Mfumuko wa bei: Vifaa vya ujenzi na vyakula vyapaa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,198
25,517
Bei za vifaa vya ujenzi na vyakula zimepaa maradufu mara baada ya kuanza kwa awamu ya tano. Mfano,wilayani Kibaha mfuko wa saruji unauzwa kwa 13500 kutoka 13000 ya mwanzo. Bei pia imeongezeka kwa bati na hata mbao.

Bei za nyama zimepaa huko Zanzibar na hata mkoani Mtwara. Huko Mtwara,kilo ya nyama inauzwa 8000 badala ya 6000. Huko Zanzibar,kilo ya nyama imefika kati ya 10000 na 15000.

Na mfumuko wa bei utupiwe jicho. Kimsingi,bei za bidhaa ndizo zinazogusa maisha ya siku hadi siku ya wananchi wa kawaida.
 
Mh. Rais Magufuli aliahidi Cement na vifaa vya Ujenzi vitashuka bei.

Kwenye Stronghold za CCM kama Dodoma, Morogoro, Iringa, Singida, na Tanga pembezoni Nyumba ni za Udongo..Tembe na hazina Bati...Nyasi au tope..... Sasa huu ni mtihani kwa Mh. Magufuli..please take action.

Kuna tetesi zimesambaa sana Tanzania nzima kuwa DANGOTA Alitaka kuuza Cement kwa 8500 Tshs kwa mfuko...ETI CCM Wakakataa. Mh... Rais, look at this.

Mh. Rais, usipofanyia kazi haya mambo, ujue wapiga kura wako DODOMA, Singida, Morogoro umewaonea sana....

Kwa nini Cementi Ktoka Kenya ni bei rahisi kutoka Tanzania?

Kwa nini Cementi ya Pakistani ni rahisi kuliko ya Tanzania?
 
Bei ya bidhaa mbalimbali (vyakula,vifaa vya ujenzi )zilipanda tangu kampeni za uchaguzi mkuu zilipoanza
 
Bei za vifaa vya ujenzi na vyakula zimepaa maradufu mara baada ya kuanza kwa awamu ya tano. Mfano,wilayani Kibaha mfuko wa saruji unauzwa kwa 13500 kutoka 13000 ya mwanzo. Bei pia imeongezeka kwa bati na hata mbao.

Mkuu hata ongezeko la 500 katka 13000 ni maradufu?
 
Hello Ndugu Sometimes, nakujibu hivi kitaalamu.

Bei ya bidhaa inatokana na vitu hivi

A - Malighafi

B- Gharama za uzalishaji ambazo ni wafanyakazi, umeme, maji na simu

C- Kodi za serikali

Maelezo:

Wafanyakazi wa Tanzania wanalipwa mshahara mdogo sana ukiondoa management ambao ni wachache

Malighafi nyingi inapatikana Tanzania, ni udongo wetu.

Kitu ambacho kinaleta bei kuwa kubwa ni Kodi za serikali..... Raisi anaweza kuchukua hatua mfano kupunguza kodi, badala yake akawaagiza TRA kukusanya kodi kutoka wafanyabiashara wakubwa

Kuacha matumizi makubwa mfano sasa anavyofanya sasa.

----Wewe Ndugu Sometimes, Mh. Rais ameshasema ataleta mabadiliko, na ameanza.... Kama wewe umebaki kizamani zamani na awamu ya 4 -- Pole sanaaa.....
 
Nipo kibaha hadi tunavyoongea leo 23 ,11 2015 cement ni 14500 na nyama imekuwa 9000 kutoka 6000.. Ukiwauliza wauzaji wanasema. #Hapa Kazi Tu# ngoja tusubiri tuone.
 
Umekula maharage ya wapi
Nafikiri haujasoma vizuri mtoa mada alichoandika. Amesema "Bei za vifaa vya ujenzi na vyakula zimepaa maradufu mara baada ya kuanza kwa awamu ya tano." Sasa unatajaje Awamu ya tano bila kumhusisha Mhe. Magufuli? Kuhusu maharage nimekula ya kwenu!
 
Mh. Rais Magufuli aliahidi Cement na vifaa vya Ujenzi vitashuka bei.

Kwenye Stronghold za CCM kama Dodoma, Morogoro, Iringa, Singida, na Tanga pembezoni Nyumba ni za Udongo..Tembe na hazina Bati...Nyasi au tope..... Sasa huu ni mtihani kwa Mh. Magufuli..please take action.

Kuna tetesi zimesambaa sana Tanzania nzima kuwa DANGOTA Alitaka kuuza Cement kwa 8500 Tshs kwa mfuko...ETI CCM Wakakataa. Mh... Rais, look at this.

Mh. Rais, usipofanyia kazi haya mambo, ujue wapiga kura wako DODOMA, Singida, Morogoro umewaonea sana....

Kwa nini Cementi Ktoka Kenya ni bei rahisi kutoka Tanzania?

Kwa nini Cementi ya Pakistani ni rahisi kuliko ya Tanzania?

MPadmire, cement ya Kenya imepigwa marufuku (kwa huku nlipo haipo tena madukani).., ni kweli ilikuwa inauzwa kwa bei nafuu kidogo ukilinganisha na simba cement!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom