Mgodi wa dhahabu buhemba watelekezwa

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,536
2,000
Ivi ni kwamba madini yameisha chini au?
Nasikia vitu vimeanza toweka wakati kuna walinzi
Mbaya zaidi wameacha MASHIMO jamani ivi hii serikali iko serious bse ata sustainable environmental protection zero.
In years to come tutashuhudia mengi
So far how much have we gained as a nation akina Lissu kuna haja ya kuhoji ili bungeni
 

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,452
2,000
Yaani nchi hii tutatabakiziwa mashimo,hivi yale Mabwawa hawawezi kufuga Samaki... Au yatakuwa na sumu...
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,606
2,000
Mwekezaji siku mingi hayupo nchini..........baada ya kugundua amemaliza kutuibia kwa kibali cha serikali ya kifisadi ya CCM ambao hata ukiwauliza leo huyu mwekezaji mchango wake kwenye pato la taifa ni nini.........hawawezi kukuambia.................maji sumu yanatiririka kuelekea maakazi ya watu........sijui mwisho wetu utakuaje...............inakuwa kama vile tunalaana vile..................na huu umasikini wa kujitakia..........
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,536
2,000
Inakera alafu inaudhiiiiiiiiiiiiiiiii
Tz tutakuja bakiwa na mashimo tuu
 

TGS D

Senior Member
Aug 3, 2010
114
0
Jey Kei na Wengine wapo bize kuchakachua baraza la mawaziri. Nchi imeishauzwa kwa mafisadi.

Sidhani hata kama wana hiyo habari.

Inasikitisha sana watu wanachukua mali yetu, wanaondoka wanatuachia mashimbo na vifusi vya mawe huku hatujanufaika kitu chochote.Angalia mazingira yanayozunguika mgodi halafu linganisha na thamani ya mawe yanaochibwa hapo, unaweza kulia kwa kweli.

Pole Tanzania, CCM hii...... Ole wao!!!!!!!!!!
 

bhageshi

JF-Expert Member
Jul 24, 2010
264
195
Mtoa mada Njowepo napenda nikukumbushe kuwa unapozungumzia mgodi wa buhemba unazungumzia Meremeta, na unapozungumzia wawekezaji unazungumzia watanzania wenzako ila wao wenye mlengo wa kifisadi tena ni ambao walipewa dhamana ya juu kabisa na wananchi katika uongozi. Hivyo kusema wametuachia mashimo si sahihi kwani wamo humuhumu nchini wakivinjari ila uongozi uliopo hauna uthubutu kuwakamata ili kuwajibika na mshimo hayo. kwa taarifa yako hii ni issue iliopelekea Waziri Mkuu kuapa kuwa yupo tayari ku....... kuliko kutoa siri ya Jeshi. Mgodi huo baada ya kusimamishwa ulinzi wake ni vijana wa IGP Said Mwema na wanaelewa kabisa kinachoendelea au kilichoendelea hapo na ni wao kabisa ndio wanaoendesha zoezi zima la kuingiza wezi na kuiba vifaa na mshine hizo. Kipindi kijacho 2015 nakuomba uwe tayari kupigwa maji ya upupu ili kuikomboa nchi hii kutoka kwa wakoloni Mafisadi.
 

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
500
Baada ya kusikia habari za Buhemba kwa muda mrefu niliamua kutembelea kijiji kile mwaka jana. mmm ni huzuni imetengenezwa milima ya uhakika na hakuna dhahabu tena na maisha ya wale watu yako katika ufukara wa kutisha chini ya Mbunge wao mkono kwa mkono watu wake wamezama kwenye ufukara wa kutisha wakizungukwa na milima bandia huku dhahabu yao ikiwa imekwenda na wajanja wanaoitwa wawekezaji au maarufu kama meremeta
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,536
2,000
Kumbe Buhemba=Meremeta naona hakuna haja ya kushangaa.
Asante mkuu kwa kunipa connection.
Tz itaendelea kuwa shamba la bibi hadi lini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom