Mfuasi wa CHADEMA mbaroni.

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, linamshikilia na kumhoji anayedaiwa kuwa ni mfuasi wa Chadema, Prosper Mfinanga (40), mkazi wa Kijenge kwa tuhuma za kutembea na bango lenye maandishi yanayodaiwa kuwa ya uchochezi na uvunjifu wa amani.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alisema jeshi hilo linamshikilia mfuasi huyo tangu Juni 5, mwaka huu.


Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na bango hilo katika maeneo ya Soko Kuu majira ya saa 11:30 jioni, huku akilitembeza barabarani.


Aidha, Mpwapwa alisema bango hilo lilikuwa na maandishi katika pande mbili, ambapo upande wa kwanza ulisomeka “Heri Ukimwi uendelee kuliko CCM iendelee kutawala.”


Mpwapwa alisema upande wa pili ulisomeka kama “Kumkamata waziri kivuli ni kuvunja sheria za mabunge ya Jumuiya ya Madola” huku akisisitiza kuwa maandishi hayo yanaashiria uchochezi ndani ya jamii.


Alisema jeshi hilo kwa sasa linamhoji mtuhumiwa huyo, nia na madhumuni ya kuwa na bango hilo na kujua endapo maandishi hayo, aliandika mwenyewe au aliandikiwa na watu wengine.


Alisema endapo mtuhumiwa huyo atathibitika alihusika na tuhuma zinazomkabili, atafikishwa mahakamani.

Source: IPPMEDIA
 
hizo ni proganda za wafuasi wa chadema mbona Nape hakukamatwa apotoa kauli za uchochezi na ukabila kwa kusema 'chadema ni chama cha wachaga na yeye si mchaga' kwa hiyo alitaka kuuaminisha umma kuwa ndani ccm hakuna wananchi wa kabila la wachaga?
 
Kwa nini sasa wamekaa nae mpaka leo??kuna sheria ya kumuweka mtu sero for 3 days??inabidi wamuachie sivyo wampeleke mahakamani,wasilete ujinga wao hao vilaza.
 
Polisi ni vilaza ndiyo mana wengi wao wameishia darasa la pili.
 
Polisi wanatumika kisiasa, vibaka mtaani akipelekwa polisi usiku kesho asubuhi unamkuta mtaani, huyo jamaa kutembea na bango tu lupango siku tatu...
 
Hivi wanatudhihilishia ujinga wao wa kisheria ama la? Toka juni 5 si haki.
 
Jamani someni gazeti la leo la mwanahalisi mtapata majibu ya kwanini wanachadema wanakamatwa kamatwa na serikali ya magamba.
 
Polisi ni vilaza ndiyo mana wengi wao wameishia darasa la pili.

Mkuu kabisa police hawana elimu yoyote wanaokotwa tu mtaani na kufanyishwa mazoezi, sasa hapo tunategemea nini kutoka kwao???
 
tuwe makini sana tusije kuishia kwenye kila mwenye issues zake ajiassociate na chadema, na kila jambazi mwishowe atakua chadema

hakuna haja ya mabango kutwa
hakuna hata ya kulalama kutwa
hakuna haja ya uassociate uhalifu na chadema kila wakati

we are heading south
 
Jamani someni gazeti la leo la mwanahalisi mtapata majibu ya kwanini wanachadema wanakamatwa kamatwa na serikali ya magamba.
Mkuu naomba utueleze kwa kifupi gazeti hilo limesema nini kwa sababu wengine hatuwezi kulipata gazeti hilo kwa sasa.
 
Tatizo lililopo kwa polisi ni la kimfumo zaid unategemea nini kwa IGP KUCHAGULIWA NA RAIS AND THE LIKE?
 
kuna sababu ingine au ni hayo maandishi tu? hao polisi wanatumia akili au makalio?
 
chadema sasa kuna haja ya kuimarisha idara ya sheria na haki za binadamu..

ili tuweze kuendana na upepo wa sasa....

chadema arusha....tuklifanyie kazi sasa
 
Hata wakikamata kila siku haitasaidia kuondoa ukweli wa mambo vinginevyo waongeze magereza ya kutosha kutuweka CDM sote

polisi machangudoa tu hawa vinashabikia magamba ingali mama zao mtaani na vijijini wanachapika na maisha magumu na kulala njaa
 
Mwanahalisi ya leo inasema...
"...CCM wapanga kuhujumu CHADEMA...mkakati unalenga kuzuia viongozi wa Chadema kufanya kazi za kisiasa na hata za ubunge, kwa kuwapotezea muda ktk malumbano na polisi, serikali na mahakama...inaendelea
...CCM na serikali yake wamepanga kuwakamata na kuwafungulia kesi viongozi wakuu wa chama hicho ili kuzima moto uliowashwa na chama hicho mjini na vijijini...."

Mbona NAPE anatukana watu hovyo hovyo halafu hashikwi na polisi kwa kosa la kutukana na ubaguzi?
 
Back
Top Bottom