Mgogoro Arusha - Tatizo ni Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro Arusha - Tatizo ni Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamende, Aug 3, 2011.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wajameni nimelazimika kuingia jukwaani jioni hii na kuleta msimamo wangu kwa mujibu wa mambo yanavyoendelea siku kwa siku ili yatakapotokea makubwa zaidi ifahamike wazi nani kichocheo kikuu cha matatizo yote ya Arusha.

  Mheshimiwa WM Pinda December mwaka jana aliiahidi CHADEMA kwamba ifikapo Januari 5 mwaka huu atakuwa amemaliza tatizo la utata wa kuchaguliwa meya wa jiji la Arusha. Akawaomba wasifanye maandamano yoyote wala kuchukua hatua yoyote kwani ana uhakika wa kutatua tatizo hilo.

  Mhe. Pinda alinukuliwa akisema bungeni kuwa Mauaji ya Arusha yalisababishwa na CHADEMA na hivyo wao ndo wakubebeshwa lawama. Hata pale Mhe. Lema alipoleta ushahidi bingeni kuonyesha wazi kwamba WM aamelidanganya bunge bado si bunge wala serikali ilishadiriki kuweka ushahidi huo bayana.

  mazungumzo ya kinachoitwa MUAFAKA WA ARUSHA yamefanyika kwa maelekezo ya Uongozi wa CHADEMA kwamba "kwa kweli kuna umuhimu wa kumaliza sintofahamu ya Arusha kwa kujadiliana na kuafikiana namna njema ya kufikia MUAFAKA WA HAKI KWA PANDE ZOTE. Katika madai ya muhimu ya CHADEMA kwenye meza ya majadiliano zilikuwepo hoja kuu zifuatazo:
  1. Kwamba uchaguzi wa Meya uliowapa CCM ushindi ulikuwa batili na kwa hiyo lazima kuwepo mgawano mpya wa haki wa madaraka.
  2. Kwamba serikali iwajibike kuwafidia marehemu waliofariki kutokana na vurugu zile za tr. 5/1/2011
  3. Kwamba majeruhi wanaoendelea na matibabu wapatiwe huduma stahiki
  4. Kwamba OCD wa Arusha (W) awajibishwe kwa aliyoyafanya binafsi.
  5. Kwamba kesi iliyoko Mahakamani dhidi ya Viongozi wa CHADEMA walioandamana tr. 5/1/2011 ifutwe.
  Alipopelekewa draft ya kwanza tu ya kuanza kwa MAJADILIANO na akijua kuwa madiwani wana kikomo cha MAKUBALIANO Pinda aliwakwepa viongozi wa CHADEMA siku hadi siku kwa lengo la kuhakikisha kuwa MUAFAKA unafikiwa kwa makubaliano kwenye hoja ya kwanza peke yake. Wakati huo shughuli zote za uratibu wa MAJADILIANO zilikuwa zikifanyika chini ya Mhe. Raymondo Mushi - DC wa Arusha.

  Ipo nguvu kubwa sana inashinikiza miuafaka huu ubaki ulivyo. lengo ni kumnusuru Pinda na tuhuma za kuongopea bunge na pia kuinusuru CCM na dhambi ya kusababisha umwagaji wa Damu kwa tamaa yao ya kutawala kwa nguvu.

  Waungwana hebu angalieni ukweli ninyi wenyewe; iko sababu gani ya kuukubali MUAFAKA wa kugawana madaraka tu na kuachana na hoja zote hizo nyingine? Kwa nini serikali inataka kuamini kuwa inaweza kuwaendesha watu wote kama wajinga?
  Kwa hakika kama Pinda anataka amani itamalaki Arusha, aondoe wingu linalofunika MUAFAKA huu feki kwa kuondoa kila visingizio vya kinafiki. Likitokea lolote sasa Arusha hakuna namna litakavyokosa kuunganishwa moja kwa moja na WM Mizengo Pinda.

  Umefika wakati muafaka kwa WM kupasuka kichwa akitafuta namna ya kuzima mioto yote ya mgogoro wa Arusha kwani yeye ndiye aliyeuwasha, akauchochea, akauongezea magogo na sasa unafikia kiwango cha kutozimika kirahisi tena.

  Wakuu naomba kuwasilisha!!!
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sounds good to me!
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  PM ndiyo tatizo! Lakini pia taarifa kutoka juu CDM kushuka kwa viongozi wa chini hazikuwa nzuri
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nadhani PM ni tatizo kwa mengi, yupo kama kipozeo tu, hovyo!
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  This sounds stupid to me. Mgawano wa haki wa madaraka ndiyo kitu gani? Leo utawaambiaje hao madiwani kuwa walichofanya siyo kutekeleza hayo maagizo ya makao makuu? Ubebe lawama huo uongozi wa CDM uliotoa hayo maelekezo na siyo Pinda!
   
 6. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi hayo majadiliano kuanzia namba moja mpaka namba tano ni viongozi gani walioandaa CDM taifa au CDM mkoa!

  Naona Madiwani wameyafanyia kazi haya majadiliano namba moja ya kugawana madaraka wakati watu wauwawa na wengine wana vilema vya maisha
   
 7. g

  graceirene Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kipengele cha kwanza kinasema uchaguzi wa meya urudiwe , mtoa mada huenda amepitiwa au anamaslahi na kipengele hicho
   
 8. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ninawasiwasi na aunthenticity ya hizo dondoo. Ni kweli ndizo zilizokuwa dondoo za CDM??? Kwani hiyo namba moja imekaa vibaya sana. Namba Moja nahisi ni kurudia uchaguzi wa Meya sio kugawana madaraka. Kama ndivyo ilikuwa kama unavyowakilisha ni upuuzi tu.
   
 9. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili mbona linaeleweka toka siku nyingi na hisi hata kamanda wetu Dr. W.Slaa alishalijua hilo ndiyo maana taratibu za chama zinafuatwa kuwawajibisha wale wote waliohusika na ujinga kama huu.
   
Loading...