Mfumo mpya ununuzi wa korosho kuvuna bil.720/

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1572682781674.png


MFUMO mpya wa ununuzi wa korosho kwa msimu wa mwaka 2019/2020, unatarajia kuwaingizia wakulima Sh bilioni 720. Tayari mfumo huo umeanza kwa mafanikio, baada ya minada ya kwanza iliyofanyika juzi katika Wilaya za Tandahimba na Masasi, ambapo vyama viwili vikuu vya Ushirika vya TANECU na MAMCU viliendesha minada hiyo kwa kutumia mfumo wa zabuni wa wazi na kuingiza Sh bilioni 50.7.

Katika minada hiyo, korosho za daraja la kwanza ziliuzwa kwa Sh 2,559 kwa kilo na daraja la pili ziliuzwa kwa Sh 2,456 kwa kilo, ambapo jumla ya tani 20,000 zilinunuliwa kwa Sh bilioni 50.7. Akizungumza baada ya uzinduzi huo wa mauzo ya korosho kwa mfumo mpya akiwa mkoani Mtwara, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema wakulima wa korosho wa mikoa inayolima korosho nchini, wanatarajia kunufaika na fedha zaidi ya Sh bilioni 720 baada ya msimu kuanza juzi. Waziri huyo alisema fedha hizo, zitapatikana baada ya mavuno tarajiwa kuwa zaidi ya tani 290,000 kutoka tani 225,105 za msimu uliopita.

Alisema kwa mwaka huu, minada yote itakuwa ikiendeshwa kwa uwazi, tofauti na miaka iliyopita na kwamba serikali itausimamia mfumo huo ili kuwalinda wakulima. “Mfumo wa kuuza korosho unaotumika katika msimu wa 2019/2020 ni mfumo wa zabuni wa wazi, ambapo wanunuzi wanatumbukiza barua (zabuni) zao kwenye sanduku zikionesha bei, kiasi cha korosho wanazohitaji, ghala zilipo na taarifa za makampuni.

“Zabuni zinawekwa kwenye sanduku kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni na baada ya hapo sanduku la zabuni linafunguliwa na mnada kufanyika, ambapo baada ya wakulima kuridhia mshindi anatangazwa mbele ya wakulima siku hiyo hiyo,” alisema Waziri Hasunga.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Korosho, Francis Alfred alisema bei ya korosho kwa kilo moja kwa daraja la kwanza, itaendelea kupanda kutokana na sababu mbalimbali. “Bei ya korosho katika Soko la Dunia hupanda na kushuka, mpaka kufikia jana (juzi) bei ya korosho ghafi pamoja na gharama ya kusafirishs (CIF) nchini India ilikuwa kati ya dola ya Marekani 1,550 hadi 1,725 kwa tani moja.

Hivyo bei waliyouza korosho wakulima ya jana ya shilingi 2,559 mali ghalani (EXW) inaendana na mwenendo korosho duniani kwa daraja la kwanza,” alisema. Hata hivyo, jana ulikuwa ni mnada wa kwanza ambapo ni asilimi 50 tu ya wanunuzi waliosajiliwa, walijitokeza ili kushiriki minada hiyo miwili. “Tunataraji minada ijayo ya Jumamosi Novemba 2 chini ya usimamizi wa Chama Kikuu cha Ushirika Lindi (LINDI MWAMBAO) na Jumapili Novemba 3, chini ya Chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI itakuwa na wanunuzi zaidi na ushindani utaongezeka,” alisema Alfred.

Alisema wanunuzi waliojitokeza kununua korosho katika minada hiyo, walikuwa ni 55 ambapo katika mnada wa MAMCU kulikuwa na wanunuzi 27 na mnada wa TANECU kulikuwa na wanunuzi 28. Alfred alisema kuwa idadi ya makampuni yaliyosajiliwa kwa ajili ya ununuzi wa zao la korosho nchini kwa msimu huu hadi juzi ni 73, lakini kati ya hayo makampuni yaliyotimiza vigezo vyote, ikiwa ni pamoja na kuweka kinga ya zabuni (security bond) na kupatiwa leseni ni 37.

Aliyataja makapuni hayo kuwa ni: 3d & b holding co Ltd, Afri (E.A) Ltd, Afrisian Ginning Ltd, Agricova Tanzania Limited, Alpha Choice Ltd, Alpha Namata Company Ltd, Blazing Star Company Ltd, BPS Impex Tanzania Limited, Budang Cashew Co Ltd, Cdjkl Nuts Ltd, Dizygotic BA Company Limited, Easy Dream Co Ltd, ECM Trends Limited, Export Trading Company Limited, Govind Agri Commodities (T) Ltd.

Mengine ni Green Bridge (TZ) Ltd, Imperial Cashew Trading Limited, Iscon Commodities (T) Limited, Kijani Crops Exportations Tanzania Ltd, Korosho Africa Limited, Maragi Limited, Micronix Systems Limited, Mohamed Enterprises Ltd, Nafaka Commodities Limited, Rbst International Agribusiness Limited na Royal Nuts Tanzania Limited.

Zipo pia Sibatanza Limited, SM Exim (T) Private Limited, SM Holdings Limited, Star Brands Ltd, Subh Nuts Trading Company Limited, Sunshine Commodities Pvt Ltd, Tanzania Commodities Trading Company Limited, Tastey Nuts Commodities Limited, Taza Trading & Investment Limited, Valency Agro Tanzania Ltd na Virtue International Co. Ltd.
 
Hayo makampuni yakisha nunu korosho yanauza nje hivyo hivyo au yanabangua maana ilisemekana marufuku kuuza korosho tutabangua wenyewe..
 
Kwa bei ya msimu uliopita ya 3300 serikali iliingia hasara?
So waliwagomea bure wafanyabiashara ambao walikuwa wanatoa bei kuendana na bei ya soko la dunia
 
Back
Top Bottom