Mfumo wetu wa elimu hauwezi kuboreshwa na wasomi waliotokana na mfumo wenyewe

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Mfumo mbovu wa elimu unatoa wataalamu wabovu na ni vigumu kuchukua wataalamu hawa wabovu wakuboreshee mfumo wenyewe wa elimu uliowatengeneza.

Wataishia kuhamisha hiki kule na kurudisha hiki huku lakini mwisho wa siku mtabaki palepale mkiwa na elimu ileile ila mpangilio tofauti. Elimu ni maarifa yale mtu anayapata kichwani mwake na hivyo kutumia wataalamu walewale ni sawa na kujitungia mtihani na kujisahihisha, Utatunga unayoyajua na hata majibu utakayokosea utajipa tiki maana uelewa wako unakuambia hayo ndo majibu.

Kama tunahitaji kupata elimu bora ni bora tufanye yafuatayo.

1. tuainishe mapungufu yaliyopo katika products zinazotoka katika elimu yetu. Hapa ikiwezekana tuchukue utafiti tuwahoji watu wa vijijini wanona mapungufu gani kwa watoto wetu wanaotoka shule, tuwahoji watu wa mijini wanaona mapungufu gani, tutazame jamii zetu zina changamoto gani ambazo wataalamu wameshindwa kuzitatua, tuwahoji wataalamu wetu waliofanya kazi na wageni waliotoka mataifa yenye mifumo tofauti wameona tofauti zipi katika wataalamu wa nje na wao au wataalamu wetu, tuwahoji wageni wanaona mapungufu gani kwa wataalamu wetu.

2. Tufanye utafiti wa mifumo ya elimu kwa wenzetu, mtoto wa chekechea anafundishwa mambo gani, msingi anafundishwa mambo gani, sekondari anafundishwa mambo gani, vyuoni wanafundishwa mambo gani. Tutafute haya wanayofundishwa wanatumia utaratibu gani. hapa tutazame nchi zilizopiga hatua kama america, japani, china. Tutafute nchi zilifanya mapinduzi ya haraka kama Thailand.

3. Tuweke malengo ya elimu kwa awamu tofauti, yaani kama hatuna haja ya kuweka msisito katika elimu ya anga za mbali kama kuwakalilisha watoto vipenyo vya sayari zote, hali ya hewa ya huko, n.k kwa sasa kwa kuwa uchumi wetu haujafika kwenye sisi kwenda anga za mbali. tuweke malengo ya elimu yetu kwa sasa katika mambo ambayo tunategemea kuyafanya ndani ya miaka kadhaa ijayo ili watoto wakimaliza wanayafanyia kazi. Tutaenda tuna badili malengo kutokana na jamii yetu inavyobadirika.

5. Tuchunguze mitaala iliyokuwepo au mazingira yaliyokuwepo yamechangiaje katika changamoto tulizonazo

4. Tukishapata changamoto na maono yetu ndipo tukae chini kutengeneza mitaala ya eimu yenye kutoa majibu. Hapa tutumie wataalamu wetu wa ndani kutengeneza majibu 1, tutumie wataalamu wa nje labda kutoka marekani kutengeneza majibu 2, tutumie wataalamu kutoka ulaya kutengeneza majibu 3, tutumie wataalamu kutoka asia kutengeneza majibu 4.

5. mwisho ni kuchukua majibu yote manne na kuyachambua kuchagua majibu yenye tija zaidi.

Hapa tunaweza kuleta mapinduzi makubwa katika jamii yetu.

Tukifanya makosa tutajikuta tunacheza na namba za miaka ya kusoma, futa topic fulani na leta topic nyingine lakini unakuta tunatumia watu walewale kufanya makosa yaleyale tuliyokuwa tukifanya mda wote na mwishi hatutapata matunda.

Elimu ni mzizi wa maendeleo, na ukitumia gharama kubwa katika kupanga utapata tija katika utekelezaji.

Tusione gharama kubwa kuwa na tume tatu, nne kila moja ikitafuta majibu ya kwake alafu baadae tupitie na majibu yote na kuibuka na jibu moja.
 
Hoja kuntu. Sifa za kwenda mjengoni ni kujua kusoma na kuandika hivyo watu wenye sifa hizi hawawezi kuuchakata mfumo wa elimu nchini na kuja na maboresho yatakayoisaidia nchi.
 
Wanasema huwezi tatua tatizo kwa akili ile ile iliyotengeneza tatizo.

Inshu hapa leteni washauri wa kielimu kutoka mataifa ya nje yaliyoendelea katika mifumo ya kielimu..leta wachina,wazungu waarabu wahindi.

Watupe uzoefu na ushauri wao kisha tulinganishe na maisha yetu halisi kisha tufanye maamuzi.

Tofauti na hapa yatakuja yale yale masuala ya phsychemistry.

Suala la miaka ya kusoma ipunguzwe asee..mana mtoto anatumia nusu ya maisha yake kusoma tu.

Angalau 21 mtoto kamaliza digrii yake ya kwanza.

#MaendeleoHayanaChama

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfumo mbovu wa elimu unatoa wataalamu wabovu na ni vigumu kuchukua wataalamu hawa wabovu wakuboreshee mfumo wenyewe wa elimu uliowatengeneza.

Wataishia kuhamisha hiki kule na kurudisha hiki huku lakini mwisho wa siku mtabaki palepale mkiwa na elimu ileile ila mpangilio tofauti. Elimu ni maarifa yale mtu anayapata kichwani mwake na hivyo kutumia wataalamu walewale ni sawa na kujitungia mtihani na kujisahihisha, Utatunga unayoyajua na hata majibu utakayokosea utajipa tiki maana uelewa wako unakuambia hayo ndo majibu.

