Ni ipi kazi ya vyama vya wafanyakazi, kama kwa mfumuko wa bei hivi sasa hakuna chama chochote kimetoa kauli kutetea maboresho ya mishahara?

Ni ipi kazi ya vyama vya wafanyakazi, kama kwa mfumuko wa bei hivi sasa hakuna chama chochote kimetoa kauli kutetea maboresho ya mishahara?

gimmy's

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Posts
3,330
Reaction score
3,388
Ndugu zangu vita inayoendelea Irani imesababisha upandaji wa bei ya nishati kitu ambacho kimesababisha mfumuko wa bei kwenye bidhaa karibu zote,kwenye uchumi gharama za nishati/mafuta/gas zikipanda lazima bei ya bidhaa ipande.

Kwasasa hali ya maisha kwa upande wa wafanyakazi imekua mbaya zaidi kwani kipato cha mtumishi kwa mwezi ni fixed.

Inapotokea upandaji wa gharama za maisha kwa kiwango kikubwa kama ilivyo sasa wahanga wa kwanza ni wafanya kazi.

Nauli za usafiri makazini zimepanda kiasi ambacho watumishi inawalazimu wakati fulani kutembea waendapo makazini,

Bidhaa kama gas yakupikia nayo tayari imepanda mara dufu,hivi kukaa kimya ni sawa?

Upo utitiri wa vyama vya wafanyakazi lakini haieleweki vina msaada gani kwa hao wanaowatumikia.

Kama walikua wamelala basi sasa waamke wajue wajibu wao,

Kama viongozi wa vyama vya wafanyakazi waliopo wamewekwa na dola basi ni vizuri wajitafakari kama bado wanapaswa kuendelea kuwepo kwenye nafasi zao.
 
Viongozi wa hivyo vyama wote wamewekwa na dola. Niamini mimi huto sikia yeyote ananyanyua bakuli lake na kukemeaa chochote
 
Kwenye utawala wa Jakaya namkumbuka kiongozi mmoja wa chama cha wafanyakazi nafikiri aliitwa Mgaya yule jamaa alimnyima usingizi Jakaya
 
Ni mpaka lini tutaamini matatizo yetu wenyewe ni lazima tupiganiwe na vyama vya siasa? Kwa nini wananchi tusiingie barabarani kuishinikiza serikali kuchukua hatua?
 
Wenye mishahara wana lalamika kuliko ma jobless
 
Back
Top Bottom