Mfumo wa usajili majina ya biashara BRELA

Planeti

Member
Jun 4, 2020
86
93
Wakuu habari zenu,

Nimeanza jana kujaribu kusajili Jina la biashara kwa mfumo wa Brela ORS. Nimejisajili vizuri tu ili kuendelea na hatua inayofata, sasa shida ndio imeanzia hapo..

Kila nikijaribu kupakia taarifa ili kuendelea na hatua inayofuata, wao hunigomea. Wanadai kuna taarifa sijazijaza. Narudi kuzijazza tena kwa usahihi kabisa, lakini jamaa wanaendelea kudai nimekosea.

Nimejaribu hadi nimechoka, nadhani hii ni mara ya 100, na hatimae nimechoka. Imagine wanadai sijajaza taarifa za maeneo ya biashara, mara sijui namba ya simu. Nimepiga huduma kwa wateja lakini napo sijapata msaada.

Nimekuja kwenu ndugu jamaa na marafiki. Naombeni msaada wenu.

Nimeshindwa kuscreenshort sababu natumia PC.

Karibuni
 
Mi nadhani tatizo ni system yao maana hata mimi yamenikutahadi sasa sijafanikiwa.

Kwanza nilifanya mwenyewe nikashindwa ndipo nikawaendea kwenye maonesho ya biashara yalikuwa Dodoma nikawaeleza wakasema ngoja tukuingizie data wenyewe kwenye mfumo then wakaniambia tayari utasibiri siku kama tatu then utatumiwa control number ukalipie. Nimekaa siku tatu ikaja sms ile ile kama ya mwanzo kuwa taarifa zangu hazijakamilika wakati wameingiza wenyewe.

Kwa ufupi ni shida na kwa njia hii tusahau kupata wawekezaji ambao ni serious. Hata waziri mweye dhamana nimejaribu kumtumia sms bado hajachukua hatua.
 
Back
Top Bottom