Mgao wa Umeme: Tatizo ni UKAME - Kikwete akihojiwa na BBC

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,443
113,452
Mahojiano na Rais Kikwete yaliyofanywa na Mwandishi wa BBC Bw. Omar Mutasa huko Afrika Kusini ambako Rais Kikwete alikuwa anaendelea na ziara yake ya Kiserikali.

BBC: Suala la Umeme Mheshimiwa Rais Kikwete ungependa kulizungumzia nini?

Rais Kikwete: Tatizo la umeme kimsingi ni suala la ukame tu. Kwa sababu mabwawa yetu ya kuzalisha umeme yanayotoa umeme karibu MW600 sasa hivi yanatoa umeme kidogo sana. Maji pungufu ndio maana kuna tatizo hilo.

BBC:Mheshimiwa, hili suala si la leo wala si la jana limekuwepo kwa muda mrefu, kwanini serikali haina njia mbadala ya kuweza kutatua suala hili? Tanzania ina raslimali nyingi mheshimiwa Kikwete!

Rais Kikwete: Kwanza, serikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe, unajua unajua hivyo, Kwa sababu (kicheko) ingekuwa na uwezo wa kufanya mvua inyeshe mabwawa yale yangejaa. Ni kweli kuwa Tanzania inazo raslimali za kutosha na katika kipindi hiki - toka wakati ule - sisi tulipoingia tumekuta suala la Ukame na mwaka 2007 tukapata matatizo ya kwanza.

Baada ya pale tukafanya uamuzi kwamba sasa tuanze kuwekeza katika vyanzo vingine; tuongeze uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo vingine. Tuongeze uzalishaji wa umeme kutoka vya vya kutumia gesi asilia twende kwenye makaa ya mawe. Kutoka vyanzo vya gesi asilia tayari tuna mtambo pale Ubungo, na toka mwaka 2009 mpaka sasa tumeshaongeza MW145, itakapofika Disemba tutakuwa tumeongeza MW160 nyingine. Tutakuwa tumeongeza MW300 siyo kidogo.

BBC: Mhe. Kikwete Mmoja katika wabunge Bw. John Mnyika ambaye ni Mbunge wa upinzani ambaye ni Waziri Kivuli wa Nishati amekuwa akilalamika na kwamba amewahi kusema kwamba hili tatizo ni tatizo linalowahusu Watanzania wote na amesema mje pamoja na kuona vipi mtakavyotatua tatizo hili. Na sasa hivi Bungeni wamesimamisha mswada, wa kutoa bajeti ya nishati ya Tanzania. Wewe unachukulia vipi matamshi kama haya kutoka kwa Wabunge?

Rais Kikwete: Mimi nasema hivi yeye si Mbunge atoe maarifa yake tu; anayo maarifa gani na anapendekeza kitu gani. Kwa sababu toka Uhuru mabwawa tuliyotengeneza ni Kidatu MW200, Mtera MW80, Kihansi MW 165 mimi nilipokuwa Waziri wa Nishati, pale Pangani tumeongeza.
Sasa ufikirie kwamba toka Uhuru tumeweza kuzalisha umeme wa MW600, lakini toka 2009 mpaka Disemba mwaka huu tutakuwa tumeongeza MW300! Ni jitihada kubwa. Mimi nasema kwamba usipozitambua hizo ni kwamba wewe mwenyewe siyo mkweli.

Sasa ni hivi, unajua hii mitambo ya umeme si mitambo unaenda kununua kama unavyonunua jaketi lako hili. Ni kwamba ukitaka mitambo ya umeme, lazima uweke order wakutengenezee. Huu mtambo unaofika mwaka huu Disemba order tuliweka mwezi wa Juni mwaka jana. Inachukua muda huo kutengeneza. Sasa ingekuwa mnaenda kutafuta mitumba, mitumba ya mitambo tu ya kununua iko mingi kweli. Tukasema hatuwezi kufanya hivyo.

Mimi nasema hivi, kitu kikubwa ni kuwa na subira. Tumefanya jitihada kubwa. Ni lazima watu watambue kuwa tumefanya jitihada kubwa katika miaka hii toka 2009 mpaka sasa hivi 2011 Disemba tutakuwa tumeongeza MW300 kulinganisha na MW600 ambazo tumeziongeza katika miaka yote hii. Nasema ni lazima watu watambue hivi. Sasa kama kuna mtu ana maarifa ya haraka zaidi nasema mtu atoe maarifa hayo na sisi kama yapo tutayafanyia kazi.

BBC: Kuna njia kama umeme wa jua, umeme wa kutokea ardhini wa mvuke, kwanini serikali haitafuti njia mbadala kuzalisha umeme kwa njia hizo?

