Mganga asakwa kwa tuhuma za kumbaka, kumpa mimba mwanafunzi wa Shule ya Msingi

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi linamtafuta Juma Salumu maarufu ‘Juma Kipanya’ ambaye ni mganga wa kienyeji mkazi wa Manispaa ya Lindi kwa tuhuma za kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 15 Wilayani Lindi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Foka Dinya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa mama mzazi wa mtoto huyo aligundua mtoto wake kuwa mjamzito mwezi Disemba 2021 akatoa taarifa Polisi Februari 3, 2022 ambapo tayari Mganga huyo alikuwa ametoroka kusipojulikana.

Kwa upande wake Mama Mzazi wa Mtoto huyo amesema mwezi wa sita mwaka jana mtoto wake alipelekwa kwa mganga huyo na babu yake kwa madai ya kwenda kutengeneza dawa baada ya mganga kutoa sharti la dawa yake ni lazima itengenezwe na binti kigoli (asiyezaa wala kushiriki tendo la ndoa) na alipopelekwa binti huyo alimbaka kisha kumtishia asiseme kwa watu, kwani akisema mizimu itampa adhabu.

Mama huyo amesema binti yake aliporudi nyumbani hakusema chochote na aliendelea na masomo yake mpaka ilipofika Decemba 2021 ambapo waligundua hali isiyokuwa ya kawaida na walipombana akaeleza kwamba alibakwa na mganga Juma Salum alipokwenda kutengeneza dawa ya babu yake.
Source: Swahili Times
 
Mganga wa Kienyeji, Juma Salumu mkazi wa Lindi anatafutwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba (15).

Tukio hilo lilitendeka Juni 2021 baada ya mganga kutoa sharti kwa babu wa mwanafunzi apeleke binti kigoli ili kutengeneza dawa.


Source: Swahili Times
Mganga wa kizazi cha nyoka
 
15years darasa la saba!!!
Kipanya wangemuacha tu,

hii nchi inabidi iangalie namna gani katiba na sheria za nchi zinafanyiwa maboresho
 
Back
Top Bottom