Huu ndio muonekano wa Hospitali ya Uhuru iliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma , Ujenzi wa hospitali ya Uhuru umegharimu kiasi cha Shilingi Billioni 3.9 (Milioni 3900).
Ujenzi wa hospital ya uhuru ni agizo la aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alilolitoa kwa kusema fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania bara za Disemba 9, 2018 zitumike kujenga hospitali hiyo.
NOTE: Kama kila Kiongozi wa nchi hii angeokoa Fedha zinazoelekezwa kwenye MATUMBO ya Viongozi kwa mwavuli wa sherehe za kitaifa za Uhuru, Muungano na Mapinduzi Tanzania ingekuwa na hospitali kama hizi au zaidi ya hii si chini ya 100, tungekuwa na shule za kisasa za Kata, tungekuwa na viwanda vingi vya kuchakata mazao n.k.
Mgala muueni haki yake mpeni. Uongozi ni maono na moja ya eneo ambalo Magufuli alikuwa na maono chanya ilikuwa ni pamoja na eneo hili la sherehe za Uhuru na Muungano. Alidhubutu kupunguza gharama za sherehe hizo kwa asilimia kubwa. Hukuishia tu katika kupunguza gharama bali akaenda mbali katika kusherehekea sherehe hizo kwa njia ya tofauti kama kutumia fedha hizo kwa ajili ya miundombinu ya madaraja, barabara na hospitali. Hili kwangu naona ni bora sana.
Kuliko kuwakusanya Viongozi nchi nzima na kulipana mabilioni ya posho ni bora kutumia mabilioni hayo kuweka alama itakayodumu na kunufaisha Watanzania wengi kuliko kunufaisha MATUMBO ya wachache.
Hapa hata Mtanzania akiingia kutibiwa ukamwambia karibu matunda ya UHURU anakuelewa. Sherehe hazimsaidii Mwananchi wa kawaida bali huwanufaisha Viongozi na familia zao.
Hakika baniani mbaya lakini kiatu chake dawa.
Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti