PreGE2025 Mfupa uliomshinda Magu, Heche na CHADEMA wanauweza.

PreGE2025 Mfupa uliomshinda Magu, Heche na CHADEMA wanauweza.

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hello!

Magu na uzalendo na upendo wake kwa wananchi maskini alishindwa kupiga marufuku kamari ambayo kwa jicho la haraka ni Kodi kidogo inaingia serikalini, lakini inaleta hasara kubwa kwa kuwafanya vijana wengi kutofanya kazi wakiamini betting ni mojawapo ya kazi. Pesa nyingi inaenda nje yaliko anzishwa makampuni haya ya kubeti, wananchi wakiachiwa utumwa na umaskini,

Unakuta boda boda anashinda na kukesha akikwepana na maroli barabarani, akipata 20,000, anapekeka 10,000 kubeti na analiwa zote, pata picha, kwa mwaka anapoteza kiasi gani na nchi inapata hasara kiasi gani kwa 80%ya mapato ya betting yanayoingia kwenye nchi za nje kupitia betting 🤔

Sasa watumishi hawa wa Mungu John Heche na CHADEMA wameliona Hilo na kuliweka wazi mapema kabisa bila kuhofia kupoteza kura fake za wacheza kamari na wamiliki wa michezo hiyo ya kubahatisha akina Mwigu.

NB: Truth shall set you free.

Mungu ibariki CHADEMA

Mungu Mbariki John Heche.

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania.

Karibu ni🙏
Mchezo wa kubeti na mikopo kausha damu inadumaza akili ya kubuni mbinu endelevu za kujiingizia kipato
 
Mchezo wa kubeti na mikopo kausha damu inadumaza akili ya kubuni mbinu endelevu za kujiingizia kipato
Halafu kuna mdau anataka CHADEMA ipoteze muda kuelimisha watu waache kubeti,

Huko ni kupoteza muda.

Ni kuwafutia vibali kampuni za betting, wabakie wa kamari vichochoroni ambao polisi watamalizana nao.
 
Kuelimisha watu kuacha kubeti ni kupoteza muda,
Kamari haijawahi kuwa Banned kila sehemu ndio maana kuna Casino na mpaka kuna sehemu ambazo ni kamari mwanzo mwisho.., kwahio badala ya watu kuaminishwa tatu mzuka na kwamba unaweza ukashinda matrilioni kuwepo pia na upande wa pili wa Media ambazo zipo kwa ajili ya UMMA kama TBC n.k. kuelimisha watu kwamba hakuna mtu anayeshinda kamari in the long run zaidi ya mchezeshaji (The HOUSE)
Mbona zamani wacheza kamari walikuwa wakimwona askari wanakimbia wenyewe?
Walikuwa wanakimbia kwenye Casino au kitaa ambapo ilikuwa kosa kisheria (karata tatu n.k.) na kwamba hao wachezeshaji hawana vibali ?

Kwahio utaona kwamba sheria inapindishwa sasa hivi na Kamari imekuwa so out there hata kuweza kufikiwa kwa urahisi na ni vigumu kuzuia labda through elimu ya madhara yake..., pia ni sheria ndio inaweza kuzuia matangazo hususan matangazo ambayo ni ya uongo kuaminisha watu kwamba watapata bila kuonyesha effects zao.., after all takwambia hata hizi speculations za Stock Markets na kutokana na insider trading zote ni Kamari tu....
Kuhalalisha betting/ kamari ni UOVU mkuu.
Huwezi ukapinga / kuzuia betting moja kwa moja mtu anapunter pesa ndogo kwamba timu yake itashinda au kushindwa (for leisure) LAKINI ni vigumu kuzuia huyu mtu kutumbukia kwenye addiction unless kumuelezea madhara yake mara kwa mara (hii ndio njia)

By the way umesema huwezi kuhalalisha Kamari ni Uovu sasa hao uliowataja wana mandate gani au uwezo gani wa kuzuia hio.., kumbuka hata hii kitu ikiwa illegal ( kama ilivyokuwa USA enzi za kuzuia Pombe na Kamari) ndio hapo palitokea rise of Mafioso waliokuwa wanafanya underground bookies na bootlegging
 
Kweli Chawa hana Gamba wala Gwanda... Yaani ishakuwa pande zote ni mwendo wa propaganda na kuvishana vilemba vya ukoka badala ya kujikita kwenye Hoja..., Case in point badala ya hapa kuongelea athari za addiction tunaongelea nadharia za hawa watu kumaliza hii issue !!???

Wanamaliza vipi ? kwamba ni kama switch ya kuzima na kuwasha ? AU...
  • Kutumia elimu na kuelewesha watu athari, (Hili linaweza kufanywa vema na Wasanii)
  • Kutumia sheria kupinga utangazaji na promotion ya kamari (Serikali na Watunga Sera)
  • Kuhakikisha watu wana ujira wa kutosha na kuacha kufukuzana na illusion ili huu mwaka uwe wao... Na hili ni la kitamaduni zaidi sababu jamii ya sasa inataka quick results
By the way kuongelea mtu mmoja kumaliza betting na addictions ndio yaleyale ya kudhani mtu mmoja anaweza kuleta mabadiliko zaidi ya ushirikishwaji wa watu husika...
Kiongozi usiwachukulie serious chadema hata siku Moja, wao, wakiongozwa na tamaa yao ya madaraka pamoja na chuki kwa Samia, wanaweza kuropoka lolote lile Ili mradi tu wawachote akili wasiokuwa na fikra sawasawa.
 
Tukianza kuwagawa watu katika makundi tunakosea, kwahio tuendelee kupinga na kukataa lolote ambalo halipo sawa no matter linatoka pande zipi..., sababu tukiongelea status quo, ndio hii matangazo ya Kamari hadi wakati wa taarifa ya habari wala yasiojali muda ambao watoto wanasikiliza (hii ni mbaya sababu ni recruitment hata kwa wale ambao hawajaingia kwenye addiction) Kwahio ingawa sipendi a Police state ya kuwapangia watu hata kwenda Casino (ingawa naweza kuwapa onyo) lakini sio busara kuachia watu wafanye recruitment tena kwa kuongea uongo.., Na Serikali kufanya hiki kama kipato sababu kila masikini huyu anavyopoteza wenyewe wanavuna pesa ambazo sio kwamba zinawekwa kwenye kutatua hili tatizo bali sijui zinakwenda God know where...
 
Wazee wa betting mmeambiwa kweli chungu.

Ni kumeza tu hakuna namna.
Tatizi kubwa vigogo wa ccm wabafaidi betting wanafumbia macho hasara hii.

1. Hakuna nchi imeendelea kwa kubet
2. Pesa nyingi zinasepa nje na kuharibu mzunguko wa oesa nchini
 
Tatizi kubwa vigogo wa ccm wabafaidi betting wanafumbia macho hasara hii.

1. Hakuna nchi imeendelea kwa kubet
2. Pesa nyingi zinasepa nje na kuharibu mzunguko wa oesa nchini
Uchumi wa kubahatisha!
 
Halafu kuna mdau anataka CHADEMA ipoteze muda kuelimisha watu waache kubeti,

Huko ni kupoteza muda.

Ni kuwafutia vibali kampuni za betting, wabakie wa kamari vichochoroni ambao polisi watamalizana nao.
Akili za ki CCM, mchezo wa kubeti ulisababisha hizo sarafu zipotee pia kwenye sarafu wajajanja wamepiga Hela za kutosha
 
Siku ikitokea Chadema imekufa mtajuta!
Ni sawa na kifo cha Yanga au Simba!
 
Wachina na madubwi yao wameondoa mzungukoni sarafu za mia mbili 😡
 
Kuamini kutoboa maisha kwa betting ni uwendawazimu.
Ni kuamua kuwa maskini, maisha hayabetiwi
 
Mapeema, serikali ya ccm imeiga na kuanza kupiga pin betting.
 
Hello!

Magu na uzalendo na upendo wake kwa wananchi maskini alishindwa kupiga marufuku kamari ambayo kwa jicho la haraka ni Kodi kidogo inaingia serikalini, lakini inaleta hasara kubwa kwa kuwafanya vijana wengi kutofanya kazi wakiamini betting ni mojawapo ya kazi. Pesa nyingi inaenda nje yaliko anzishwa makampuni haya ya kubeti, wananchi wakiachiwa utumwa na umaskini,

Unakuta boda boda anashinda na kukesha akikwepana na maroli barabarani, akipata 20,000, anapekeka 10,000 kubeti na analiwa zote, pata picha, kwa mwaka anapoteza kiasi gani na nchi inapata hasara kiasi gani kwa 80%ya mapato ya betting yanayoingia kwenye nchi za nje kupitia betting 🤔

Sasa watumishi hawa wa Mungu John Heche na CHADEMA wameliona Hilo na kuliweka wazi mapema kabisa bila kuhofia kupoteza kura fake za wacheza kamari na wamiliki wa michezo hiyo ya kubahatisha akina Mwigu.

NB: Truth shall set you free.

Mungu ibariki CHADEMA

Mungu Mbariki John Heche.

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania.

Karibu ni🙏
Ngoja tuone wataishia wapi
 
Back
Top Bottom