Mganga wa kienyeji Mbaroni akidaiwa kubaka mgonjwa wake

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1677305870408.png

JF SUMMARY

Jeshi la Polisi linamshikilia Sabihi Mpando, Mkazi wa Chipuputa kwa tuhuma za kumfanyia Ukatili wa Kingono Mgonjwa mwenye mwenye miaka 17 aliyekuwa akimtibu wakiwa Makaburini.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Hamis Ramadhani, amesema, Mganga alimlaghai mwathirika na kwenda naye eneo la Makaburi, wakiwa hapo alimwingilia kimwili kinguvu huku akidai anampa Matibabu.

Mtuhumiwa yuko Mahabusu kwaajili ya Mahojiano zaidi ambapo Upelelezi ukikamilka atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

==============

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara likimshikilia mtu mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 17 aliyekuwa akimtibu katika makaburi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 24, 2023, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Hamis Ramadhani amesema mtuhumiwa alifanya kitendo hicho katika eneo la Mingano Makaburini na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

Amesema kuwa mnamo Februari 23, 2023 nyakati za usiku, Sabihi Mpando miaka (41) ambaye ni mganga wa kienyeji na mkazi wa Chipuputa alimbaka binti huyo.

“Tukio hilo lilitokea wakiwa katika makaburi ya Mingano na mbinu iliyotumika ni kumlagai mwathiriwa na kwenda naye maeneo ya Makaburi kwa ajili ya kumpa matibabu, kisha kumwingilia kimwili huku akimweleza kuwa ni tiba,” amesema.

Amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa na yupo mahabusu kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo, ambapo upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma.

Katika tukio linguine Jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa tukio la mauaji ya mwanamke aliyejulikana kwa jina la Ziada Jafari Kondo (40) mkazi wa Matanki.

“Tukio hili liligundulika mnamo Februari 22 majira ya saa sita usiku huko mtaa wa Wapiwapi “A” Masasi, ambapo alikutwa ameuwawa na watu wasiofahamika wasiofahamika,” amesema.

Amesema uchunguzi wa kitabibu na daktari ulibaini kuwa chanzo cha kifo cha marehemu ni kukosa hewa baada ya kumkaba koo na kunyimwa pumzi.

MWANANCHI
 
Hawa wanawake wanaonda kwa waganga wa kienyeji wenyewe uhadithia wanayokutana nayo huko ikiwemo kutakwa kingono. Wapo wanaokataa kufanyiwa mambo hayo na wengine hukubali. Kuna wale wanaotaka dawa za uzazi, hawa hawana namna ya kukataa maana wakiambiwa wanaingiziwa dawa kwa dushe hukubali tu. Kwa ujumka wanawake waendao kwa waganga wa kienyeji ni chakula cha mganga akimtamani hana ujanja wa kukwepa
 
Tukio hilo lilitokea wakiwa katika makaburi ya Mingano na mbinu iliyotumika ni kumlagai mwathiriwa na kwenda naye maeneo ya Makaburi kwa ajili ya kumpa matibabu, kisha kumwingilia kimwili huku akimweleza kuwa ni tiba,” amesema.

NI TIBA YA UGONJWA GANI?
YAWEZEKANA KUMUINGILIA KIMWILI KWA NGUVU NDIO TIBA YENYEWE, KAMA UGONJWA WENYEWE HAUJULIKANI.
MTOTO WA MIAKA 17 KWENDA MAKABURINI, JE WAZAZI WALEZI NDUGU ZAKE HAWAKWENDA NAYE?

SIKU ZINAKUJA, HAWA WANAOSHINDA KUTAFUTA UPAKO NA MIUJIZA NAO WANAKUJA NA SHUHUDA ZAO
 
  • Thanks
Reactions: apk
Dem tako hilo kaenda kwa mganga
Unafikiri mganga ataacha kumla

Ova
 
Kwa mganga wa kienyeji, si jambo jipya ni muendelezo tu, dawa ni pale watakapoacha kujazana kwa waganga kwa kila jambo linalowafikwa.
 
Kama mtu anataka mganga wa uhakika mganga wa Tanga aje pm ilaa aandae kunitumia 5000 Kwa akili ya connection.


Alisikika m Tanzania mmoja akisema Vibora vinagharama Quality is Expensive kama hutaki unataka cheap chukua ya kwenye nguzo utapeliwe.


Nikimtapeli mtu anireport nipigie life ban

Karibuni PM/DM
 
Back
Top Bottom