Mgao wa Umeme: Tatizo ni UKAME - Kikwete akihojiwa na BBC

Alishasema umasikini uliopo nchini hajui hata sababu za kuwa masikini hazijui! Ni mchumi wa shahada hapo mlimani kikubwa ni mjeshi taaluma ambayo huitaji kuumiza kichwa zaidi ya kutekeleza tu lakini bado ameshindwa kutambua. Hitler hakuwa na shahada yoyote lakini ujerumani ilinawiri sana kipindi chake achilia mbali mauaji ya wayahudi ndiyo yanyomchafua. Lakini alijua wajibu wake kwa wajerumani.
 
Kweli Rais tunaye...Hivi mvua zisiponyesha kwa zaidi ya mwaka ndo kusema tutaishi gizani muda wote???

Je kuna ukweli kwamba hakuna Makampuni yenye mitambo kwenye show room zao?

Watanzania wataachaje kubeza wakati wako gizani toka 2006, wakati wajanja wanajitoa mafweza??

Sina hata jina la kumpa mkuu wangu huyu!!
Safi saana mkuu hapa umekuwa mungwana..
 
Kwa hio hii mitambo ni customized.., yaani ukitoa order ndio watu wanaingia kiwandani kuanza kutengeneza.., hakuna stock kabisa

customized ndo hiyo iliyokoo show room yaani ilishatenegenezwa...mitambo anayosemea jk ni personalized
 
VoR hata iwe customized vipi, 5 good years is more than normal delivery time!!! I am telling you, JK huwa anajibu maswali tu ili auze sura yake basi... hili si jibu la rais makini!!! Kwanza nahisi alimuona mwandishi wa BBC kama nampotezea muda wake wa kuwahi birthday na shopping!!!

Shame on us wa-TZ, kama ulimpa kura JK basi juta, funga na fanya malipizi usamehewe na Mungu wako!! Maana na uhakika ni ngumu kwa mTZ yeyote kukusamehe!!!

JK na serikali yake ni janga la kitaifa...

Laiti watanzania wangelijua hili hata kama tumechelewa!
 
customized ndo hiyo iliyokoo show room yaani ilishatenegenezwa...mitambo anayosemea jk ni personalized

Safi sana mkuu,

Hivi mtu ambaye alisoma chuo kikuu halafu akaonesha uwezo mdogo sana baada ya kuhitimu (abuse of intellectual ability and qualifications), haweze kunyang'anywa digree aliyopewa wakati anahitimu?
 
Hiviiii...hatuwezi kulipiga mnada ili mtu akimbie na mgawo wake? Naona ujinga wetu utatufikisha mahali tukute akina RA na washirika wao (wakiwemo akina Ngeleja) wameshamaliza mapaja na kila sehemu yenye nyama ya kuku, na kutuachia miguu tu. Tutamlaum nani?Kwa nini kila mtu asiondoke na kipande chake sasa??
Huu ujinga umetugharimu na bado utatugharimu saaana. Mi naona wamgeuwasha uishe basi tujue hakuna tu umeme. Karaha tupu. Mpaka wakati mwingine naona madhara ya huu mgao wenzetu sijui hawayapati ? Aah, hatari !
 
hivi haiwezekani kumchangia huyu jamaa walau kila mtanzania shilingi mia mbili kisha tumpatie aende zake akaishi anakopenda, atuachie nchi yetu tuifumue na kuijenga upya kabisa. kwa kweli naanza kupoteza ujasiri wa kujitambulisha kwamba mimi ni mtz
 
Tatizo sio maji wala nini...tatizo ni rushwa iliyokuwa ikitolewa katika kuwarubuni wabunge wapitishe mikataba hewa, mitambo mibovu, ya Richmond nk. Sasa ndo tumejua kuwa badget ya wizara ya nishati na madini huwa wanawapa rushwa wabunge inapita tu... Matokeo yake ndo haya tunayaona sasa.
 
