Mfuko wa Utamaduni Tanzania unamfaa nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfuko wa Utamaduni Tanzania unamfaa nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kimatire, Mar 31, 2009.

 1. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia Mfuko huu wa Utamaduni kama kweli unawafikia walengwa wa sekta ya Utamaduni.
  Wale wanaoujua naomba wanimegee ni kwa kiasi gani unatufaa wadau.Binafsi nimepeleka maombi yangu mara tisa bila mafanikio,Kila nikiwatembelea pale kwenye ofisi zao marufuku kabisa kumwona huyo mwana mama Mtendaji,Na ukibahatika kuonana naye anainua pua kama unanuka vile,Na kutoa maelezo mengi yasiyofaa huku tukijua jinsi anvyojinufaisha na fedha hizo zinazotolewa na wafadhili na Wizara husika ,Habari,Utamaduni na Michezo.Sasa swali langu kwenu wadau na hata wizara husika mnajua kwamba kuna ufisadi wa kupindukia kwenye Mfuko huu wa Utamaduni Tanzania??Walionufaika aidha wanajuana na wahusika au ni ndugu marafiki au maswahiba wa kibiashara?
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kuna pesa ngapi kwa sasa?

  Kuna vigezo gani kupata hii pesa?

  Kule kijijini kwangu kuna mila zinapotea: je nifanyeje kupata pesa kwa kupitia huu mfuko?

  Je kuna upendeloe ktk utoaji wa hii pesa?
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...Mfuko wa Utamaduni wanatoa GRANTS kwa wasanii na wazalishaji ktk sekta na tasnia ya sanaa nchini. Ila kwa kutumia mwanya huo baadhi ya watendaji wake wasio waaminifu wamekuwa wakitumia mwanya huo kujinufasiha kinyume na sheria.
  Ninaunga mkono madai yako lakini napenda kuongezea kuwa baadhi pia ya wajumbe wa bodi wanahusika na ubadhilifu huu.
  Ila kikubwa ni kukosekana kwa ushahidi wa wazi ingawa kimazingira ushahidi upo.
  Kibaya zaidi ni kwamba serikali ambayo inalo jukumu la kuchangia ktk mfuko haijawahi kufanya hivyo mpaka wafadhili wakaamua kujiondoa kwani mahela wanayochangia yamekuwa pia yakikwapuliwa na serikali kupitia taasisi zake zinazojihusisha na utamaduni na sanaa....
  Wenye ushahidi mwingine au fununu azimwage hapa ili tujadili kwa kina...
   
 4. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Ni dhahiri kabisa kuwa mahali hapa kuna ubadhirifu wa ruzuku za wadau katika sekta ya Utamaduni wa hali ya juu,Kuna ushahidi wa kutosha jinsi watendaji wa Mfuko walivyojilimbikizia mali tangu mwaka 2000,Zipo kumbukumbu za kutosha kuonyesha ufisadi ambao umekuwa ukifanywa na watendaji,na bodi ya wadhamini.Kwanza kwa kila mjumbe wa bodi amekuwa akipewa ruzuku kila mwaka tangu Mfuko huo uanze kupewa fedha na wafadhili wa Foundation for Civil Society,Finland,Denmark,Sweden na Norway.Pili kila Mwenyekiti wa Bodi akimaliza muda wake naye anapewa kiinua mgongo chake kwa kufadhiliwa mradi wake au gagari yoyote ile alimradi ajichotee pesa kwenye Fuko hili.Hayo yote yamekuwa yanafanyika kiujanja janja na kinara wake ni Katibu Mtendaji ambaye ndiye Mtendaji Mkuu japo muda wake umemalizika lakini yupo yupo tuu kwa kupalilia bodi isione maovu yake aliyoyafanya na anayoyafanya.Kiujumla Mfuko huu umekufa kwa sababu haukuwa endelevu na viongozi wake wamekatia kula hela hizo za ufadhili pasipo kuangalia mbele.Ruzuku ya Serikali ipatayo kiasi cha shilingi Millioni Mia Mbili inayotolewa kila mwaka wa fedha inaishia kuliwa na watendaji hao,Katibu Mtendaji,na Afisa Programu ni mafisadi halisi wa Mfuko wa Utamaduni,Nawasilisha kwenu wadau pamoja na vyombo vya uchunguzi kufuatilia ufisadi uliosemwa na Mdau.
   
Loading...