwenda kwenye mkutano Kata ya Olorieni Kijenge na huku kulikuwa na kifo cha Regia Mtema Mbunge yeye akatumia nafasi hiyo kwa kuwaingiza wapambe wake na kujichagulia nafasi anayotaka.

Huyo ni muhuni kama wahuni wengine wanaotumika na magamba pamoja na madiwani wasaliti.

Kuhusu kuwa na undugu na Lema Mbunge asitegemee upenyo wa kirahisi maana Lema hauzwagi bei nafuu namna hiyo ni mpambanaji na anaweza hata kumkana kama ataleta mambo ya kihuni kwenye chama kama taasisi siyo mali ya familia kama wengi mnavyopenda kusema Mboya atafukuzwa uanachama na wengine wote ambao wanashabiakia uhuni ndani ya chama na CHADEMA KITAENDELEA SIKU ZOTE.
 
Asante Rais wangu wa moyoni kwa maelekezo sahihi maana huyu Mboya aliwatishia makada wa CDM. Na kutaka hata kumgonga na gari mmoja wao aliposhindwa alimtishia kumuua kwa gharama yoyote na mashahidi wapo waliona tukio hilo na anachunguzwa na Polisi na kama ataendelea kuleta siasa chafu ndani ya chama atajimaliza na kupotea kabisa kwenye wigo wa siasa.

Ni kweli huyu jamaa ana kesi nyingi kabla ya kujiingiza kwenye siasa na baada ya kujiingiza ndo zimezidi,kikubwa hapa huyu bwana hana Elimu na waweza kosa elimu lkn ukawa na busara na hekima lakini yeye hanavyote zaidi ya majigambo na vitisho visivyoo kuwa na msingi zaidi ya kuzidi kuonyesha upupu wake.
Alisha wahi kaa magereza kwa kesi za wizi akiwa dereva tax,bado anakesi kama tatu ambazo anachuzwa zikiwemo za uchochezi.
Chadema kama wanataka uendelea kuishika Arusha wanapaswa kuweka viongozi Imara wenye Elimu, maadili na utu,sio kuumpa mtu anaye tafuta sifa kwa lazima.
 
Wanabodi.
Baadhi ya viongozi wa Chadema kata ya Elereai, wamepinga kufukuzwa kwao madarakani na kuhishutumu kamati ya utendaji ya wilaya chini ya Mwenyekiti wake, Efatha Nanyaro.

Viongozi wanaopinga kufukuzwa madarakani ndani ya kata hiyo ni pamoja na Mwenyeketi wa Kata ya Elerai, Dominick Mboya na Katibu wake Joseph Warioba.

Wengine Mwenyekiti wa Wazee, Bakari Kasembe, Mwenyekiti wa Vijana, Paul Maganga, na Katibu wake, Sia Temu, Mwenyekiti wa Wanawake, Mariam Suleman pamoja na mweka hazina. Baraka.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa viongozi hao, Dominick Mboya alisema kwa mujibu wa katiba ya Chadema kamati tendaji ya wilaya haina mamlaka ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi uliowaingiza madarakani, kilichofanyika ni uhuni na ubabe tu.

Hizo ndio siasa za Chadema Arusha.
hii inatoa picha mbili kwanza kukomaa kwa demokrasia ndani ya chama kila mtu anaruhusiwa kutoa maoni yake au kupinga chochote bila woga fanya hivo kwa chama magamba kama hujawa kolimbalized, pia sura ya pili ni kuwa kwa CDM kuvuana magamba hakuhitaji mlomlongo mrefu ukikosea au ukihisiwa tu umekosea unavuliwa gamba on the spot unapewa nafasi ya kujitetea ukishindwa ngoma inachwea!! sio magamba miaka mitano sasa inaisha wanavutana kuhusu gamba!!
 
nanyaro tuna shida hapa arusha..hayo majibu unayotoa ni ya mkama ya kusema ccm ipo imara wakati inachechemea..hatutaki kufika huko..chadema sio chama chako..tatizo lipo..huyo mboya mi simfahamu ila nimepata jana hizi taarifa..otherwise utuambie chama kinashughulikia hili suala..kama unaona huwezi achia kiti waje wengine..


Hata kama tatizo lipo kikawaida haliwezi wekwa hadharani kama ufikiliavyo,kinachotakiwa ni kuketi na kutatua mgogoro kwa njia za amani,hata siku moja migogoro ya kisiasa ndani ya chama haitatuliwi kupitia makelee ya mitandaoni ama mageziti,kwani kila chama cha siasa kina kanuni,sheria na taratibu zake,kupitia hizo ndivyo migogoro hutatuliwa na ukienda kinyume na matakwa ya katiba,sheria,kanuni na taratibu za chama basi ni vyema ukajiengua kabla ya kulazimishwa kuondoka

Nadhani
Nanyaro ni mtu aliyeiva kisiasa na hii inaonekana kwa majibu yake,kwa hiyo ni vyema mgogoro huo ukatatuliwa ilikuepusha misuguano na ndivyo siasa inavyokwenda,pindi kunapokuwa na mpishano,tunatakiwa kutatua mivutano hiyo na si kufukuzana,

mfano mzuri ni wenzetu wa ANC mda si mrefu kijana Marema atapewa mda tena wa kujitetea na ikionekana hana hatia,atakuwa huru ktk kifungo ama kupunguziwa adhabu

Nawaomba CDM nao watatuwe matatizo yao kupitia mifano hiyo na sio kufukuzana kama ilivyotokea kwa CUF na NCCR na hiyo huleta mifarakano na makundi kwa wanachama na hupunguza mtaji wa kura,

nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko
 
Pata upupu wa huyu bwana mwaka jana mwishoni aliitisha mkutana wa serikali ya kata yeye na katibu Tarafa tena usiku wa saa2 kisa kumjadili Mtendaji amekamatwa na aliye mchongea kukamatwa kwakwe,sasa. Aliitisha mkutano na kuhudhuria kama nani kwenye serikali ya kijiji,hatma yake waliishia kukamatwa.
Huyu jamaa yuko kama mwiko.
 
Pata upupu wa huyu bwana mwaka jana mwishoni aliitisha mkutana wa serikali ya kata yeye na katibu Tarafa tena usiku wa saa2 kisa kumjadili Mtendaji amekamatwa na aliye mchongea kukamatwa kwakwe ni yeye,sasa, Aliitisha mkutano na kuhudhuria kama nani kwenye serikali ya kata,hatma yake waliishia kukamatwa,yeye na katibu Tarafa
Huyu jamaa yuko kama mwiko.
 
Mkuu Nanyaro mleta hoja katoa maelezo yanayojitosheleza kata majina na nyazifa wanazoshikilia,eneo na nk wewe unakanusha bila kutoa maelezo ya kina yatakayojitosheleza.Kwahiyo unataka kutuambia Dominick Mboya bado ni mweyekiti wa Elerai na Joseph Warioba I hope si waziri mkuu mstaafu bado ni Katibu ?.

CHADEMA Arusha,hakuna mgogoro,chama kipo IMARA,kuliko kipindi kingine chochote,
 
Back
Top Bottom