Mfumuko wa bei

hakiba

Member
Jun 1, 2021
19
33
Salama wakuu.

Kwa wale tuliobahatika kusoma uchumi kwa kiasi chake,hebu tuzungumze kuhusu hili suala la mfumuko wa bei "inflation" .Nimekuwa nikiona mara kadhaa serikali ikitoa takwimu na namna ambavyo inapambana kudhibiti mfumuko wa bei nchini,lakini hii imekuwa ikinipa maswali flani flani mimi binafsi, je njia zinazotumika kuzuia mfumuko wa bei hapa nchini ni salama kwa uchumi wa mtanzania mmoja mmoja?

Je, ni kweli uzalishaji wa bidhaa unakwenda sawa na uhitaji wa bidhaa uliopo? Na tukumbuke ya kwamba increase in income lead to increase in demand and it may lead to increase in price if suppy remain constant. Na bei ikishaongezeka ndo unaweza kutokea mfumuko wa bei huko.

To make my thread short,niweke wazi namna ambavyo mimi naiona hii kitu ya kuzuia mfumuko wa bei inayofanywa na serikali kisha na nyie mtatoa mitazamo yenu.

Mimi nafikiri ya kwamba mfumuko wa bei umekuwa ukipungua kutokana na kwamba vipato vya watu vipo chini au vimebaki pale pale,hapawezi kuwa na mfumuko wa bei kama vipato vya watu vipo chini.na huenda hakuna effort yeyote inafanyika isipokuwa hii tu mfano kama kutokuongeza mishahara n.k

Hili kwenu limekaaje au mnalionaje?

Note: Sisemi pawepo na mfumuko wa bei lakini najaribu kuiwaza hii kitu kiuchumi zaidi.Nimekuwa nikijiuliza maswali kuhusu suala hili na leo niliona muongozo wa chama cha mapinduzi kwa wizara ya fedha katika bejet ya serikali itakayopitishwa, katika vipaumbele ambavyo chama kimetoa kama suala la kuangalia miongoni mwavyo ni hili la mfumuko wa bei.

Karibu utoe mawazo yako.

Salaaam.
 
Back
Top Bottom