Kama tunahitaji kupata elimu bora ni bora tufanye yafuatayo.

1. tuainishe mapungufu yaliyopo katika products zinazotoka katika elimu yetu. Hapa ikiwezekana tuchukue utafiti tuwahoji watu wa vijijini wanona mapungufu gani kwa watoto wetu wanaotoka shule, tuwahoji watu wa mijini wanaona mapungufu gani, tutazame jamii zetu zina changamoto gani ambazo wataalamu wameshindwa kuzitatua, tuwahoji wataalamu wetu waliofanya kazi na wageni waliotoka mataifa yenye mifumo tofauti wameona tofauti zipi katika wataalamu wa nje na wao au wataalamu wetu, tuwahoji wageni wanaona mapungufu gani kwa wataalamu wetu.

2. Tufanye utafiti wa mifumo ya elimu kwa wenzetu, mtoto wa chekechea anafundishwa mambo gani, msingi anafundishwa mambo gani, sekondari anafundishwa mambo gani, vyuoni wanafundishwa mambo gani. Tutafute haya wanayofundishwa wanatumia utaratibu gani. hapa tutazame nchi zilizopiga hatua kama america, japani, china. Tutafute nchi zilifanya mapinduzi ya haraka kama Thailand.

3. Tuweke malengo ya elimu kwa awamu tofauti, yaani kama hatuna haja ya kuweka msisito katika elimu ya anga za mbali kama kuwakalilisha watoto vipenyo vya sayari zote, hali ya hewa ya huko, n.k kwa sasa kwa kuwa uchumi wetu haujafika kwenye sisi kwenda anga za mbali. tuweke malengo ya elimu yetu kwa sasa katika mambo ambayo tunategemea kuyafanya ndani ya miaka kadhaa ijayo ili watoto wakimaliza wanayafanyia kazi. Tutaenda tuna badili malengo kutokana na jamii yetu inavyobadirika.

5. Tuchunguze mitaala iliyokuwepo au mazingira yaliyokuwepo yamechangiaje katika changamoto tulizonazo

4. Tukishapata changamoto na maono yetu ndipo tukae chini kutengeneza mitaala ya eimu yenye kutoa majibu. Hapa tutumie wataalamu wetu wa ndani kutengeneza majibu 1, tutumie wataalamu wa nje labda kutoka marekani kutengeneza majibu 2, tutumie wataalamu kutoka ulaya kutengeneza majibu 3, tutumie wataalamu kutoka asia kutengeneza majibu 4.

5. mwisho ni kuchukua majibu yote manne na kuyachambua kuchagua majibu yenye tija zaidi.

Hapa tunaweza kuleta mapinduzi makubwa katika jamii yetu.

Tukifanya makosa tutajikuta tunacheza na namba za miaka ya kusoma, futa topic fulani na leta topic nyingine lakini unakuta tunatumia watu walewale kufanya makosa yaleyale tuliyokuwa tukifanya mda wote na mwishi hatutapata matunda.

Elimu ni mzizi wa maendeleo, na ukitumia gharama kubwa katika kupanga utapata tija katika utekelezaji.

Tusione gharama kubwa kuwa na tume tatu, nne kila moja ikitafuta majibu ya kwake alafu baadae tupitie na majibu yote na kuibuka

Wanasema huwezi tatua tatizo kwa akili ile ile iliyotengeneza tatizo.

Inshu hapa leteni washauri wa kielimu kutoka mataifa ya nje yaliyoendelea katika mifumo ya kielimu..leta wachina,wazungu waarabu wahindi.

Watupe uzoefu na ushauri wao kisha tulinganishe na maisha yetu halisi kisha tufanye maamuzi.

Tofauti na hapa yatakuja yale yale masuala ya phsychemistry.

Suala la miaka ya kusoma ipunguzwe asee..mana mtoto anatumia nusu ya maisha yake kusoma tu.

Angalau 21 mtoto kamaliza digrii yake ya kwanza.

#MaendeleoHayanaChama

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
100 % true

yabo mambo mengi sana mengine yanahusu maudhui yanayofundishwa

mengine yanahusu mda wa kufundisha

mengine yanahusu mbinu za kufundishia.

yaani tunataka "comprehensive education overhaul"
 
Kwa elimu yetu hii
Ukijitambua na kuweza kuhandle uchumi wako mwenyewe shukuru sana
 
Ndiyo maana wanasema wasomi wanashindwa kujiajiri. yaani watu wanafundishwa irrelevant materials tofauti na kinachoendelea on ground
 
Umeeleza vizuri kwenye heading tu

Solution ndogo tu.ukiona mfano mfumo wa elimi wa VETA wa China ni mzuri just copy and paste ulete Tanzania
 
haya ndiyo tunataka hawa viongozi watufanyie.

Lakini siyo kumchukua mwalimu wa veta huyo huyo eti akuandalie maboresho ya elimu ya veta. Fikra zitabaki zilezile ila zitafanyiwa rearangement kidogo.

Kuchukua wataalamu wetu kuboresha elimu yetu ni sawa mwalimu wa veta kutumika kuboresha elimu ya veta.

sisi tunataka kujua mtoto anayesoma ufundi marekani kwa ngazi kama ya veta anasoma nini? wa ulaya anasoma nini? wa china anasoma nini? wa india anasoma nini?

katika hayo yote tutazame wa kwetu tumsomeshe yapi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom