Real Patriotist
JF-Expert Member
- Feb 6, 2016
- 296
- 698
Kilichotokea muda mfupi katika ukaguzi wa rais kwenye kalavati la Kayegeya linalounganisha barabara ya Morogoro na Dodoma ambalo hivi siku za karibuni limekwenda na maji hivyo kupelekea serikali kuagiza kutengenezwa daraja eneo hilo.
Kwa kweli usumbufu kwa wasafiri na wasafarishaji wa mizigo umekuwa ni mkubwa sana ukizingatia hiyo ni barabara kuu inayopitisha abiria na mizigo mingi ya ndani na nje ya nchi kwa majirani zetu kama vile Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi n.k
Leo Mh. Rais Magufuli akipita maeneo hayo amekagua ujenzi unaoendelea hapo wa daraja ambalo nalo lilienda na maji. Rais amekasirishwa sana na maelezo aliyokuwa anapewa na watendaji wake akiwemo Waziri wa ujenzi na uchukuzi ambaye amekiri makosa na kuomba msamaha wa wazi kwa rais.
Kufuatia hali ya watendaji wale wa Wizara na TANROADS kutokuwa na majibu ya kumridhisha rais, binafsi nimemuona rais akitafakari kwa kina kuona ni hatua gani stahiki ambayo angeweza kuchukua dhidi ya watendaji hao.
Ametafakari kwa muda alipokosa cha kuamua ikabidi auze mchezo kwa wananchi waamue nini afanye ambapo wananchi wamesema awasamehe tu, ila mheshimiwa rais ameagiza kusimamishwa kazi wahandisi takribani 13 wa TANROADS na uchunguzi ufanyike dhidi yao.
Kwa muonekano aliokuwa nao rais alitaka kumtumbua waziri na safu ya maofisa wa TANROADS hasa meneja wa mkoa wa Morogoro lakini akaona anaweza kumtumbua waziri na akamuacha CE wa TANROADS ambaye yeye mwenyewe amekiri laivu ni kutokana na kuguswa na kazi zake anazozifanya zinamkosha.
Kwa Leo ni hilo tu limemuokoa Eng. Kamwelwe kutumbuliwa lakini pia tukumbuke mahusiano makubwa yaliyopo kati ya boss huyo wa TANROADS na Rais pasi na shaka ndio yameathiri maamuzi ya mheshimiwa rais hivyo kuishia kutoa onyo kwa Mfugale na Kamwelwe.
Sent using Jamii Forums mobile app