Kamende
JF-Expert Member
- Mar 1, 2008
- 416
- 45
Wajameni nimelazimika kuingia jukwaani jioni hii na kuleta msimamo wangu kwa mujibu wa mambo yanavyoendelea siku kwa siku ili yatakapotokea makubwa zaidi ifahamike wazi nani kichocheo kikuu cha matatizo yote ya Arusha.
Mheshimiwa WM Pinda December mwaka jana aliiahidi CHADEMA kwamba ifikapo Januari 5 mwaka huu atakuwa amemaliza tatizo la utata wa kuchaguliwa meya wa jiji la Arusha. Akawaomba wasifanye maandamano yoyote wala kuchukua hatua yoyote kwani ana uhakika wa kutatua tatizo hilo.
Mhe. Pinda alinukuliwa akisema bungeni kuwa Mauaji ya Arusha yalisababishwa na CHADEMA na hivyo wao ndo wakubebeshwa lawama. Hata pale Mhe. Lema alipoleta ushahidi bingeni kuonyesha wazi kwamba WM aamelidanganya bunge bado si bunge wala serikali ilishadiriki kuweka ushahidi huo bayana.
mazungumzo ya kinachoitwa MUAFAKA WA ARUSHA yamefanyika kwa maelekezo ya Uongozi wa CHADEMA kwamba "kwa kweli kuna umuhimu wa kumaliza sintofahamu ya Arusha kwa kujadiliana na kuafikiana namna njema ya kufikia MUAFAKA WA HAKI KWA PANDE ZOTE. Katika madai ya muhimu ya CHADEMA kwenye meza ya majadiliano zilikuwepo hoja kuu zifuatazo:
Ipo nguvu kubwa sana inashinikiza miuafaka huu ubaki ulivyo. lengo ni kumnusuru Pinda na tuhuma za kuongopea bunge na pia kuinusuru CCM na dhambi ya kusababisha umwagaji wa Damu kwa tamaa yao ya kutawala kwa nguvu.
Waungwana hebu angalieni ukweli ninyi wenyewe; iko sababu gani ya kuukubali MUAFAKA wa kugawana madaraka tu na kuachana na hoja zote hizo nyingine? Kwa nini serikali inataka kuamini kuwa inaweza kuwaendesha watu wote kama wajinga?
Kwa hakika kama Pinda anataka amani itamalaki Arusha, aondoe wingu linalofunika MUAFAKA huu feki kwa kuondoa kila visingizio vya kinafiki. Likitokea lolote sasa Arusha hakuna namna litakavyokosa kuunganishwa moja kwa moja na WM Mizengo Pinda.
Umefika wakati muafaka kwa WM kupasuka kichwa akitafuta namna ya kuzima mioto yote ya mgogoro wa Arusha kwani yeye ndiye aliyeuwasha, akauchochea, akauongezea magogo na sasa unafikia kiwango cha kutozimika kirahisi tena.
Wakuu naomba kuwasilisha!!!

- Kwamba uchaguzi wa Meya uliowapa CCM ushindi ulikuwa batili na kwa hiyo lazima kuwepo mgawano mpya wa haki wa madaraka.
- Kwamba serikali iwajibike kuwafidia marehemu waliofariki kutokana na vurugu zile za tr. 5/1/2011
- Kwamba majeruhi wanaoendelea na matibabu wapatiwe huduma stahiki
- Kwamba OCD wa Arusha (W) awajibishwe kwa aliyoyafanya binafsi.
- Kwamba kesi iliyoko Mahakamani dhidi ya Viongozi wa CHADEMA walioandamana tr. 5/1/2011 ifutwe.