Rais Kikwete: Nasema hivi, hata umeme wa jua lazima ujenge, umeme wa mvuke lazima ujenge, si kitu cha mwezi mmoja. Nasema huo ndio ukweli wenyewe na wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - "unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo" - tungeweza kufanya hivyo.

Sisi sasa hivi kwa mfano tunajiandaa kuzalisha umeme wa kutumia Upepo, pale Singida. Tuna mwaka wa tatu sasa tuna mipango na Wakorea wa Kusini, umeme haujakuwepo. Kwa hiyo nasema hayo ni maelezo rahisi. Wanasema "mbona jua lipo?" katengeneze umeme wa jua kama jua lipo! (kicheko).

BBC: Watanzania wamekuwa wakisema (mwisho kabisa) kwamba Tanesco ingebinafsishwa ili waweze kupata makampuni kufanya kazi hiyo ya umeme?

Rais Kikwete: Aah! Kwani ukitaifisha kesho ndio utapata mitambo kesho? Nasema hivi ni vizuri kuelewa tu - kwanza tatizo la msingi - ni maji kukauka kwenye mabwawa. Maji yasingekauka kwenye mabwawa tatizo hili halipo. Maji yamekauka kwenye mabwawa kwa sababu ya ukame. Hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzuia ukame usiwepo. Sasa hiki ndicho kiini cha tatizo. Sasa nasema sisi jitihada ambayo tumeifanya ni kupunguza sasa kutegemea umeme unaotakana na nguvu ya maji.

Toka mwaka 2009 tumewekeza adi Disemba 2011 tutakuwa tumeongeza MW 310, yenyewe hiyo ni hitihada kubwa, ni vizuri ukaitambua jitihada hiyo. Kulikoni kusema kitu tu nasema hatakam huna majawabu rahisi utuambie tu.

MWISHO.

Rais Jakaya Kikwete, ameuzungumzia mgao wa umeme unaendelea sasa nchini kote, amesisitiza "tatizo ni ukame".

Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye mahojiano maalum na BBC akiwa nchini Afrika Kusini yaliyorushwa jioni hii na BBC Swahili.

Rais amesisitiza, kwa vile mitambo yetu mingi inategemea nguvu za maji, hivyo tatizo la umeme limesababishwa na ukame.

Mwandishi akahoji kuwa tangu 2006 mgawo ulipoanza, bado tuu mlikuwa mkitegemea mvua ili hali Tanzania ina rasilimali nyingi?.

Rais alijibu kuwa "kwanza serikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe" ingekuwa na uwezo wa kufanya mvua inyeshe, mabwawa yale yangejaa". baada ya 2006 hatua mbalimbali zimechukuliwa kuzalisha umeme kwa njia za gesi, makaa ya mawe hata umeme wa nguvu za upepo, lakini miradi hii yote inahitaji muda muafaka wa kuagiza mashine, akasisitiza ununuzi ewa mitambo unachukua muda, "huwezi kununua mitambo ya umeme hivi hivi tuu kama unavyoingia dukani kununua koti lako, mitambo huagizwa kwa kupeleka order kiwandani utengenezewe. hata hii mitambo inayoingizwa nchini hivi sasa, iliaagizwa toka mwaka jana.

Rias Kikwete amewataka wanasiasa wasibeze juhudi za serikali kuwaletea umeme wa uhakika Watanzania.

Pia Rais Kikwete, ameuhakikishia tena ulimwengu kupitia BBC kuwa serikali yake ni sikivu, kama kuna watyu wenye hoja za msingi kuhusu utatuzi wa tatizo la umeme, wasiishie tuu kulalamika, bali waje na hoja za jinsi ya kutatua tatizo hili na serikali yake itazipokea hoja hizo na kuzifanyia kazi.

My Take.
Japo ni kweli sababu kuu ya mgao huu wa umeme ni ukame, Tanzania would have done better by now kama tatizo lilijulikana tangu 2006, ila pia huu ni wakati kwa sisi Watanzania tuitikie mwito wa rais wetu, " Tupunguze kulalamika tuu, tuje na solutions, serikali ikizikataa ndipo tuibeze kuwa "Tuliwashauri na hamkusikia!"

Pasco

Update kwa hisani ya Dark City
 
Rais Jakaya Kikwete, ameuzungumzia mgao wa umeme unaendelea sasa nchini kote, amesisitiza "tatizo ni ukame".

Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye mahojiano maalum na BBC akiwa nchini Afrika Kusini yaliyorushwa jioni hii na BBC Swahili.

Rais amesisitiza, kwa vile mitambo yetu mingi inategemea nguvu za maji, hivyo tatizo la umeme limesababishwa na ukame.

Mwandishi akahoji kuwa tangu 2006 mgawo ulipoanza, bado tuu mlikuwa mkitegemea mvua?.

Rais alijibu kuwa baada ya 2006 hatua mbalimbali zimechukuliwa kuzalisha umeme kwa njia za gesi, makaa ya mawe hata umeme wa nguvu za upepo, lakini miradi hii yote inahitaji muda muafaka wa kuagiza mashine, akasisitiza ununuzi ewa mitambo unachukua muda, "huwezi kununua mitambo ya umeme hivi hivi tuu kama unavyoingia dukani kununua koti lako, mitambo huagizwa kwa kupeleka order kiwandani utengenezewe. hata hii mitambo inayoingizwa nchini hivi sasa, iliaagizwa toka mwaka jana.

Rias Kikwete amewataka wanasiasa wasibeze juhudi za serikali kuwaletea umeme wa uhakika Watanzania.

Kweli Rais tunaye...Hivi mvua zisiponyesha kwa zaidi ya mwaka ndo kusema tutaishi gizani muda wote???

Je kuna ukweli kwamba hakuna Makampuni yenye mitambo kwenye show room zao?

Watanzania wataachaje kubeza wakati wako gizani toka 2006, wakati wajanja wanajitoa mafweza??

Sina hata jina la kumpa mkuu wangu huyu!!
 
Mmmmmm!!! Safari ni ndefu sana, sijui tutafika salama?
Glue, tutafika tuu, maadam tatizo ni ukame, hatimaye mvua zitanyesha na tatizo litakwisha, na hata zisiponyesha, hatua za kudumu za kutotegemea umeme maji, ziko njiani.
 
nilikuwa namheshimu sana jk kwa jinsi alivyojieleza tanzania hatuna rais.tangu mwaka 2006 mpaka leo anataka kutueleza kuwa hakuna watu wanaoweza kutengeneza mitambo kwa muda mfupi?????.hata kama ni corrupt dk.idrissa sasa tunakukumbuka tupo giza.
 
Kweli Rais tunaye...Hivi mvua zisiponyesha kwa zaidi ya mwaka ndo kusema tutaishi gizani muda wote??? Je kuna ukweli kwamba hakuna Makampuni yenye mitambo kwenye show room zao?Watanzania wataachaje kubeza wakati wako gizani toka 2006, wakati wajanja wanajitoa mafweza??Sina hata jina la kumpa mkuu wangu huyu!!
Kaka mkubwa, ya nini uumize kichwa hata kumtafutia jina....mwache tu abaki rais Sina Jina.Eti juhudi za serikali kutupa umeme wa uhakika? Zipi hizo ilhali kila siku hali ni mbaya zaidi ya jana?Hivi kweli serikali inaliona hili? Kuna wakati nahisi hata hawajali tena na wameamua liwalo na liwe!
 
kwahiyo ina maana nchi ina ukame kwa miaka sita sasa eh???

Hivi haoni kwamba anajidhalilisha kwa wanaomsikiliza??? hao waandishi wana dataz kuliko yeye mara mia
 
Mkuu Pasco asante sana!! Maana wengine tulikuwa bado tumejichimbia kwenye haya maofisi ya waajiri wetu, hatukumsikia.

Lakini JK simlaumu, maana upole wetu umemfanya amelala usingizi wa pono!!! Wakati mgao unaanza kushika kasi 2006, tulimsikia huyu akisema serikali yake itaondoa kabisa tatizo la umeme, liwe historia!!!

Namuone huruma JK, maana mwandishi kamuuliza swali zuuri sana; I quote "toka 2006 mlikuwa mnasubiri mvua tu..." end of quote. Jibu lake ni la ajabu sana, "huwezi kununua mitambi kama unavyoenda kununua koti. Hili ni sawa, lakini ina maana zaidi ya miaka mitano majenereta hayawezi kuwa yametengenezwa na kuletwa kwetu!!! Kweeeli.... Hivi, si ukipata jibu kama lake unageuka na kumuacha maana haya ni majibu ambayo hata mtoto wa shule ya chekechea anaweza kataa!!!

He should pilot his cabinet to leave the office!!! A failed president...
 
Acha tu mdogo wangu....Kuna wakati unajaribu kutegeneza picha ya mtu unaishia kuona nyota nyota....Huyu JK anayemjua ni Mungu wake peke yake!!

Ngoja niinigie kijijini nikapambane na giza la kulazimisha!
 
Glue, tutafika tuu, maadam tatizo ni ukame, hatimaye mvua zitanyesha na tatizo litakwisha, na hata zisiponyesha, hatua za kudumu za kutotegemea umeme maji, ziko njiani.
Tafadhali Pasco!Hatua ni zipi hizo? Na ziko njia gani ambako hakupitiki miaka nenda rudi?Fikiria makali ya umeme 2006 hadi leo yameongezeka kiasi gani? Kila siku juhudi za makusudi zinafanywa na hatuzioni sisi/mimi!Mwanzoni mwa mwaka tuliambiwa mgao ni kwa mwezi wa January tu....leo hii ni July na hali ni mbaya kuliko.Hebu nisaidie na mm niishi kwa matumaini Pasco.
 
kwahiyo ina maana nchi ina ukame kwa miaka sita sasa eh???

Hivi haoni kwamba anajidhalilisha kwa wanaomsikiliza??? hao waandishi wana dataz kuliko yeye mara mia

Siyo sita tu..Utaenda hadi 2015 na zaidi..

Labda King maker atuonee huruma!
 
Mkuu Pasco asante sana!! Maana wengine tulikuwa bado tumejichimbia kwenye haya maofisi ya waajiri wetu, hatukumsikia.

Lakini JK simlaumu, maana upole wetu umemfanya amelala usingizi wa pono!!! Wakati mgao unaanza kushika kasi 2006, tulimsikia huyu akisema serikali yake itaondoa kabisa tatizo la umeme, liwe historia!!!

Namuone huruma JK, maana mwandishi kamuuliza swali zuuri sana; I quote "toka 2006 mlikuwa mnasubiri mvua tu..." end of quote. Jibu lake ni la ajabu sana, "huwezi kununua mitambi kama unavyoenda kununua koti. Hili ni sawa, lakini ina maana zaidi ya miaka mitano majenereta hayawezi kuwa yametengenezwa na kuletwa kwetu!!! Kweeeli.... Hivi, si ukipata jibu kama lake unageuka na kumuacha maana haya ni majibu ambayo hata mtoto wa shule ya chekechea anaweza kataa!!!

He should pilot his cabinet to leave the office!!! A failed president...
JK sio mple, alijiingiza kwenye tafrija akasahau kuwa yeye ni mlinzi, sasa wameiba hadi vitasa unadhani atasema nini?
 
Acha tu mdogo wangu....Kuna wakati unajaribu kutegeneza picha ya mtu unaishia kuona nyota nyota....Huyu JK anayemjua ni Mungu wake peke yake!!Ngoja niinigie kijijini nikapambane na giza la kulazimisha!
Afu wamepandisha bei ya mafuta ya taa, hata huko kijini utakuta koroboi haziwaki!Hili linchi, kila kukicha najiskia hasira zaidi ya jana.
 
mitambo huagizwa kwa kupeleka order kiwandani utengenezewe. hata hii mitambo inayoingizwa nchini hivi sasa, iliaagizwa toka mwaka jana.

Rias Kikwete amewataka wanasiasa wasibeze juhudi za serikali kuwaletea umeme wa uhakika Watanzania.

Kwa hio hii mitambo ni customized.., yaani ukitoa order ndio watu wanaingia kiwandani kuanza kutengeneza.., hakuna stock kabisa
 
Afu wamepandisha bei ya mafuta ya taa, hata huko kijini utakuta koroboi haziwaki!Hili linchi, kila kukicha najiskia hasira zaidi ya jana.

Hiviiii...hatuwezi kulipiga mnada ili mtu akimbie na mgawo wake?

Naona ujinga wetu utatufikisha mahali tukute akina RA na washirika wao (wakiwemo akina Ngeleja) wameshamaliza mapaja na kila sehemu yenye nyama ya kuku, na kutuachia miguu tu. Tutamlaum nani?

Kwa nini kila mtu asiondoke na kipande chake sasa??
 
mwaka 2005 babayangu alisema maneno haya '' kikwete is the worst president we ever had''

juzi nimeenda kumuona huko kijijin kwake akatoa tena kauli hii ''' we have the president who cannot think beyond the next meal''

Kwa hio hii mitambo ni customized.., yaani ukitoa order ndio watu wanaingia kiwandani kuanza kutengeneza.., hakuna stock kabisa

VoR hata iwe customized vipi, 5 good years is more than normal delivery time!!! I am telling you, JK huwa anajibu maswali tu ili auze sura yake basi... hili si jibu la rais makini!!! Kwanza nahisi alimuona mwandishi wa BBC kama nampotezea muda wake wa kuwahi birthday na shopping!!!

Shame on us wa-TZ, kama ulimpa kura JK basi juta, funga na fanya malipizi usamehewe na Mungu wako!! Maana na uhakika ni ngumu kwa mTZ yeyote kukusamehe!!!

JK na serikali yake ni janga la kitaifa...
 
JK sio mple, alijiingiza kwenye tafrija akasahau kuwa yeye ni mlinzi, sasa wameiba hadi vitasa unadhani atasema nini?
Sikutaka kucheka maana nina hasira hapa na hili giza...basi tu!Yaani majibu yake tu mi ndo huwa nachoka mara dufu! Eti mitambo haininuliwi kama koti.... Nani alisema inaninuliwa kama koti! Sasa ndo upate picha huyo ndo rais sasa!Acha tuteketee na chaguo letu toka kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom