Mgao wa Umeme: Tatizo ni UKAME - Kikwete akihojiwa na BBC

My Take.
Japo ni kweli sababu kuu ya mgao huu wa umeme ni ukame, Tanzania would have done better by now kama tatizo lilijulikana tangu 2006, ila pia huu ni wakati kwa sisi Watanzania tuitikie mwito wa rais wetu, " Tupunguze kulalamika tuu, tuje na solutions, serikali ikizikataa ndipo tuibeze kuwa "Tuliwashauri na hamkusikia!"

Pasco

Unajua hii nchi haitaendelea hadi pale watu wote wenye mawazo kama ya kwako watakapokuwa wamekufa!!

Nchi zilizoendelea na zinazoendelea viongozi wake wana wajibika kwa kujiuzulu pale wanaposhindwa kutimiza mahitaji ya jamii wanazoziongoza. Wananchi wanamchagua kiongozi ambaye wanaamini ana uwezo wa kutatua matatizo yao na siyo yule ambaye atawaomba ushauri wa jinsi ya kuyatatua.

Hata kama ni ushauri, raisi tayari ana washauri na wataalam wa kila aina na wanalipwa mishahara kwa kazi hizo, sasa ushauri gani tena anaoutaka kutoka kwa mama yangu kule kijijini? Ndio maana tunafanya uchaguzi na kumkabidhi mtu mmoja mamlaka yote hadi ya kumnyonga mtu tukiamini kuwa ana uwezo wa kutumia raslimali zilizopo pamoja na watu wake ili kuiendeleza nchi.

Anaposhindwa majukumu yake watu wana haki kabisa ya kulalamika na kama yeye ni mtu mstaarabu basi inabidi arekebishe mambo haraka iwezekanavyo au aachie ngazi. Watu biashara zao zinayumba, maofisi ya serkali hakuna ufanisi wa kazi maana wanahitaji umeme ili wa-fax, print, photocoy, watumie computer nk. Nchi inakufa halafu rais anasema nipeni ushauri ili nijue cha kufanya?????!!!!!
Sijawahi kusikia rubani wa ndege ambaye yupo angani na anawaomba abiria wake ushauri pale ndege inapoanza kusua sua.

Tatizo la msingi hapa ni kwamba wananchi hawapewi haki na uhuru wa kuwachagua viongozi wenye uwezo. Tunaongozwa na viongozi wachakachuaji, Hili ni fundisho na changamoto kwa watanzania kama kweli tupo serious na maendeleo ya nchi yetu, tujitahidi kwa kila hali ili chaguzi zijazo ziwe za ukweli na uwazi. Viongozi wawe ni chaguo la wananchi na siyo NEC, usalama wa taifa, wakuu wa mikoa / wilaya au polisi.
 
Mitambo ya kuzalisha umeme na hata second hand iko Ulaya imejaa tele wala si ya kutafuta.Nenda Ujerumani , Poland na Hungary kote huko iko , Holland wala si ya kutafuta ni kuchagua unataka ipi .Hadithi za ajabu sana sana .
 
nilimsikiliza mkulu nikashangaa sana...alijibu maswali kwa jeuri na kiburi cha hali ya juu. Huyu bwana anajiamini nini?

nilikuwa nafikiri kwa cheo chake angejibu kwa busara na logic zaidi. i think he is thinking "what the hell, i have nothing to lose". Hatuna rais wandugu.

Suala la ukame nchi hii nani alikuwa halijui? Kulikuwa na precautions kibao..ila kwa sababu walizozijua wao, hakuna aliyechukua hatua.
 
Rais Jakaya Kikwete, ameuzungumzia mgao wa umeme unaendelea sasa nchini kote, amesisitiza "tatizo ni ukame".

...

Pia Rais Kikwete, ameuhakikishia tena ulimwengu kupitia BBC kuwa serikali yake ni sikivu, kama kuna watyu wenye hoja za msingi kuhusu utatuzi wa tatizo la umeme, wasiishie tuu kulalamika, bali waje na hoja za jinsi ya kutatua tatizo hili na serikali yake itazipokea hoja hizo na kuzifanyia kazi.
Pure arrogance! Does the President imply that we either do something about it or put up with it? Kama yeye na serikali yake hawana suluhisho la utatuzi wa tatizo la umeme, basi akae pembeni awapishe wale wenye suluhisho na asitake kupata majibu ya dezo hapa!
Statement kama hizi kweli Rais si anatafuta kutukanwa!
 
My Take.
Japo ni kweli sababu kuu ya mgao huu wa umeme ni ukame, Tanzania would have done better by now kama tatizo lilijulikana tangu 2006, ila pia huu ni wakati kwa sisi Watanzania tuitikie mwito wa rais wetu, " Tupunguze kulalamika tuu, tuje na solutions, serikali ikizikataa ndipo tuibeze kuwa "Tuliwashauri na hamkusikia!"

Pasco

Pasco
  • Hizo solution zinawakilishwa taasisi gani.?
  • Nipe mfano wa taasiis yeyote ya seriali wewe binafsi uliyowai kuandika maoni kwenye tovuti, kunadika barua au kupiga simu kuomba kuongea na muhisika ukapata resposne ya kueleweka. Response ya kueleweka sio kwamba wakubali bali mtaalam akujibu hiki kitu hakiwezekani sababu ya gharama , hiki hakiwezekani sababu kitachukua muda au hiki hakiwezekani sbabu ya sheria ........ Au hiki ngoja tujaribu kuangalia.
  • Utaratibu wa tenda wa richmond ulichukua muda gani toka kuanza hadi siku mitambo kuwashwa. Kwa nini wasingerudia kufanya utaratibu kama huo na waondoe wanasiasa kuingilia kama ilivyo kwenye utaratibu wa mwanzo.?
  • Je serikali wataalamu UDSM kitego cha electriity wamehsindwa kufanya research na kuja na proposal au wanasiasa wameidharau?
Mimi miaka na nyuma nimekuwa najaribu kupiga simu kutoa maoni kwa simu au tovuti ( Sio kuhusu nishati sababu sio mtaalam) au kulalamika kero fulani kwenye taasisi mbali mbali Hizo tovuti zao wameweka kama fashion tu. Wazitumia kama one way communication. hawategemei wala kutaka kupata repone yeyote. Niambie ni email ya taasisi gani umweai kuandika ikajibiwa. hata kama ni kuwapongeza.

Nimewai kupiga simu na kuongea na mjumbe mmoja kuhusu mapungufu na mapendekezo yangu fulani. kile nilichomwambia akasema wamekizungumia kwenye kikao siku tatu zilizopitana kitafanyiwa kazi soon. Ni zaidi ya mwaka sasa naona hiyo soon ni bado. Hiiz ndio response unazoweza kupata kutoka taasisi za serikali.

Kama JK na watendaji wake wangekuwa Serious wangekuwa wanaona baadhi ya maoni ya wataalamu. Mfano nitashanga kama kuna mtu wa tanesco au nishati anasema hajawai kuona aukusoma comment za mtu ambaye anaonekana ana idea nzuri then wawasiliane nae.. Mfano una member anajii Eng Nsiande. may be akiwa JF anapata nafasi kuelzea ufahamu na aidea zake tofauti na akiwa kazini( nadhani yuko tanesco)
 
mwaka 2005 babayangu alisema maneno haya '' kikwete is the worst president we ever had''juzi nimeenda kumuona huko kijijin kwake akatoa tena kauli hii ''' we have the president who cannot think beyond the next meal''
umesema kweli mkuu!eti hakuna umeme kisa kuna ukame,jee nchi zenye mvua haba miaka yote kama ethiopia hakuna umeme?ina maana pesa za kilimo kwanza zimepotea bure mwaka huu kisa hakuna mvua?
 
Jk hawez kulitatua tatizo la umeme kwani hawezikugeuka kuwa mvua na kunyesha ili ajaze mabwawa tupate umeme
 
nilikuwa namheshimu sana jk kwa jinsi alivyojieleza tanzania hatuna rais.tangu mwaka 2006 mpaka leo anataka kutueleza kuwa hakuna watu wanaoweza kutengeneza mitambo kwa muda mfupi?????.hata kama ni corrupt dk.idrissa sasa tunakukumbuka tupo giza.
Milindi, kama ni kweli, ulikuwa unamheshimu JK lakini kwa jinsi alivyojieleza ndio unasema sasa Tanzania hatuna rais!, this is not right, ukisema hatuna rais, sasa huyu aliyepo ndio nani?.

Hoja yako ni ya msingi, ulikuwa unamuheshimu JK, lakini sasa Tanzania hatuna rais, hii haijatulia. Hapa JF tunabishana kwa hoja, lakini nawaomba wana jf wenzangu, katika kubishana kwetu kwa hoja, tusikalie kubishana tuu, pia tusaidiane, mathalani ukiona mwana jf mwenzako amepost hoja yenye mantiki, lakini akashindwa kuijengea hoja, unamsaidia kama ambavyo mimi najitolea kumsaidia Milindi.

Ndugu yangu Milindi, ungeijenga hoja yako vizuri ili iwe na mashiko zaidi, mathalani ungesema, kama zamani ulikuwa unamuheshimu JK, ungesema heshima hiyo ilitokana na nini?. Nijuavyo mimi, heshima ni kitu cha bure na hutolewa bila vigezo vyovyote, ila yule anayepewa heshima hiyo, akifanya vitendo vya kujivunjia heshima, ndipo hapo unavitaja vitendo hivyo na kusema humuheshimu tena.

Kwa JK kusema tatizo la umeme limesababishwa na ukame, amejivunjia heshima kivipi?.

Pili pia unaweza kusema Tanzania hatuna rais, ila unatakiwa pia kesema huyu aliyepo ni nani sasa?. Katika kujenga hoja, kuna vitu ni facts, huwezi kuvikanusha, kama vile dunia ni duara, its a fact, dunia inazunguka, its a fact etc, vivyo hivyo, rais wa Tanzania ni Jakaya Mrisho Kikwete, this is a fact, sasa uwe ulimchagua, hukumchagua, unamtambua, humtambui, JK ndio rais wa Tanzania, ni rais wa waliomchagua na ni rais wa wasio mchagua, ni rais wa wanaomtambua pia ni rais wa wasio mtambua, akishatangazwa kuwa ni rais, hiyo inakuwa fact, yaani urais ni taasisi ya urais ambayo kwa kipindi hiki, inashikiliwa na JK, ukisema hatuna rais, then Tanzania basi tuna Mfalme, Malkia, Chifu, Mangi, au Mkama etc. Its a fact that Tanzania tuna rais.

Kwa vile urais ni taasisi inayoshikiliwa na mtu, aliyeushika urais huo, ni binadamu aitwaye JK. Huwezi kubeza uwepo wa taasisi ya urais, lakini unaweza kumbeza aliyeishika taasisi hiyo, mathalani unaweza kumbeza rais aliyepo kwa vigezo vyako vyovyote mli mradi ujenge hoja yenye mashiko dhidi ya hoja zako.

Mathalani unaweza kujenga hoja, kuwa JK ni hivi na vile, lakini haiondoa fact kuwa yeye ndiye rais

Tuendelee.

Pasco
 
Mkuu Pasco asante sana!! Maana wengine tulikuwa bado tumejichimbia kwenye haya maofisi ya waajiri wetu, hatukumsikia.

Lakini JK simlaumu, maana upole wetu umemfanya amelala usingizi wa pono!!! Wakati mgao unaanza kushika kasi 2006, tulimsikia huyu akisema serikali yake itaondoa kabisa tatizo la umeme, liwe historia!!!

He should pilot his cabinet to leave the office!!! A failed president...
Mkuu Nyunyu, pale mwaka 2006 rais wetu alipotuambia maneno hayo, kuwa serikali yake itaondoa kabisa tatizo la umeme liwe historia, jee pia alisema ataliondoaje?, na jee aliweka time frame?. Kwa vile kipindi chake ni miaka kumi, kwa wale wenye imani kali kama yangu, bado tunaaminia kuwa kabla hajamaliza miaka yake 10, tatizo la umeme litakuwa ni historia.

Nyunyu, pia kwa vile umekiri Watanzania ni wapole, hata tukidanganywa kama watoto wadogo, unategemea ndio tungefanya nini?. Nakuomba at the moment, usimuite a failed president kwa vile kipimo cha kupasi au kufeli hufanyika kila baada ya miaka mitano, baada ya kuja na zile ahadi za maisha bora kwa kila Mtanzania kwa mwendo ule wa ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya kuelekea hayo maisha bora kwa kila Mtanzania, tulipashisha kwa alama za A, kwa kumpatia zaidi ya asilimia 80. Miaka mitano ya kwanza alimaliza na maisha bora yenyewe ndio haya likiwepo hili giza, lakini ulipofika kipindi cha mtihani pili na wa mwisho, alikuja na ahadi kubwa na nono zaidi, ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi, huoni kuwa sasa ndio tutapaa kabisa kimaendeleo?, si alipasi kwa maksi za daraja C, asilimia 48 na watoaji wa maksi hizo ni sisi Watanzania baada ya kuridhishwa na kazi nzuri aliyotuifanyia. Sasa unawezaje kumuita a failed president huku kipindi cha ahadi zake hakija malizika?.

Nasisitiza, lets be patience, good things are coming before 2015!
 
Tafadhali Pasco!Hatua ni zipi hizo? Na ziko njia gani ambako hakupitiki miaka nenda rudi?Fikiria makali ya umeme 2006 hadi leo yameongezeka kiasi gani? Kila siku juhudi za makusudi zinafanywa na hatuzioni sisi/mimi!Mwanzoni mwa mwaka tuliambiwa mgao ni kwa mwezi wa January tu....leo hii ni July na hali ni mbaya kuliko.Hebu nisaidie na mm niishi kwa matumaini Pasco.
bht, ili uweza kuishi kwa raha, lazima uwe na imani pasipo mashaka kuwa good things are coming no matter when. Kwa hili la umeme, limehubiriwa sana hata katika mkukuta lipo, kwenye mkurabita lipo, kwenye mkumbita lipo, na hata katika huu mpango wa maendeleo wa juzi juzi pia lipo, naomba tuwe na subira kama walivyo nduigu zetu wanaomsubiria masiya wakikesha na kuomba kwa maana hamjui siku atakaporudi,

Nasi tuishi kwa matumaini makubwa, kabla ya 2015 mambo yatakuwa super!.
 
Kwa hio hii mitambo ni customized.., yaani ukitoa order ndio watu wanaingia kiwandani kuanza kutengeneza.., hakuna stock kabisa
Katika mahojiano hayo rais alisisitiza kama ni mitambo tuu bora mitambo, hii ipo tele!, sisi hatutaki bora mitambo, tunataka mitambo bora, na mambo mazuri siku zote, hayataki haraka, tumeshaiagiza na imeshaanza kuwasili. Kama hasira za Watanzania ni hiki ki giza cha leo, basi msiwe na wasiwasi, kabla ya 2015, tutapata mwanga wa milele na tukiwarudisha tena ndio tunaelekea kabisa kwenye nuclear power plant!.
 
Mbona hayo maneno hatwambi raia wake kupitia TBC anakwenda yasemea ughaibuni?
Watu, hili nalo neno!. Kusema ukweli viongozi wetu wa kitaifa wana ulimbukeni wa kupapatikia vyombo vya habari vya nje, na mimi binafsi hili linanisikitisha na kunihuzunisha.

Mimi binafsi ni mwandishi wa kujitegemea, kila nikukutana na rais wetu humu nyumbani katika matukio mbalimbali, hutamani sana kumsogezea kipaza sauti, sio siri siri, licha ya kuzuiwa na watu wake wa usalama, JK mwenyewe ni mtu mwenye dharau, anatudharau sisi waandishi wa nyumbani, lakini akiwa huko safarini, utayasikia mahojiano yake ya man to man.

Ila pia myonge, mnyongeni lakini haki yake mpeni, uhusiano wa JK na waandishi wetu ni bora mara mia kulo Ben na Mwinyi ndio kabisaaa!.

Katika kipindi cha miaka kumi ya Mwinyi, sikuwahi kusikia kama aliwahi kufanya hata press conference moja in person, enzi hizi ilikuwa ni Choks tuu. Alipokuja Ben ni hivyo hivyo lakini Ben alikuwa angalau angalau.

Wakati huo wa Ben, niliwahi kuomba kufanya naye mahojiano nikakataliwa nikiambiwa eti "utamuembarass". Ikatokea wakati fulani nikiwa UN, GA, ndipo Press Sec wake mmoja akaniambia, "We Pasco, si ulitakaga kufanya mahojiano na rais, nafasi sasa ndio imepatikana, tukupangie muda ukamuhoji?, lakini lazima yawe ni mambo ya kuhusu UN-GA, sio siri, nilimkatalia, nikamwambia kwa nini nifanye mahojiano na rais wangu, ughaibuni?, nikamsisitizia, kama kweli ana nia njema nifanye mahojiano na rais wangu, naomba mahojiano hayo nije niyafanyie nyumbani, that did never happen.

Mkapa tulikuwa tunamuona tuu CNN, BBC lakine never on any TV Studio nyumbani! Tena kuna wakati aliadhiriwa na Tim Sebastian wa BBC kwenye Hard Talk, siyo siri, niliyaangalia mahojiano yale, kimoyomoyo nikijisemea hatimaye amekipata alichokokuwa anakitaka kwa kuwa kimbelembele na waandishi wa kizungu!.

Kwa vile najipanga kushika tena jembe kurudia shamba langu la tasnia ya habari, nianze kulima tena, nitafanya atempt nyingine kwa JK na kumsikilizia.
 
Katika mahojiano hayo rais alisisitiza kama ni mitambo tuu bora mitambo, hii ipo tele!, sisi hatutaki bora mitambo, tunataka mitambo bora, na mambo mazuri siku zote, hayataki haraka, tumeshaiagiza na imeshaanza kuwasili. Kama hasira za Watanzania ni hiki ki giza cha leo, basi msiwe na wasiwasi, kabla ya 2015, tutapata mwanga wa milele na tukiwarudisha tena ndio tunaelekea kabisa kwenye nuclear power plant!.
duh...wandugu...maneno mengine yanaumiza kweli! kweli bongo unaweza kufa kwa pressure ukiwa serious! wenzetu wachina wamejenga daraja refu kuliko yote duniani kwa miaka minne.....sisi watanzania kuleta mitambo ya umeme iliyokwisha tengenezwa inatuchukua miaka mitano?? unaendaje kwenye uzalishaji wa umeme kwa nguvu za neclear wakati hata huu wa upepo unatushinda??unawaza nuclear power plants wakati hata contingency plans nch hii hakuna... angalia mabomu yenyewe tu yanavyotuzingua!! nachukulia hoja yako hapo juu kama joke tu ...lakini kama uko serious...k.m! ngoja nilale mie kuzaliwa bongo kweli nuksi!
 
Back
Top Bottom