Magu, Mwanza: Rais Samia ashiriki Tamasha la Utamaduni, Mila na Desturi za Tanzania, atawazwa kuwa Chifu wa Machifu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,547
Rais Samia Suluhu Hassan leo Septemba 8, 2021 atashiriki Tamasha la Utamaduni, Mila na Desturi za Tanzania lililoandaliwa na Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) katika Viwanja vya Redcross - Magu, mkoani Mwanza.



UPDATES
- Katika Viwanja vya Redcross - Magu tukio linaendelea huku Machifu wakihojiwa na burudani mbalimbali kutoka vikundi vya kiutamaduni vikiendelea huku Mgeni Rasmi Rais Samia akisubiriwa kuwasili.

- Rais Samia Suluhu Hassan amewasili leo jijini Mwanza kwa kutumia Helikopta maalum kwa ajili ya kuhudhuria na kufunga Tamasha la utamaduni wa Mtanzania linalohitimishwa leo katika viwanja vya Msalaba-Mwekundu wilayani Magu mkoani Mwanza. Katika tamasha hilo viongozi wa kimila Zaidi ya 150 wamehudhuria.

1631085217448.png

1631085261938.png


Rais Samia amesimama sehemu kadhaa na kuwasalia Wanamwanza ikiwa pamoja na kuwaeleza masuala mbalimbali ya kimaendeleo. Sambamba na hilo Rais Samia ameeleza nia yake ya kuifanya Mwanza kuwa kitovu cha biashara Mwanza.

Zaidi ya hayo, Rais Samia aagiza viongozi wa ngazi mbalimbali kutatua kero na matatizo ya wananchi:

VIDEO: Rais Samia akisalimiana na Wanamwanza


10: 45 Rais Samia amewasili katika viwanja vya Msalaba-Mwekundu wilayani Magu kwa ajili ya kushiriki tukio hili la kiutamaduni kama mgeni rasmi. Apokewa kwa Ngoma ya mamlaka ya kimila.

- Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel akaribishwa ambapo amefanya utambulisho wa viongozi mbalimbali waliopo kwa kuzingatia itifaki. Sambamba na hilo, muwakilishi wa Umoja wa machifu Chifu Aron Mkomangwa afanya utambulisho wa Machifu waliohudhuria na kutoa shukrani kwa Rais.

- Chief Aron Mikomangwa amesoma risala akianza kwa kumpongeza Rais sambamba na kueleza imani ya Machief katika utawala wake. Risala ya Machief imeeleza changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo katika mazingira yao pamoja na kumuomba rais kutekeleza masuala mbalimbali.

Hotuba ya Rais Samia
- Rais aanza kwa kutoa salamu pamoja na shukrani za kualikwa katika tukio hilo.

Kama ilivyosemwa awali kwamba leo mara ya siku ya kwanza kwangu kushiriki tamasha kama hili. Mwaka 2018 nilishiriki kwenye Tamasha la Urithi wa Utamaduni wa Mtanzania lililofanyika jijini Dodoma kumuwakilisha mpendwa wetu Hayati Magufuli wakati ule akijulikana kwa jina la Kilekangano na nakumbuka siku ile na mimi mlinipa jina la Kilelamhina likimaanisha Mama mlezi wa Wanyonge.

Katika Risala iliyosomwa nimesikia leo nimeitwa jina lingine na jina lenyewe ni Hangaya likiwa na maana kwamba ni nyota inayong'ara. Nawashukuru Umoja wa Machifu na Watemi kwa kunipa jina hili zuri sana. Namuomba Mwenyezi Mungu anijaalie niendane na nyota inayong'ara. Kung'ara huku kusiwe kwa kuning'arisha mimi tu, kunisaidie pia ning'arishe nchi yangu Namuomba Mungu anisaidie hilo.

Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema na hapa namnukuu "Utamaduni ni kiini ama roho ya taifa lolote. Taifa lisilo na Utamaduni ni sawa na Mkusanyiko wa watu wasio na roho". Hii ni kwa sababu utamaduni ni miongoni mwa mambo muhimu yenye kutambulisha taifa. Mathalani, lugha ya kiswahili ni moja kati ya tamaduni zetu za Tanzania unaotutambulisha kama taifa. Zaidi ya hapo utamaduni unatusaidia kueleza historia, mila na desturi za jamii ama taifa husika. Aidha, utamadun unasaidia kurithisha maadili kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Kwa kuzingatia hili napenda kuwapongeza viongozi wa Watemi wa kisukuma kwa kuandaa tamasha hili, Zaid ya hapo naamini tamasha hili litahamasisha makabila yote kutangaza mila na desturi zao. Ningependa kusikia mwakati makabila mengine, Machifu wengine wanafanya tamasha katika mkoa fulani na kutuonesha mila na desturi namatamasha haya yakazunguka kila mkoa ili Watanzania tukajua mila na desturi zetu za kila mkoa na pembe za Tanzania.

Katika dunia ya sasa utamaduni ni biashara na pia ni chanzo kikubwa cha mapato hii ni kwa sababu utamaduni kivutio kikubwa cha utalii. Kwa nchi za wenzetu wa Bara la Asia, Japani, Indonesia utamaduni ni kivutio kikubwa cha watalii hata hapa karibuni Ethiopia utamaduni umekuwa kivutio cha utalii nasi hatuna budi kufuata njia hii. Hivyo basi, na sisi tunapaswa kukuza utalii wa kiutamaduni.

Niliwahi kusikia kuwa moja kati ya mambo yanayofanya nchiyetu ipokee idadi ndogo ya watalii na Watalii wengine wanaokuja kutokurudi tena nchini ni kuwepo kwa wigo mdogo wa shughuli za kitalii. Utalii wetu umejikita zaidi kwenye mali asili, wanyama, misitu, fukwe, milima na mambo mengine. Hii inachangia watalii wanaokuja nchini kukaa siku chache. Serikali imejipanga kuhakikisha inapanua wigo wa vivutio vya kitalii ukiwemo utalii wa kitamaduni na katika hili kama mnavyofahamu kwa takribani wiki nzima saizi nimekuwa nikizunguka kuandaa program na filamu ya kutangaza fursa ya vivutio vilivyopo nchini kwetu.

KUHUSU KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIUTAMADUNI
Rais Samia amesema, Serikali imeanzisha mfuko wa maendeleo ya sanaa na utamaduni ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya maendeleo ya nchi yetu mfuko tumeupatia bajeti ya shilingi bilioni 1.5. Aidha, hivi sasa tupo katika mchakato wa kuandaa sera mpya ya utamaduni itakayoendana na mazingira ya sasa ya dunia lakini itakayolinda maadili yetu.

Niagize Wizara katika mchakato wa maandalizi wa sera hii lazima tupate maoni kutoka kwa Watemi na Machifu wetu. Maoni yao yaingizwe katika sera hii ili tuendeleze utamaduni wetu. Ni imani yangu hatua hizi zitasaidia kulinda, kukuza, kuenzi na kuendeleza utamaduni wetu.

Rais Samia avalishwa mavazi ya kimila na kutawazwa kuwa Chief wa machifu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akivalishwa Mavazi ya Kimila kuwa Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Hangaya yani ni Nyota inayong`aa, katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika leo Septemba 8, katika Viwanja vya Redcross Kisesa Magu, mkoani Mwanza.

1631103655137.png

PICHA: Rais Samia akivalishwa Mavazi ya Kimila kuwa Chifu Mkuu wa Machifu wote

1631097734046.png

PICHA: Rais Samia baada ya kutawazwa kuwa Chief Hangaya
 
Huyu mama hana mvuto,mji hauna hamsha hamsha kabisa,zaidi wamekusanywa vijana wa boda boda tangu saa 11 asubuh,wamechoka,njaa,wanasinzia,bendera za ccm zinapepea kwenye ofisi zao tu,mji umepoa utafikiri ni ziara ya Prof Lipumba anakuja kuhutubia

View attachment 1928903
We mwenye mvuto una Nini!zaidi yakuongezwa upenyo kwenye masaburi tu
 
Tanzania in amagaidi.

hamza na Mbowe.
sio kawaida ya watalii kutembelea nchi za kigaidi
 
Hii Royal tour ni ujinga wa dhahiri na dharau kwa wananchi wake.
Hakuna mtalii atakuja kwenye ugaidi
ndugu hata kama una chuki na mtu lakini angalia kuna watu wananufaika na watanufaika na hii kazi mama anafanya wale wanaoongoza watalii idadi ikiongezeka watanufaika sana mmoja mmoja na taifa kwa ujumla wake kila mtu anamapungufu yake lakini kila mtu anamchango kwa taifa hiki anachokifanya kinamanufaa zaidi kuliko hasara unayoiona
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo Septemba 8, 2021 atashiriki Tamasha la Utamaduni, Mila na Desturi za Tanzania lililoandaliwa na Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) katika Viwanja vya Redcross - Magu, mkoani Mwanza.



UPDATES
- Katika Viwanja vya Redcross - Magu tukio linaendelea huku Machifu wakihojiwa na burudani mbalimbali kutoka vikundi vya kiutamaduni vikiendelea huku Mgeni Rasmi Rais Samia akisubiriwa kuwasili.

- Rais Samia amewasili katika uwanja wa ndege Mkoani Mwanza kwa ajili ya kwenda kushiriki Tamasha la Utamaduni na Desturi mkoani humo. Apokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.

Halafu baada ya hapa.
 
Back
Top Bottom