Njo na bango lako ubungo mataa tukuunge mkono!!! Kama mkweliWatanzania tumenyanyasika sana, tumeonewa sana, tumedhulumiwa sana, tumeumizwa sana na hii serikali yetu kwa hii migao ya umeme isiyokwaisha na inayokuja na visingizio lukuki. Imefika wakati sasa tuamke na kudai haki yetu ya kupata umeme masaa 24 kama wanavyopata wao. Kwani wao wana haki ya nchi hii kuliko sisi? Nani atutetee watanzania katika huu mgao mkali.
Hivi kuna mgao? maana mie naishi karibu na baraza la maaskofu kurasini umeme upo 24/7
Mkuu inategemea wewe unatoka Tanzania ipi. Cahnzo cha mgao au tatizo la umeme kinajulikana, lakini still bado watu wamelala. Tunatatzi la kulalamika tu lakini hatufanyi lolote.
Nakumbuka General Ibrahim Badamasi Babangida aliwahi kusema akiwa ziarani hapa Tanzania kuwa "it is easy to rule Tanzania than to ride a herd of cattle", wakati ule tuliona kejeli, lakini ni ukweli sasa tunauona. Ujinga huu ungetokea Lagos au Abuja sidhani kama "TANESCO" wa kule wangechekewa kama hapa.
Hivi kuna mgao? maana mie naishi karibu na baraza la maaskofu kurasini umeme upo 24/7
Hivi kuna mgao? maana mie naishi karibu na baraza la maaskofu kurasini umeme upo 24/7
:happy: kwa hiyo hata hutembei kujua mambo yanaendaje?
Utakuwa unawaibia umeme toka kwenye majenereta yao
Muda wa kupata umeme na muda wakuwa gizani ukweli ni kwamba muda wa kuwa gizani ni mkubwa kuliko wa kuwa na umeme kwa kweli hali ni ngumu sana tunavumilia ila ukweli safari hii tunashindwa hii ndio kusherehekea mika hamsini ya uhuru fedha za maandalizi bora ziende kwenye vitu vingine tusiadhimishe hali ni mbaya sana
Kuna rafiki yangu anaishi Fire huu mgao wanausikia kwenye vyombo vya habari tu.Hapana mkuu jamaa hawakatiwi umeme kabisa!