Mfugale amuokoa Kamwelwe kutumbuliwa

Mfugale amuokoa Kamwelwe kutumbuliwa

Mfugale akimuona Mh. Waziri Mkuu ataonyesha heshima kubwa sasa, maana juzi alionyesha kupingana na PM alipoenda mara ya pili alipotaka kujua kwnn Eng wa TANROAD mkoa bado hajaondolewa.

Mfugale ni mtu wa serikalini siku nyingi sijui kwanini alifanya lile kosa. Alitakiwa atelekeze amri ya Waziri Mkuu haraka sana bila shuruti maana PM hua anatumwa na rais. Naamini hatarudia tena
 
Mkuu @paskal hivi leo nikuulize mbele ya hadhara ya Jf
Wewe ni mwanaharakati wa ccm au chadema au neutral maana ukija kwa chadema huwa unaponda sana ccm na sera zake,ukija tena chadema huwa unawaponda...
Nami nitachangia kukujibu, hata kama yeye hajakupa jibu.

Ni wapi kaonyesha uharakati kwa CCM au CHADEMA?

Andiko lake hilo liko wazi; na maandiko yake mengi hayatofautiani na hilo hapo juu.

Yeye ni mwanaharakati wa mtu aitwaye Magufuli, ambaye ni rais wa Tanzania. Kwao ni Kanda ya Ziwa.

Tafuta maandiko yake yote, utauona ukweli huo.
 
Hizi taarifa ni too much sasa wakuu. Hivi nani mwenye akili zake timamu anajali haya mambo ya kutumbuana? Ishachuja. Kama ni daraja au barabara mbovu warekebishe wasafiri waendelea na safari zao. C'mon people! Dramas za nini? Mbona awamu nyingine haya mambo hayakuwepo! Kila mtu afanye kazi zake kimya kimya aisee, wanaoshindwa waadhibiane huko huko kimya kimya, embu tuache ku-dramatize mambo kitoto. Yaani siku hizi ni mavideo clips tu, ni kwamba watu hawawezi kufanya kazi bila makamera! Tuwaambie watu, "grow up, achana na micromanagement na macamera".
Give us a break! Khah!
 
Mkuu paskal hivi leo nikuulize mbele ya hadhara ya Jf
Wewe ni mwanaharakati wa ccm au chadema au neutral maana ukija kwa chadema huwa unaponda sana ccm na sera zake,ukija tena chadema huwa unawaponda...

Wewe ni mtu gani?
Mwana siasa mlengwa gani?
Sitaki ku tag mada zako hapa ukinilazim nifungue uzi nitafungua ila hebu tufahamishe hapa mkuu..
Naheshim maoni yako
Swali lako siyo sahihi kutaka kujua mchangiaji Paskali yuko chama gani kwa kuwa kuna siku anaiponda CCM na siku nyingine anaiponda CHADEMA. Hivyo ndivyo mchangiaji mzuri anapaswa kuwa: unatafakari jambo na kutoa maoni yako kufuatana na vipi unaona mambo yanapaswa kwenda. Siyo kwa kuwa uko CHADEMA basi kila kitu kinachofanywa na CHADEMA ni kizuri na kila kitu kinachofanywa na CCM ni kibaya. Swali lako limedhihirisha kabisa kwa nini Rais Magufuli analaumiwa kila kukicha. Najiuliza hivi ni kweli hakuna kitu kizuri alichofanya mtu huyu tangu aingie madarakani miaka minne iliyopita? Swali lako limenipa jibu kwamba analaumiwa kwa kuwa tu yuko chama tofauti na mchangiaji; siyo kwa sababu amefanya kitu kibaya. Tubadilike Watanzania: tukosoe panapokuwa na mabaya na tuunge mkono panapokuwa na mazuri.
 
