mycall
JF-Expert Member
- Dec 17, 2014
- 867
- 523
Bei za vifaa vya ujenzi na vyakula zimepaa maradufu mara baada ya kuanza kwa awamu ya tano. Mfano,wilayani Kibaha mfuko wa saruji unauzwa kwa 13500 kutoka 13000 ya mwanzo. Bei pia imeongezeka kwa bati na hata mbao.
Bei za nyama zimepaa huko Zanzibar na hata mkoani Mtwara. Huko Mtwara,kilo ya nyama inauzwa 8000 badala ya 6000. Huko Zanzibar,kilo ya nyama imefika kati ya 10000 na 15000.
Na mfumuko wa bei utupiwe jicho. Kimsingi,bei za bidhaa ndizo zinazogusa maisha ya siku hadi siku ya wananchi wa kawaida.
Mimi naona bei ya nyama haijapanda,waongeze ifike kilo sh.20000 labda serikali itaona umhimu wa wafugaji
Wanathamini nyumbu, pundamilia na sokwe kuliko hata binadamu. Wafugaji wanapigwa risasi na wanafukuzwa kila sehemu, wanaambiwa wapunguze idadi ya ng'ombe. Sasa wameitikia wito ng'ombe wamepungua imekuwa malalamiko kila kona.
Nafikiri sasa serikali iruhusu tuanze kutumia nyumbu kama kitoweo maana ng'ombe hawana thamani kama nyumbu.Ndiyo maana sijawahi kusikia serikali ikisema ipunguze maeneo ya hifadhi ili wafugaji wapate malisho.
Anaye lalamikia bei ya nyama ajuwe sababu ni sisi wenyewe pamoja na serikali kupuuza na kudharau mahitaji ya wafugaji.
Nyama ndo kilikuwa kitoweo rahisi na kinachopatikana popote karibu na maeneo tunayoishi, serikali haioni umhimu huh,sasa ngoja tuisome namba.