Ingawa hata hao wapinzani wana mapungufu yao, ila ni ukweli ulio wazi; Ccm inatumia nguvu nyingi sana ili tu kuendelea kuwatawala watanzania.
Mkitaka fair competition, muwaruhusu na hao wapinzani wenu wafanye mikutano ya kisiasa nchi nzima, rudisheni bunge live, ipitisheni tu ile rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba kama ilivyo, halafu ndani yake kuwe na tume 'huru' ya uchaguzi (siyo hii ya kusimamiwa na wakurugenzi), polisi kazi yao ibakie tu kuangalia usalama na isionekane inawakandamiza hao wapinzani kwa namna yoyote ile!
Hakika saa mbili tu asubuhi mtakua mmesha angukia pua hata kama hao wapinzani wataweka tu kwenye zile fomu za kuchagua wagombea 'picha ya jiwe kubwaaaa'!