Mfungwa kwenye basi la abiria!!

Clarity

JF-Expert Member
Jul 6, 2010
1,553
1,968
Nasafiri ndani ya basi la ngorika kutoka Moshi kuja Dar Gari la magereza limeleta mfungwa akiwa na maaskari magereza watatu
Swali langu wana JF je ni kawaida kusafirisha mfungwa kwenye public transport tena akiwa amefungwa pingu?
 
Sasa hivi nchi yetu haiko kwenye hali ya kawaida! Kwenye movie hapo ingekuwa arranged ajali afu achukuliwe na makubwa ya maadui! Bongo ndo home wallah!
 
Kiofisi hapo ishaandikwa pesa ndeefu,mafuta ya Gari toka Kilimanjaro mpaka Dar,posho za askari(per diem) kumbe wametumia short cut! hii nchi bwana!
 
Hayo ya kawaida sana Bongo haswa kama anasafrshwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingne.ila swali kubwa la kujiuliza;huyo mfungwa ana tuhuma gani?askari km walibeba bunduki inaweza ku7bisha madhara gani kwa abiria?na kuna uhalali gani kufanya ivyo?
 
Kisheria mfungwa anapokuwa katika public transport hairuhusiwi kumtia pingu kwa kuwa dhamana ya usalama wa abiria wote ina kuwa chini ya dereva-basila abiria,rubani ndege,nahodha meli.boti nk
 
Mkuu Clarity Mshukuru mungu kwa kuwa mlifika salama haikutokea ajali ya kutengeneza ili mahabusu aokolewe. Nadhani kesi yake ilikuwa ni ya kukaba...ingekuwa ni kesi kama ya mauwaji au wizi wa mabilioni wasingempeleka dar kwa Ngorika....defender ingetumika
 
Last edited by a moderator:
Sasa hivi nchi yetu haiko kwenye hali ya kawaida! Kwenye movie hapo ingekuwa arranged ajali afu achukuliwe na makubwa ya maadui! Bongo ndo home wallah!

Hahahaha hapo steringi anakuwa wapi?
 
Tumeona wakisafirishwa kwenye treni na meli ambazo nazo ni public transport, I don't see any problem.
 
Kiulizni ni hatari sana na haipaswi kusafirishwa hivyo, kwani kunaweza kutokea njama za kumtorosha kwa kuliteka Basi.

Pia hairuhusiwi kuingia na Silaha aina yoyote ndani ya Basi la Abiria, na hao Askari bila shaka kama walikuwa hawana bunduki huenda walikuwa na Pistol ambapo ni hatari sana.

Walipaswa kwa safari ndefu kama hiyo kutumia usafiri wa binafsi na siyo basi la abiria.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom