Elections 2010 Mgaya anang'ata Kongoli, ana meno sasa!

Chonde chonde kuna mtu mwenye clip ya statement ya Kikwete kukataa kura za wafanyakazi?, inahitajika sana kwa sasa, hata ikiwa Mp 3 itakuwa poa tu, naihitaji kuiweka kwa simu yangu iniongezee machungu na kupandisha mori!
 
Pia suala la salary linaathiri pia sekta binafsi. Kwa sababu katika sekta binafsi vyama vya wafanyakazi havina nguvu na mahali pengine havipo. Wafanya kazi sekta binafsi wapo wengi, wahamasishwe pia ili wampigie Dk Slaa kura. Wafanyakazi sekta binafsi hawana pa kusemea. Wenye makampuni au waajiri sekta binafsi wako after big profit na kumbuka wanachangia ccm ili wawadhulumu wafanyakazi na kukwepa kodi.
 
Chonde chonde kuna mtu mwenye clip ya statement ya Kikwete kukataa kura za wafanyakazi?, inahitajika sana kwa sasa, hata ikiwa Mp 3 itakuwa poa tu, naihitaji kuiweka kwa simu yangu iniongezee machungu na kupandisha mori!


Mkuu ukiipata mie nipe naifanyia remix then tunaingia Studio na mzee Mr II ngoma lazima iwe in music things...Itatupa midadi ya kuzidi kumchukia huyu jamaa..
 
Wafanyakazi katika nchi nyingi wana nguvu ya kudetermine nani waunde serikali. Kwa mfano wafanyakazi wa SA huwezi kushinda uchaguzi kama huungwi mkono na chama cha wafanyakazi, na vyama vya wafanyakazi SA huwa na msimamo wa kuchagua chama na mgombea watakaye muunga Mkono. Nadhani huu ndio wakati ambapo TUCTA inaweza kurudisha uhai wa vyama vya wafanyakazi na pia kuwafufua wafanyakazi tena, Mgaya anatakiwa kuwa na strategic meeting na kamati zake ili waweze kulobby kwa wagombea namna watakavyoweza kuwasaidia kushinda uchaguzi lakini nao watakavyoweza kuboresha mazingira ya wafanyakazi at the same time lazima wakubaliane terms za kuboresha uzalishaji na kuongeza tija ya utendaji kazi wa wafanyakazi.
 
Kwa kusema ule ukweli wa kutoka rohoni, siwaamini wafanyakazi (TUCTA). Nikikumbuka historia yao, mmmmhhh!
 
Kwenye nyekundu ni takwimu ya mwaka gani?? Hivi wafanyakazi ni asilimia ngapi ya Watanzania wote? Maana sasa nchi hii inataka kuwa ni wafanyakazi kila siku. Na wangapi ndio wanaopiga kura??? Ufanisi wa hao wafanyakazi ukoje? Wanawahi kazini?? Hawaibi? Rushwa na utendaji wao ukoje? Mbona hatujawahi kuona shirikisho hili likisimama kidete kwenye kuzorota kwa utendaji?

aanze kwa kuwaambiwa hawa wafanyakazi wajibu wao kwanza ingependeza maana kwa kweli ufanisi wao haueleweki. Ndio maana mara customer service, rushwa, ardhi nk. Hawa wote ni wafanyakazi.

Kwa vyovyote utakuwa MKWERE WEWE! sasa changanya na zakwako nadhani utajitambua
 
Huyu Mgaya na TUCTA yake ndiyo wanaomharibia Dr Slaa. Tayari pingamizi limeshaandaliwa mafisadi wanasubiri Dr Slaa arudishe fomu ndipo wamwekee pingamizi kwenye Tume ya Uchaguzi aenguliwe kwa kukiuka utaratibu, ati ameanza kampeni kabla ya muda.

TUCTA wangesubiri Dr Slaa apate uteuzi wa Tume ya Uchaguzi ndipo waanze kuhamasisha apigiwe kura. Hili pingamizi likifanikiwa sitawasamehe wote watakaokuwa wamesababisha.
 
Huyu Mgaya na TUCTA yake ndiyo wanaomharibia Dr Slaa. Tayari pingamizi limeshaandaliwa mafisadi wanasubiri Dr Slaa arudishe fomu ndipo wamwekee pingamizi kwenye Tume ya Uchaguzi aenguliwe kwa kukiuka utaratibu, ati ameanza kampeni kabla ya muda.

TUCTA wangesubiri Dr Slaa apate uteuzi wa Tume ya Uchaguzi ndipo waanze kuhamasisha apigiwe kura. Hili pingamizi likifanikiwa sitawasamehe wote watakaokuwa wamesababisha.
Kumbe mafisadi ndio wameandaa pingamizi sasa inauhusiano gani na TUCTA kumharibia Slaa unachanganya sana mambo kajipange upya ndipo uje tena, kuna magreat sinka hawadanganyi na story za kuchonga.
 
Mbona sielewei elewi?! Wakati ule ilikuwa ni kipindi kuelekea World Economic Forum(Africa)! Yanakuja kuibuka tena kipindi cha kuelekea kwenye kampeni na hatimae uchaguzi mkuu! What's behind the scene?! Siwezi kum-support kwa sababu i am convinced kwamba huyu jamaa anawatumia wafanyakazi kwa maslahi yake! Vilevile am not convinced coz' naona anapoteza muda wake kv najua ni asilimia ndogo sana ya wafanyakazi wa TZ hii unaoweza kuwaambia fulani ndie anaefaa halafu akakuelewa!

Red :maslahi yake yapi kivipi ?mbona unaongea tuhuma kubwa bila supporting evidence au wafanyakazi wakipandishwa mishahara anapata percentage kwa kila kichwa. Ukiuliza nyakati ulizo taja ni kujua muda gani wa kubonyeza na muda kani wa kusubiri peoples skill.
Blue :wewe aliyesema maneno ya dharau ,kejeli na vitisho kwa wafanyakazi mna maono sawa .
 
Tumehamia kwenye faida za kisiasa badala ya kuangalia MASLAHI YA WAFANYAKAZI & HUDUMA WANAZOTOA......! swali....UMEWAHI KUWA NA KESI MAHAKAMANI WEWE? HAKI ILITENDEKA? HUKUTOA CHOCHOTE?, UMEWAHI KUVAMIWA NA MAJAMBAZI? ULIRIPOTI POLISI? WALIKUPA MAJIBU GANI?......AU HUJAWAHI BAMBIKIWA KESI?.....HOSPITALINI UMEWAHI FIKA? ULIPOKELEWA KAMA MGONJWA AU KAMA KIBAKA?.....TRAFIKI WAMEWAHI KUKUSIMAMISHA BARABARANI? HAWAKUKUOMBA CHOCHOTE KWELI? NA KUKUTISHIA KUWA USIPOTOA WANAKUADHIBU ZAIDI?......UMEWAHI OMBA AJIRA HUKU UNA SIFA STAHILI? ULIPATA AU ULIKUSA? UNDAHANI KWA NINI ULIKOSA?.......HAWA NDIYO WATUMISHI UNAOWATETEA WANAOHUDUMIA JAMII? AU UNAHITAJI MTAJI WA KISIASA?
 
Ndugu yangu kama wewe upo private sector kaa kimya. Kuna watu wetu wa karibu sana wanafanya kazi serikalini kwa kujituma hasa lakini hakuna anayethamini nguvu zao.

Tanzania's public sector is a main employer and derives about 90% of the economy. Kama unakumbuka enzi za zamani wakati wa mei mosi rais alikuwa akitangaza kuongesha mshahara kwa 10% bei za vitu zinaongezeka kwa 40%. Hii ni kuonesha kuwa unapotaka kuleta maisha bora kwa kila mtanzania basi mlipe vizuri mfanyakazi ili akamuunge muuza nyanya, muuza mitumba etc.

Hivi kwa nini hujiulizi why kila mtu Tanzania anataka kuwa mwanasiasa hata kama ana taaluma nzuri ya kuendeleza?, Jibu ni kuwa nobody cares. Viongozi wote wa nchi, nasema tena wote hakuna hata mmoja mwenye kuangalia masilaahi ya nchi, what they want is personal gain and interests, colluding with corrupt businessmen to overstate prices of Govt supplies and take 10%.

Watanzania ni wachapa kazi wazuri sana kama unawalipa kulingana na kazi wanazofanya. Hao unawaongelea wezi, corrupt etc ni jambo dogo tu linalo wasumbua, wengi wao hela wanayolipwa haitoshi kuishi hata kwa wiki moja wakati huo huo kuna mtu analipwa kwa kusinzia mjengoni tu karibia laki tatu kwa siku. Wakurugenzi sina tatizo nao maana kama wanalipwa kutokana na taaluma yao haijalishi ila serikali haina mwenyewe. Yaani ni kama shamba la bibi kuchuma zaidi ya uwezo wako. Chief accounting officer wa nchi, rais kalala usingizi wa pono kwa kuogopa kudhuliwa/kurogwa kwa kuwachukulia hatua wezi rafiki zake.

Haiingii akilini mtu ana darasa la saba au form four failure anakaa mjengoni kwa miaka 5 akilala na kusema ndiyo anaondoka na 45M wakati Professor aliyefundisha kwa miaka 40 ana staafu na kupewa Tshs 10m au less. Tanzania inahitaji structural change kubwa sana ya kuanzia kwenye siasa mpaka kwenye utendaji. Tunahitaji mtu kama Dr. Slaa angalau kwa miaka mitano tu aturekebishie nchi yetu. Suala la nitawataja, nawajua, halisaidii. Bora kufa kishujaa kuliko kuishi kimbwa koko.
AKILI NYINGI SANA........Mapoints matupu.....
 
Chonde chonde kuna mtu mwenye clip ya statement ya Kikwete kukataa kura za wafanyakazi?, inahitajika sana kwa sasa, hata ikiwa Mp 3 itakuwa poa tu, naihitaji kuiweka kwa simu yangu iniongezee machungu na kupandisha mori!
Hapo mkuu
 

Attachments

  • Kama Hawataki wasinipigie.mp3
    770.3 KB · Views: 28

''We will decide whom to give the votes at the general meeting in September, after ascertaining that the presidential candidate has the interest of the workers at heart,'' Mr Mgaya, who was presiding over Researchers, Academician and Allied Workers Union (RAAWU) meeting, said.[/COLOR]
[/FONT]

.

Mr Mgaya, the answer is very very clear, I wonder why you haven't decided yet. VOTE FOR KIKWETE, because he promised NOT to increase your salaries even if you complain for eight years! Sasa huo mkutano mkuu wa nini? au ajenda hiyo katika mutano huo ya nini?
 
Back
Top Bottom