KERO Mfumo wa ESS kwa watumishi

KERO Mfumo wa ESS kwa watumishi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

kwe2tu

Senior Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
140
Reaction score
230
Mimi ni mojawapo ya mtumishi ambae nimeathiriwa na mfumo huu wa ESS katika upandishaji wa madaraja.

Nimejaribu kufatilia je, ni sehemu gani sijaenda sawa hata sioni ninaandaa azimio la kazi ninaandaa andalio la somo ninasaini log book. Ninaandaa zana za kufundishia, ninasaini class journal, nipo shuleni kila siku nina saini out and in

Na katika mfumo mpk mwezi wa 12 nilifikisha aslimia 100. Lkn nakuja kuangalia baada ya mfumo kufungwa nakuta nina 58% na kunifanya nisipandishwe daraja na hivyo kuathili maisha yangu kwa sehemu.

Cha kushangaza zaidi mpk shuleni kwangu nimepewa zawadi kwa kufaulisha wanafunzi kwa kuwa na A na B nyingi lkn wamegoma kunipandisha eti asilimia ni ndogo. Nimeumia sana.
USHAURI KWA WAHUSIKA

1. Nashauri kuwe na njia nyingine ya kutathimini utendaji wa kazi wa mwl km vile class journal. Attendances na mkuu wa shule pia kuliko kutegemea asilimia za kwenye mfumo tu. Kwani kwa kutegemea mfumo tu watu wanaweza kukaa nyumbani na kujaza tu na wakawa na asilimia nyingi lkn darasani ht hawaingii ( sisemi wote)
2. Mtazamo wangu huu mfumo wa asilimia ht hauna uhalisia sehemu nyingi mtu analipwa pesa anawajazia walimu wote na sio kila mwl kujaza je uhalisia uko wapi hapo. Huu mfumo ungebaki kwa ajili ya huduma nyingine na isiwe kingezo cha kupandisha walimu madaraja
Lbd ingebaki kuombea mikopo. Uhamisho na likizo tu.

Nina uhakika niliyeonewa sio mimi tu watumishi wengi wanalia kwa mfumo huu tunaomba mamlaka itazame kwa upya na itusaidie sisi tulioonewa.

Wako
Hata kesho nisiku
 
Uliajiriwa lini? Na huu mfumo hauwezi kushusha mtu asilimia kama supervisor wako ali aprove sub task zako, huu mfumo wa ESS umekuwa msaada mkubwa sana kwa watumishi, pia jitahidi kuwa unajaza majukumu yako kwa wakati.
 
Mwalimu unataka kuturudisha analogia,shida hamtaki kwenda na wakati.

Anaway jitahidi utumie mfumo mana kwa sasa ni new norm
 
Okay

Umeajiriwa mwaka gani?

Supervisor alikua anaaprove kazi?

Supervisor aliconclude tathmini ya mwisho wa mwaka?

Angalia wapi hapako sawa kwenye hivi vitu
 
Okay

Umeajiriwa mwaka gani?

Supervisor alikua anaaprove kazi?

Supervisor aliconclude tathmini ya mwisho wa mwaka?

Angalia wapi hapako sawa kwenye hivi vitu
Mkuu nimepanda mara ya mwisho 2023 kwahiyo mwaka huu nilistahili lkn hiyo ya supervisor sijui kwakweli
 
unapanda daraja kwa kutumia score angalau 75 sio percentage... kama ulifikisha percentage 100 automatic ungekuwa na score 70 supervisor wako alitakiwa kufanya assesment kuongezea izo 30.. kwahiyo LIA na supervisor wako labda aliset indicators vibaya
 
Nashangaa sana inaonekana supervisor wengi hawawapi maksi wafanyakazi wao kwa maksudi au kutofahamu.
unapanda daraja kwa kutumia score angalau 75 sio percentage... kama ulifikisha percentage 100 automatic ungekuwa na score 70 supervisor wako alitakiwa kufanya assesment kuongezea izo 30.. kwahiyo LIA na supervisor wako labda aliset indicators vibaya
 
Inaonekana mkuu wako hakukufanyia assesment kabisa ndo maana alama zako hazikufika.Ata kama mkuu alikosea kuset alama 30 na 70 mwaka jana mfumo uliruhusu kumuasess mtu kwa kumwekea marks mpaka 100.Hivo ata kama ww mwalimu maks zako ziligotea 30 yeye mkuu alikuwa na uwezo wa kuzipandisha maka ata 100 kama angekufanyia assessment.Mfumo ni mzuri sana ila wasimizi ndo hawakufanya assessment ndo maana umekwama kufikisha 75
 
Back
Top Bottom