Huu ujinga umetugharimu na bado utatugharimu saaana. Mi naona wamgeuwasha uishe basi tujue hakuna tu umeme. Karaha tupu. Mpaka wakati mwingine naona madhara ya huu mgao wenzetu sijui hawayapati ? Aah, hatari !

Ndugu yango hao ni wajanja..Wanajitengenezea immunity kwa sababu wanajua mapema kama vile wamepewa taarifa za utabiri wa hali ya hewa...Baada ya hapo wanajinunulia majereta ya kutosha na mengine tuuzia ili tuwalipie gharama zao...

Nadhani haku kampuni inayowatendea dhambi kuu watanzania kama Tanesco...Naamini kila dhambi iko pale!
 
Safi sana mkuu,

Hivi mtu ambaye alisoma chuo kikuu halafu akaonesha uwezo mdogo sana baada ya kuhitimu (abuse of intellectual ability and qualifications), haweze kunyang'anywa digree aliyopewa wakati anahitimu?
Hamna kitu kinachoitwa personalized,customized is the right word meaning to fit customer's specifications.
Mnatia aibu jama,duh!
 
Rais Jakaya Kikwete, ameuzungumzia mgao wa umeme unaendelea sasa nchini kote, amesisitiza "tatizo ni ukame".Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye mahojiano maalum na BBC akiwa nchini Afrika Kusini yaliyorushwa jioni hii na BBC Swahili.Rais amesisitiza, kwa vile mitambo yetu mingi inategemea nguvu za maji, hivyo tatizo la umeme limesababishwa na ukame.Mwandishi akahoji kuwa tangu 2006 mgawo ulipoanza, bado tuu mlikuwa mkitegemea mvua?.Rais alijibu kuwa baada ya 2006 hatua mbalimbali zimechukuliwa kuzalisha umeme kwa njia za gesi, makaa ya mawe hata umeme wa nguvu za upepo, lakini miradi hii yote inahitaji muda muafaka wa kuagiza mashine, akasisitiza ununuzi ewa mitambo unachukua muda, "huwezi kununua mitambo ya umeme hivi hivi tuu kama unavyoingia dukani kununua koti lako, mitambo huagizwa kwa kupeleka order kiwandani utengenezewe. hata hii mitambo inayoingizwa nchini hivi sasa, iliaagizwa toka mwaka jana.Rias Kikwete amewataka wanasiasa wasibeze juhudi za serikali kuwaletea umeme wa uhakika Watanzania. Pia Rais Kikwete, ameuhakikishia tena ulimwengu kupitia BBC kuwa serikali yake ni sikivu, kama kuna watyu wenye hoja za msingi kuhusu utatuzi wa tatizo la umeme, wasiishie tuu kulalamika, bali waje na hoja za jinsi ya kutatua tatizo hili na serikali yake itazipokea hoja hizo na kuzifanyia kazi.My Take.Japo ni kweli sababu kuu ya mgao huu wa umeme ni ukame, Tanzania would have done better by now kama tatizo lilijulikana tangu 2006, ila pia huu ni wakati kwa sisi Watanzania tuitikie mwito wa rais wetu, " Tupunguze kulalamika tuu, tuje na solutions, serikali ikizikataa ndipo tuibeze kuwa "Tuliwashauri na hamkusikia!"Pasco
Mbona hayo maneno hatwambi raia wake kupitia TBC anakwenda yasemea ughaibuni?
 
Kweli Rais tunaye...Hivi mvua zisiponyesha kwa zaidi ya mwaka ndo kusema tutaishi gizani muda wote???

Je kuna ukweli kwamba hakuna Makampuni yenye mitambo kwenye show room zao?

Watanzania wataachaje kubeza wakati wako gizani toka 2006, wakati wajanja wanajitoa mafweza??

Sina hata jina la kumpa mkuu wangu huyu!!

Dark City, anachokisema rais ndicho alichoambiwa na hao washauri wake, sasa kama mashine zipo show room, tupeleke details zikanunuliwe sasa hivi only zisiwe za mitumba!.

Huna haja ya kumpa jina lolote JK, jina lake si ni Jakaya Kikwete, rais wa Tanzania?, jina jingine la nini?.
 
Kweli Rais tunaye...Hivi mvua zisiponyesha kwa zaidi ya mwaka ndo kusema tutaishi gizani muda wote??? Je kuna ukweli kwamba hakuna Makampuni yenye mitambo kwenye show room zao?Watanzania wataachaje kubeza wakati wako gizani toka 2006, wakati wajanja wanajitoa mafweza??Sina hata jina la kumpa mkuu wangu huyu!!
Mwite KILAZA au ZERO
 
Dark City, anachokisema rais ndicho alichoambiwa na hao washauri wake, sasa kama mashine zipo show room, tupeleke details zikanunuliwe sasa hivi only zisiwe za mitumba!.

Huna haja ya kumpa jina lolote JK, jina lake si ni Jakaya Kikwete, rais wa Tanzania?, jina jingine la nini?.

Hivi hujui kuwa Baba akisema au kufanya kitu ambacho kiko nje ya upeo wa mategemeo yako unahisi kujificha uvunguni mwa meza?

Sasa ikitokea kama hivyo ni kosa kubaki bila fikra kichwani kama ilivyonitokea mimi?
 
Laiti watanzania wangelijua hili hata kama tumechelewa!

Dark City, tatizo kubwa liko kwa majority ya watu wetu!!! Root problem ni watu kutotambua kuwa JK na chama chake ndiyo kiini cha majanga yote tunayoyapata!! Wewe fikiria, hivi kweli JK hana watu wanam-coach kujibu maswali akiwa ughaibuni!! Yaani aides wanaoona mbali, na kutambua kwa yeye kuwa nje issues atakazotegemea kuulizwa zipo wazi tu, and so kumtengenezea majibu yenye hadhi ya ki-rais!!!

JK akiwa nje majibu yoooooote huwa ni bomu tu....yaani hili nalo aliona ni jibu kweli!!! (Let's just leave the context and the reallity ya matatizo yetu, tuone PR yake tu...) ni disaster!!!!

Kakobe, Mwingira, Lwakatare, hamasisheni waumini wafunge na kuomba, huyu rais ni janga!!! Maana hakuna njia nyingine kwa status ya watu wetu.
 
Mbona hayo maneno hatwambi raia wake kupitia TBC anakwenda yasemea ughaibuni?
Anaogopa mngempiga mayai viza!baba mtembezi kama alifagiliwa chelewa miguuni alipokuwa mdogo!
 
Dark City, tatizo kubwa liko kwa majority ya watu wetu!!! Root problem ni watu kutotambua kuwa JK na chama chake ndiyo kiini cha majanga yote tunayoyapata!! Wewe fikiria, hivi kweli JK hana watu wanam-coach kujibu maswali akiwa ughaibuni!! Yaani aides wanaoona mbali, na kutambua kwa yeye kuwa nje issues atakazotegemea kuulizwa zipo wazi tu, and so kumtengenezea majibu yenye hadhi ya ki-rais!!!

JK akiwa nje majibu yoooooote huwa ni bomu tu....yaani hili nalo aliona ni jibu kweli!!! (Let's just leave the context and the reallity ya matatizo yetu, tuone PR yake tu...) ni disaster!!!!

Kakobe, Mwingira, Lwakatare, hamasisheni waumini wafunge na kuomba, huyu rais ni janga!!! Maana hakuna njia nyingine kwa status ya watu wetu.

Sawa mkuu,

Hivi ukiwa Rais wa nchi unaacha kutumia akili ya kuzaliwa (sijui ndiyo mnaita common sense) mpaka upikiwe majibu????
 
Back
Top Bottom