Mgao wa umeme: WaTanzania tuamke, tuukatae

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,396
7,968
Watanzania tumenyanyasika sana, tumeonewa sana, tumedhulumiwa sana, tumeumizwa sana na hii serikali yetu kwa hii migao ya umeme isiyokwaisha na inayokuja na visingizio lukuki.

Imefika wakati sasa tuamke na kudai haki yetu ya kupata umeme masaa 24 kama wanavyopata wao. Kwani wao wana haki ya nchi hii kuliko sisi?

Nani atutetee watanzania katika huu mgao mkali.
 
Naomba mnisaidie jamani maana mimi huu mgao sijui hata unakwendaje kwendaje,ratiba yao mimi kwangu ni kitendawili hata sijui nani anaweza kutegua.
 
Mada: FACEBOOK , MGAO WA UMEME , SENEGAL , Senelec , TANESCO , TWITTER

Pichani ni jengo la "Tanesco ya Senegal",Senelec,lililoshambuliwa na waandamanaji wenye hasira kuhusu kukatika umeme mara kwa mara jijini Dakar.Akina sie tunashambulia kwa matusi,lawama,na manung'uniko huko Twitter na Facebook!!!


Sio siri kwamba upole wa Watanzania ni miongoni mwa sababu kuu za mabaya mengi yanayotokea huko nyumbani.Na kama kuna suala linalosikitisha kuhusu mwamko wa Watanzania kudai haki zao ni tatizo la mgao wa umeme sambamba na ubabaishaji wa hali ya juu wa serikali na Tanesco katika kushughulikia tatizo hilo.


Sasa hivi,mitandao ya jamii ya Twitter na Facebook imetawaliwa na malalamiko ya Watanzania wengi kuhusu mgao.Wengine wanaishiwa na uvumilivu na kuishia kuitukana Tanesco,kana kwamba matusi hayo yatarejesha umeme.Wengine wamekuwa wakipeana taarifa kuhusu maeneo ambayo "Tanesco wameshachukua umeme wao".Kwa kifupi,kinachosikika zaidi ni manung'uniko,lawama,vilio na hata matusi.Cha kusikitisha ni kwamba hakuna dalili yoyote kutafsiri malalamiko hayo into vitendo.


Sio kama nawasimanga ndugu zangu.I really feel you lakini ukweli mchungu ni kwamba kelele zenu haziwezi kumaliza tatizo hilo.Kinachohitajika ni kudai haki kwa nguvu.By "nguvu" simaanishi vurugu bali kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha serikali na Tanesco wanawajibika.Mgao utaendelea milele iwapo Watanzania wataishia kulalamika tu.Hakuna miujiza katika kuleta mabadiliko.Either watu wajitoe muhanga kudai haki yao kama walipakodi au waendelee kuteswa na mgao.


Bahati nzuri,wenzetu nchini Senegal wanatuonyesha namna gani matatizo yanayoathiri nchi yanavyoshughulikiwa na umma.Nisieleze kwa maneno yangu bali naomba usome habari ifuatayo:

Associated Press


DAKAR,Senegal: Maelfu ya waandamanaji wameingia mitaani katika mji mkuu wa Senegal kupinga kukatika umeme mara kwa mara.Maandamano hayo ni tukio la tatu la vurugu nchini humo ndani ya wiki.



Wananchi wenye hasira walivamia ofisi za shirika la umeme la Senelec,jijini Dakar baada ya maandamano ya kupinga kukatika kwa umeme kwa muda mrefu.


Watu kadhaa walishambulia majengo ya serikali hapo jana.Wanadaia kuwa baadhi ya maeneo yamekuwa yakikosa umeme kwa masaa 24 au zaidi.



Kama ilivyo kawaida kwa vyombo vya dola barani Afrika,askari wa kikosi cha kutuliza ghasia walipambana na waandamanaji kwa kutumia maji na mabomu ya machozi.Msemaji wa polisi hakuweza kuthibitisha idadi ya waliojeruhiwa katika ghasia hizo.


Alhamisi iliyopita,vurugu kubwa ziliibuka kupinga mpango wa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo​

Uchaguzi ni wenu Watanzania wenzangu.Mwendelee kulalama huku Serikali na Tanesco wakiendelea kuwasanifu (mgao wa umeme hauwagusi kwa vile aidha wana jenereta zinazojazwa mafuta na hela yako mlipakodi au maeneo wanayoishi hayakatwi umeme kutokana na unyeti wake) AU muige mfano wa wenzetu wa Senegal.Hakuna njia ya mkato katika kutatua matatizo sugu yanayosababishwa na watendaji wasiotimiza wajibu wao.It's now or never!


hadi 2015 watakuwa wameshatuuzia majenereta mangapi? na vituo vya mafuta wanavyomilikii vitakuwa vimeshauza mafuta kiasi gani? THINK bIG
 
mkuu

mimi ninashauri Wiliam Ngeleja abebe virago yvake arudi nyumbani kwao sengerema, atabakia na cheo chake cha waziri wa nishati na madini kulipwa mishahara, shangingi pia atapewa na posho zote kama kawaida ya waziri halafu tumuombe balozi wa japan nchini tanzania asimamie utekelezaji wa sekta ya nishati na balozi wa Africa ya Kusini hapa nchini asimamie utekelezaji wa sector ya madini

nimekuwa na maono haya kwa sababu ndugu william ngeleja amekuwa hana uzalendo na nchi ya Tanzania
 
Mtumishi wa Mungu Rev. Kakobe alipoonewa na serikali pale walipoamua kupitisha umeme kwa nguvu kanisani kwake, alimlilia Mungu na kusema iko siku umeme hautawaka hadi hapo haki itakapotendeka.

Ndio haya sasa tunayoyaona, sio tu jiji la Dar limekumbwa na giza nene bali nnchi nzima. Watanzania tumrudie Mungu na tuache kudharau viongozi wa Mungu.
 
wacha wewe maneno mbofu mbofu, kakobe hayuko juu ya sheria, na wala hana uwezo wa kulaani umeme wa Tanzania, HP WA KULAUMIWA NI KIKWETE BADALA YA KUWAWAJIBISHA NGELEJA NA WENZIE NA KUTUMIA FEDHA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA UMEME YE ANACHEZEA HELA NYINGI KUSAFIRISAFIRI HOVYO KAMA VL HANA PA KUISHI, I real hate this guy
 
kwakweli nilishawaza ili sema ntaazaje pekee kwenda pale tanesco,ile mitambo na majenereta kuonyesha kwa vitendo hasira yangu?
tungepata wezetu japo 50 tu kweli serikali na JK na waziri wake wangeamka
 
Mwenye mkakati mzuri aulete mi niko tayari kuunga mkono,kwanza walioingia mkataba wa IPTL kama wako hai na wapo kwenye utendaji wa serikali hadi sasa hivi kwanini tusiwafukuze kinguvu sisi wananchi wenyewe..naombeni majina yao japo tuwafaham na hatua zingine zije..
 
Watanzania ni waoga sana!! Na hii ni effect ya kupata uhuru through peaceful means!
 
Naomba mnisaidie jamani maana mimi huu mgao sijui hata unakwendaje kwendaje,ratiba yao mimi kwangu ni kitendawili hata sijui nani anaweza kutegua.

Mkuu inategemea wewe unatoka Tanzania ipi. Cahnzo cha mgao au tatizo la umeme kinajulikana, lakini still bado watu wamelala. Tunatatzi la kulalamika tu lakini hatufanyi lolote.

Nakumbuka General Ibrahim Badamasi Babangida aliwahi kusema akiwa ziarani hapa Tanzania kuwa "it is easy to rule Tanzania than to ride a herd of cattle", wakati ule tuliona kejeli, lakini ni ukweli sasa tunauona. Ujinga huu ungetokea Lagos au Abuja sidhani kama "TANESCO" wa kule wangechekewa kama hapa.
 
Jamani mi niko tayari kujitoa muhanga kuhakikisha kama si kubadili utawala na watawala wa magamba basi hata wanaozuia mambo ya msingi yasijadiliwe kwa kisingizio cha kulindana, utawala bora bongo uko kwenye makaratasi tume zinaundwa na wanaotakiwa kuwajibika kuchunguza wanayotakiwa kuwajibika kwayo mf. Husein na mabomu, mwema na mauaji, ngeleja na umeme wa mgao miaka 50 ya giza uchumi tegemezi, chenji ya rada inatakiwa na magamba iliwe, ingewezekana hata hao BAE watuletee umeme kuliko kuwapa hawa magamba! imekuwa tz ya tume zisizo na tija wakati zinakula pesa zetu, upuuzi mtupu!!
 
ivi kwann wasifanye mwezi baada ya mwezi, mm siku baada ya siku wananboa hao tanesco!
 
Hivi kuna mgao? maana mie naishi karibu na baraza la maaskofu kurasini umeme upo 24/7
hongera sana mkuu!! Wakazi wa ilala na vitongoji vyake ni mateso matupu..inabidi tuandamane kama senegal..hapa napoongea wameshatukatia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom