Mfumo mbovu wa elimu unatoa wataalamu wabovu na ni vigumu kuchukua wataalamu hawa wabovu wakuboreshee mfumo wenyewe wa elimu uliowatengeneza.
Wataishia kuhamisha hiki kule na kurudisha hiki huku lakini mwisho wa siku mtabaki palepale mkiwa na elimu ileile ila mpangilio tofauti. Elimu ni maarifa yale mtu anayapata kichwani mwake na hivyo kutumia wataalamu walewale ni sawa na kujitungia mtihani na kujisahihisha, Utatunga unayoyajua na hata majibu utakayokosea utajipa tiki maana uelewa wako unakuambia hayo ndo majibu.
Kama tunahitaji kupata elimu bora ni bora tufanye yafuatayo.
1. tuainishe mapungufu yaliyopo katika products zinazotoka katika elimu yetu. Hapa ikiwezekana tuchukue utafiti tuwahoji watu wa vijijini wanona mapungufu gani kwa watoto wetu wanaotoka shule, tuwahoji watu wa mijini wanaona mapungufu gani, tutazame jamii zetu zina changamoto gani ambazo wataalamu wameshindwa kuzitatua, tuwahoji wataalamu wetu waliofanya kazi na wageni waliotoka mataifa yenye mifumo tofauti wameona tofauti zipi katika wataalamu wa nje na wao au wataalamu wetu, tuwahoji wageni wanaona mapungufu gani kwa wataalamu wetu.
2. Tufanye utafiti wa mifumo ya elimu kwa wenzetu, mtoto wa chekechea anafundishwa mambo gani, msingi anafundishwa mambo gani, sekondari anafundishwa mambo gani, vyuoni wanafundishwa mambo gani. Tutafute haya wanayofundishwa wanatumia utaratibu gani. hapa tutazame nchi zilizopiga hatua kama america, japani, china. Tutafute nchi zilifanya mapinduzi ya haraka kama Thailand.
3. Tuweke malengo ya elimu kwa awamu tofauti, yaani kama hatuna haja ya kuweka msisito katika elimu ya anga za mbali kama kuwakalilisha watoto vipenyo vya sayari zote, hali ya hewa ya huko, n.k kwa sasa kwa kuwa uchumi wetu haujafika kwenye sisi kwenda anga za mbali. tuweke malengo ya elimu yetu kwa sasa katika mambo ambayo tunategemea kuyafanya ndani ya miaka kadhaa ijayo ili watoto wakimaliza wanayafanyia kazi. Tutaenda tuna badili malengo kutokana na jamii yetu inavyobadirika.
5. Tuchunguze mitaala iliyokuwepo au mazingira yaliyokuwepo yamechangiaje katika changamoto tulizonazo
4. Tukishapata changamoto na maono yetu ndipo tukae chini kutengeneza mitaala ya eimu yenye kutoa majibu. Hapa tutumie wataalamu wetu wa ndani kutengeneza majibu 1, tutumie wataalamu wa nje labda kutoka marekani kutengeneza majibu 2, tutumie wataalamu kutoka ulaya kutengeneza majibu 3, tutumie wataalamu kutoka asia kutengeneza majibu 4.
5. mwisho ni kuchukua majibu yote manne na kuyachambua kuchagua majibu yenye tija zaidi.
Hapa tunaweza kuleta mapinduzi makubwa katika jamii yetu.
Tukifanya makosa tutajikuta tunacheza na namba za miaka ya kusoma, futa topic fulani na leta topic nyingine lakini unakuta tunatumia watu walewale kufanya makosa yaleyale tuliyokuwa tukifanya mda wote na mwishi hatutapata matunda.
Elimu ni mzizi wa maendeleo, na ukitumia gharama kubwa katika kupanga utapata tija katika utekelezaji.
Tusione gharama kubwa kuwa na tume tatu, nne kila moja ikitafuta majibu ya kwake alafu baadae tupitie na majibu yote na kuibuka na jibu moja.