Mkuu daraja linalounganisha mikoa ya Morogoro na Dodoma linawezaje kupitisha mizigo inayokwenda Malawi na Zambia ?
Bidhaa zinapitia bungeni kusainiwa na waheshimiwa.
Zambia na Malawi kumbe zinapitia Dodoma ndio najua leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa miaka mingi walaji wakubwa wa dagaa Mwanza ni Congo, Zambia na Malawi. Madereva wengi wa maroli walipendelea kupitia njia ya Mwanza-Dodoma-Moro-Mbeya kuliko kupitia ya Dodoma-Iringa kwa kuogopa usumbufu wa Nyang'oro.
Vitunguu vya Singida vinauzwa sana kwenye nchi hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali lako siyo sahihi kutaka kujua mchangiaji Paskali yuko chama gani kwa kuwa kuna siku anaiponda CCM na siku nyingine anaiponda CHADEMA. Hivyo ndivyo mchangiaji mzuri anapaswa kuwa: unatafakari jambo na kutoa maoni yako kufuatana na vipi unaona mambo yanapaswa kwenda. Siyo kwa kuwa uko CHADEMA basi kila kitu kinachofanywa na CHADEMA ni kizuri na kila kitu kinachofanywa na CCM ni kibaya. Swali lako limedhihirisha kabisa kwa nini Rais Magufuli analaumiwa kila kukicha. Najiuliza hivi ni kweli hakuna kitu kizuri alichofanya mtu huyu tangu aingie madarakani miaka minne iliyopita? Swali lako limenipa jibu kwamba analaumiwa kwa kuwa tu yuko chama tofauti na mchangiaji; siyo kwa sababu amefanya kitu kibaya. Tubadilike Watanzania: tukosoe panapokuwa na mabaya na tuunge mkono panapokuwa na mazuri.
Mkuu Ng'wanamalundi, naunga mkono hoja, na hii ndio kitu kinachoitwa kuwa mkweli daima, rais Magufuli ni binadamu na sio malaika, no one is perfect, anaweza kuwa na mapungufu yake ya kibinaadamu kama binadamu wengine wote, hivyo pamoja na mabaya yake yote, pia ana mazuri yake, tumkosoe kwa mabaya yake lakini kwenye mazuri, tumpongeze.

Tusilalamike tuu, kulaumu na kulaani kila kitu, kwenye mazuri tupongeze! Rais Magufuli is changing for the better!.

Tusikalie kumlaumu tu Rais Magufuli na Serikali yake wanapofanya mabaya, kwenye mazuri, pia tupongeze!.

Magufuli is Doing Good For This Nation, Tumuassess kwa Positive Attitude, Kwa Mazuri Tumpongeze, Tumuunge Mkono Kumsupport, lakini kwa Mabaya Tumkosoe

Magufuli is Getting Better and Better, He is Changing for The Better!. Hongera Sana!.

P
 
Mkuu daraja linalounganisha mikoa ya Morogoro na Dodoma linawezaje kupitisha mizigo inayokwenda Malawi na Zambia ?
Dah... nadhani alimaananisha sangara na sato....Ni samaki pendwa katika nchi tajwa

Sent using Beretta ARX 160
 
Mkuu paskal hivi leo nikuulize mbele ya hadhara ya Jf
Wewe ni mwanaharakati wa ccm au chadema au neutral maana ukija kwa chadema huwa unaponda sana ccm na sera zake,ukija tena chadema huwa unawaponda...

Wewe ni mtu gani?
Mwana siasa mlengwa gani?
Sitaki ku tag mada zako hapa ukinilazim nifungue uzi nitafungua ila hebu tufahamishe hapa mkuu..
Naheshim maoni yako
Ungejua Tanzania kuna zaidi ya CCM na CDM swali lako lisingekuwa "dichotomous" na huenda usingetatizika kutambua itikadi ya mtoa mada.
 
Mtu anayetoka dar kwenda iringa mbeya akipita dodoma anafika haraka kuliko mtu anayepitia mikumi nadhani umenielewa...

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio kweli, nitatumia vigezo vitatu.

1. Umbali wa barabara (Driving distance);

Umbali (wa barabara) toka Morogoro hadi Dodoma ni kilometa 310 na umbali (wa barabara) toka Dodoma hadi Iringa ni Kilometa 261, Ukijumlisha hizi ni kilometa 571 tayari.
Wakati umbali (wa barabara) toka Morogoro hadi Iringa (kupitia Mikumi) ni kilometa 312.

Kuna utofauti wa kilometa 259 tayari, kwa maana ya kwamba anayepita Dodoma atasafiri kilometa 259 za ziada. Ni kivipi huyu anawahi kufika ukilinganisha na mwenzake anayepita Mikumi ?
Au unamaanisha kwamba anayepita Dodoma anakua na gari wakati huyu wa Mikumi anatumia baiskeli ?

2. Miinuko na Makwazo:
Kwenye njia ya Mikumi utakumbana na Kitonga pamoja na kilometa 50 za hifadhi ya wanyama Mikumi ambazo unatakiwa uendeshe gari kwa mwendo usiozidi 50 KPH.
Kwenye njia ya Dodoma utakutana na Nyang'olo ambayo inatosha kabisa ku ''compensate'' muda unaopoteza Mikumi na Kitonga.

3. Personal experience:
Nimesafiri toka Mbeya kwenda Dodoma kwa kutumia njia zote mbili (Kwa basi). Yafuatayo ndio matokeo ya safari hizo mbili.

Mbeya-Iringa-Dodoma ni safari ya Masaa takribani TISA na nauli yake ni 29,000

Mbeya-Iringa-Morogoro-Dodoma (kwa sasa hii route haipo lakini, nilisafiri 2013 wakati huo hiyo barabara nyingine ilikua haijakamilika) ni safari ya masaa KUMI NA TATU na nauli yake (by then) ilikua ni 41,000.
Kwa hoja hizo tatu hapo juu naomba nikupinge.
 
Magufuli angekuwa kituko cha ajabu kama angemtumbua Waziri Kamwele halafu amuache Mfugale. Na wala sioni ni kwa jinsi gani Mfugale kamwokoa Kamwele. Wanaosimamia ujenzi wa hizi barabara ni TANROADS, sasa waziri angekuwa na kosa gani? Hata kama TANROADS iko chini ya Ujenzi lakini kwa kiasi kikubwa sana inajitegemea. Waajiriwa wake sio wa wizara kwa hiyo hawapo chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Waziri wa Ujenzi
TANROADS ni taasisi iliyo chini ya hiyo wizara husika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilichotokea muda mfupi katika ukaguzi wa rais kwenye kalavati la Kayegeya linalounganisha barabara ya Morogoro na Dodoma ambalo hivi siku za karibuni limekwenda na maji hivyo kupelekea serikali kuagiza kutengenezwa daraja eneo hilo.

Kwa kweli usumbufu kwa wasafiri na wasafarishaji wa mizigo umekuwa ni mkubwa sana ukizingatia hiyo ni barabara kuu inayopitisha abiria na mizigo mingi ya ndani na nje ya nchi kwa majirani zetu kama vile Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi n.k

Leo Mh. Rais Magufuli akipita maeneo hayo amekagua ujenzi unaoendelea hapo wa daraja ambalo nalo lilienda na maji. Rais amekasirishwa sana na maelezo aliyokuwa anapewa na watendaji wake akiwemo Waziri wa ujenzi na uchukuzi ambaye amekiri makosa na kuomba msamaha wa wazi kwa rais.

Kufuatia hali ya watendaji wale wa Wizara na TANROADS kutokuwa na majibu ya kumridhisha rais, binafsi nimemuona rais akitafakari kwa kina kuona ni hatua gani stahiki ambayo angeweza kuchukua dhidi ya watendaji hao.

Ametafakari kwa muda alipokosa cha kuamua ikabidi auze mchezo kwa wananchi waamue nini afanye ambapo wananchi wamesema awasamehe tu, ila mheshimiwa rais ameagiza kusimamishwa kazi wahandisi takribani 13 wa TANROADS na uchunguzi ufanyike dhidi yao.

Kwa muonekano aliokuwa nao rais alitaka kumtumbua waziri na safu ya maofisa wa TANROADS hasa meneja wa mkoa wa Morogoro lakini akaona anaweza kumtumbua waziri na akamuacha CE wa TANROADS ambaye yeye mwenyewe amekiri laivu ni kutokana na kuguswa na kazi zake anazozifanya zinamkosha.

Kwa Leo ni hilo tu limemuokoa Eng. Kamwelwe kutumbuliwa lakini pia tukumbuke mahusiano makubwa yaliyopo kati ya boss huyo wa TANROADS na Rais pasi na shaka ndio yameathiri maamuzi ya mheshimiwa rais hivyo kuishia kutoa onyo kwa Mfugale na Kamwelwe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nilichojifunza ni kwamba mfugale huwa hana hofu yoyote kwa bwana gywe
 
Kwa iyo mizigo ya kutoka mwanza haiwez pita pale ikaenda zambia?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana, labda kama hiyo mizigo iwe inatakiwa kufanyiwa jambo fulani mkoani Morogoro, mfano kupungiwa mikono na wakazi wa Msamvu, kusainiwa na wahadhiri wa SUA na Mzumbe n.k
Kwa maneno mengine huo mzigo uwe ''unaenda Morogoro halafu baadae Zambia''.
 
Back
Top Bottom