Mfugale amuokoa Kamwelwe kutumbuliwa

Mfugale amuokoa Kamwelwe kutumbuliwa

Kwa jinsi mh Rais alivyo kuwa amekasirishwa Na uzembe mkubwa uliojitokeza ktk ujenzi Na ukarabati wa daraja hilo, inapaswa WAZIRI kamwelo Na Mfugale wajitathimini wenyewe.
Sio kila mara msubiri kufukuzwa KAZI wakati mwengine unaweza kujiuzulu mwenyewe kuonyesha kuwajibika Kwa matendo yako, utamaduni Kwa kujiuzulu mwenyewe naona watanzania wengi hatuna huo utamaduni lkn ni utamaduni mzuri sana.
Umajitathimini mwenyewe matendo yako unaachia ngazi bila kumsumbua Rais akufukuze..
Hata hivyo wote wawili nawaona wapo kwenye mtego
 
Kwa miaka mingi walaji wakubwa wa dagaa Mwanza ni Congo, Zambia na Malawi. Madereva wengi wa maroli walipendelea kupitia njia ya Mwanza-Dodoma-Moro-Mbeya kuliko kupitia ya Dodoma-Iringa kwa kuogopa usumbufu wa Nyang'oro.
Vitunguu vya Singida vinauzwa sana kwenye nchi hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu ni usumbufu upi wa Nyang'oro (Nyang'olo) wanaouogopa hao madereva wakati kule ni lami na barabara ni nzuri kabisa ? Au unazungumzia nyakati zile (kabla ya 2014) wakati barabara ya Mtera haijakamilika!
Malori ya mbao na miti toka Iringa yanapita njia ya Mtera, Mabasi yanapita Mtera, what is so special with malori yenye shehena ya dagaa au kitunguu na hata yapite Morogoro ?
NB: Ukitoka Dodoma na ukapita Morogoro (unapokwenda Iringa) hasa kwa lori si tu unaongeza Kilometa zaidi ya 250 kwenye safari yako, bali pia unajiongezea idadi ya MIZANI njiani.
Nimeshangaa sana.
 
Ivi hakjna mtu Tanzania anaweza kuwa CEO wa tanroad?

Hakuna vijana walioiva kwenye engineering, project management, business managqment etc?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inafanya utalii wa ndani... Inapita Dodoma, then Mtera Iringa. Usihofu nimeandika kilevi tu....
Hahahaaa.... ukizingatia watalii toka nje wamepungua kutokana na Corona, acha tu mizigo italii na kuongeza pato la taifa.
 
Mkuu ni usumbufu upi wa Nyang'oro (Nyang'olo) wanaouogopa hao madereva wakati kule ni lami na barabara ni nzuri kabisa ? Au unazungumzia nyakati zile (kabla ya 2014) wakati barabara ya Mtera haijakamilika!
Malori ya mbao na miti toka Iringa yanapita njia ya Mtera, Mabasi yanapita Mtera, what is so special with malori yenye shehena ya dagaa au kitunguu na hata yapite Morogoro ?
NB: Ukitoka Dodoma na ukapita Morogoro (unapokwenda Iringa) hasa kwa lori si tu unaongeza Kilometa zaidi ya 250 kwenye safari yako, bali pia unajiongezea idadi ya MIZANI njiani.
Nimeshangaa sana.
Nimeandika "walipendelea kupita" maana yake ni kipindi hicho. Muhimu ni kujua kuwa bidhaa zinazo toka kanda ya kati/ziwa kwenda nchi za kusini zipo nyingi, ukiachana na vitunguu na samaki kuna mahindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilichotokea muda mfupi katika ukaguzi wa rais kwenye kalavati la Kayegeya linalounganisha barabara ya Morogoro na Dodoma ambalo hivi siku za karibuni limekwenda na maji hivyo kupelekea serikali kuagiza kutengenezwa daraja eneo hilo.

Kwa kweli usumbufu kwa wasafiri na wasafarishaji wa mizigo umekuwa ni mkubwa sana ukizingatia hiyo ni barabara kuu inayopitisha abiria na mizigo mingi ya ndani na nje ya nchi kwa majirani zetu kama vile Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi n.k

Leo Mh. Rais Magufuli akipita maeneo hayo amekagua ujenzi unaoendelea hapo wa daraja ambalo nalo lilienda na maji. Rais amekasirishwa sana na maelezo aliyokuwa anapewa na watendaji wake akiwemo Waziri wa ujenzi na uchukuzi ambaye amekiri makosa na kuomba msamaha wa wazi kwa rais.

Kufuatia hali ya watendaji wale wa Wizara na TANROADS kutokuwa na majibu ya kumridhisha rais, binafsi nimemuona rais akitafakari kwa kina kuona ni hatua gani stahiki ambayo angeweza kuchukua dhidi ya watendaji hao.

Ametafakari kwa muda alipokosa cha kuamua ikabidi auze mchezo kwa wananchi waamue nini afanye ambapo wananchi wamesema awasamehe tu, ila mheshimiwa rais ameagiza kusimamishwa kazi wahandisi takribani 13 wa TANROADS na uchunguzi ufanyike dhidi yao.

Kwa muonekano aliokuwa nao rais alitaka kumtumbua waziri na safu ya maofisa wa TANROADS hasa meneja wa mkoa wa Morogoro lakini akaona anaweza kumtumbua waziri na akamuacha CE wa TANROADS ambaye yeye mwenyewe amekiri laivu ni kutokana na kuguswa na kazi zake anazozifanya zinamkosha.

Kwa Leo ni hilo tu limemuokoa Eng. Kamwelwe kutumbuliwa lakini pia tukumbuke mahusiano makubwa yaliyopo kati ya boss huyo wa TANROADS na Rais pasi na shaka ndio yameathiri maamuzi ya mheshimiwa rais hivyo kuishia kutoa onyo kwa Mfugale na Kamwelwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Salehee jamani pamoja na unene wake Mh Tafadhali msamehe huyu jamaa inaonekana shule IPO na jiamini sana msamehe mkuu,kijana huyu anamadini kichwani kwa muonekano
 
Mimi ninakunwa sana na kasi ya Mhe. Rais LAKINI yale maneno aliyotumia mbele ya wateule wake wa kumwita mmoja wao pumbavu siyo maneno ya staha. Pia kumdhalilisha Mhe. Waziri wa Ujenzi mbele ya Umma siyo kitendo cha kiungwana. Ilifikia wakati Mhe. Waziri akatamka kuwa nisamehe Mhe. Rais nimekosa. Yale maneno angetakiwa kuyatamka faragha wakiwa wawili aidha kule Ikulu na siyo mbele ya watu. Dunia hii kila mtu anastahili heshima.
 
Mhandisi alitoa jibu la wazi kabisa kwamba Yule ni bridge Engineer pekee mzoefu waliyenae
Mfugale akimuona Mh. Waziri Mkuu ataonyesha heshima kubwa sasa, maana juzi alionyesha kupingana na PM alipoenda mara ya pili alipotaka kujua kwnn Eng wa TANROAD mkoa bado hajaondolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
+1
Ndo mana media kama CNN huwa zinakiwa na uandishi wa bobezi katika karibu kila sekta, ukija afya utakuta Sanjay gupta , politics akina Richard Roth, nk hii imesaidia sana wanaporiport kitu wanakuwa pricise kwa kila detail
Daraja la kiyegeya likaunganishe nchi ya Zambia na Malawi, ??? Hadi nimechoka!!
Mkuu daraja linalounganisha mikoa ya Morogoro na Dodoma linawezaje kupitisha mizigo inayokwenda Malawi na Zambia ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom