Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,717
- 47,222
Kuna taarifa kuwa mgodi wa dhahabu ambao awali ulikuwa unamilikiwa na kampuni ya Barrick umesimamisha uzalishaji kutokana na kushindwa kujiendesha.
Kampuni ya Baarick ndiyo iliyoujenga mgodi huo, na kisha kufanya uchimbaji wa dhahabu na baadaye kuamua kuondoka. Waliondoka huku wakiwa wameacha deposit ndogo ambayo ilihitaji pit mpya. Mpaka Barrick wanaondoka kwenye mgodi huo, mgodi wa Tulawaka na ule wa North Mara, ndiyo inayotajwa kuwa ilikuwa ikiendeshwa kwa faida.
Serikali iliomba iachiwe deposit iliyokuwa imebakia, miundombinu yote ikiwemo plant na majengo. Mgodi huo ulikabidhiwa kwa STAMICO, nayo kwa kupitia kampuni yake ya STAMIGOLD waliamua kufanya biashara ya uchimbaji wa dhahabu, huku wakiwa wamepewa vitu vyote bure na mwekezaji, ikiwemo plant, majengo, miundombinu mingine zikiwemo barabara, waste dump, maji, umeme, n.k. Jambo la kushangaza ni kwamba pamoja na kupewa vitu vyote hivyo bure, mgodi huo umeshindwa kujiendesha kwa faida na kufikia kuzalisha dhahabu kwa gharama ya U$1,500 na kuiuza kwa U$1,200 kwa ounce moja.
Awali, hesabu zote zilifanyika, na kuonekana kuwa uchimbaji wa deposit iliyobakia, ungefanyika kwa faida. Mpaka sasa mgodi huo unadaiwa na wazabuni mbalimbali kiasi kinachofikia shilingi zaidi ya bilioni 50. Fedha hiyo sasa ni lazima italipwa na serikali kwa sababu STAMIGOLD hawana uwezo wa kulipa.
Tuna mambo ya kujiuliza:
1) Kama serikali ilipewa vitu vyote hivyo bure, ikashindwa kufanya uchimbaji dhahabu kwa faida, je ingegharamia kila kitu kungetokea nini?
2) Tumekuwa tukiwalaumu sana wawekezaji wa nje kuwa wanatuibia, lakini wao wanaweza kuchimba kwa faida, kulipa mrabaha, kulipa corporate tax (japo ni mpaka wanapokuwa wamerejesha mitaji yao), hivi sisi tuna uwezo wa kuanzisha na kuendesha hii miradi ya uchimbaji madini?
3) Serikali na Watanzania tunajifunza nini kuhusiana na sekta hii baada ya STAMIGOLD kushindwa kufanya shughuli za uchimbaji wakati wakiwa wamepewa karibia kila kitu bure?
4) Hivi Watanzania na serikali wanatambua kuwa utafiti na uchimbaji madini, siyo sawasawa na kuchota maji, na kuwa (mining business) ni kati ya biashara zenye uwezekano wa hasara kubwa kuliko biashara nyingine yeyote?
5) Hivi kuna faida gani kuanzisha miradi ambayo badala ya kuleta mapato kwa serikali, yenyewe ndiyo inayotafuna hela za walipa kodi?
6) Kwa nini serikali haioni busara kuachana kabisa na shughuli za kibiashara kutokana na uzoefu tulioupata kuwa serikali yetu haijawahi kuendesha biashara yoyote kwa faida?
7) Matukio haya yanatupigia kengele kuhusu utendaji mbovu wa TANESCO, ATCL, TTCL, POSTA, Reli, TPA, n.k. Ninaamini kuwa shughuli zote zinazofanywa na makampuni tajwa, kama zingekuwa zinafanywa na sekta binafsi, huenda tungepata faida kubwa kiasi cha kupindukia. Kwa bahati mbaya, serikali ambayo ina uzoefu mkubwa wa kushindwa kuendesha biashara ndiye msimamizi mkuu wa akampuni haya.
USHAURI
1) Tanzania tunahitaji sana wawekezaji wa nje na ndani katika sekta ya madini, pengine kuliko sekta zote kutokana na mahitaji makubwa ya mitaji, uzoefu na risk ambazo zipo kwenye sekta hii. Serikali haitafanikiwa kufanya uchimbaji wa madini yoyote kwa faida kwa mfumo uliopo. Jukumu la serikali liendelee kuwa katika usimamiaji wa sera na sheria.
2) Wawekezaji, wawe wa nje au wa ndani, ni wadau wa maendeleo. Mahusiano ya wadau hawa na serikali ni lazima yawe ya maelewano na kiurafiki kwa faida ya wananchi wote. Kwa sasa, wawekezaji, hasa kwenye sekta ya madini, wanaonekana kama adui wa serikali. Mfano mzuri ni suala la linaloitwa mchanga wa dhahabu lilivyochukuliwa na kushughulikiwa. Wengi hawajui athari zake lakini limeiamsha Dunia kuwa Tanzania siyo mahali salama kwa makampuni ya kigeni kuwekeza kwenye madini.
3) Serikali ni lazima ifanye kwa ukaribu sana na wawekezaji katika sekta hii. Kwa sasa, takwimu zinaonesha ukuuaji wa uchumi wetu unasababishwa na sekta ya madini na utalii. Hiyo ni ishara tosha kuwa serikali inatakiwa karibu sana na sekta hizi mbili kutokana na nafasi zake kwenye uchumi wa nchi. Mafanikio kwenye biashara siku zote huwa makubwa katika maelewano kuliko penye uadui, visa, visasi au kukomoana.
4) Serikali iangalie uwezekano wa shughuli zote za kibiashara, uendeshaji wake kufanywa na sekta binafsi na serikali kubakia tu kama wabia. Makampuni kama TANESCO, TTCL, ATCL, TPA, etc, yanatakiwa kubomolewa ili yasiendeshwe na serikali.
MWISHO
Kauli aliyoitoa Waziri Mkuu alipotembelea mgodi wa Buzwagi ilikuwa ya kiungwana. kwa maneno yake, alitamka, 'Tanzania bado tunahitaji sana wawekezaji wa nje. Tunayaomba makampuni ya madini yaendelee na shughuli za uchimbaji bila wasiwasi wowote. Kinachofanyika kwa sasa kuhusiana na mchanga wa dhahabu ni kuchukua vipimo, na kisha kuptia sheria zetu, na kujiridhisha kuwa tunacholipwa ndiyo tunachostahili kulipwa'. Kauli ile ilikuwa nzuri, na ndiyo iliyostahili kutolewa toka mwanzoni kabisa kuliko kauli zile kuwa , 'makampuni yamekuwa yanaiibia sana nchi hii', wakati hatujui hata tunaibiwa kwa namna gani na kiasi gani. Na naamini haikuwa sahihi kusimamisha upelekaji wa mchanga nje kabla ya kufanya uchunguzi kwanza, na kujiridhisha kuwa tumesimamisha kwa vile tunaamini kuna ukiukaji wa makubaliano.
Ambayo yametokea ni kujikwaa kwa namna fulani kwa serikali, ni wakati wa kujirudi, na kujenga mahusiano mapya ya kuaminiani, kirafiki na maelewano kati ya wawekezaji katika sekta ya madini, serikali na jamii.
Tutambue kuwa baada ya kukosekana kwa pesa ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya madini kwa karibia miaka mitano, sasa kuna pesa za kutosha kwenye masoko ya fedha Duniani ambayo ni kwaajili ya uwekezaji kwenye sekta ya madini. Tanzania haijaweza kufaidika na uwepo wa pesa hizi kutokana na Dunia kuiona Tanzania siyo mahali salama sana kwa mitaji ya nje.