Mfanyabishara Paulo Mashauri, anajua sana aisee

BIG Africa

Member
Oct 15, 2022
84
116
Habari zenu.Naanza mwaka 2018 ndiyo ulikuwa ni mwaka wangu wa kwanza kumjua mfanyabiashara au mjasiriamali ambaye anaitwa Paulo Mashauri.

Ilikuwa katika kituo cha redio cha Times FM kipindi kilikuwa kinaitwa "Mambo ya fedha" ambacho kilikuwa kinarushwa kila jumapili kuanzia saa nane mchana.Kiufupi jamaa alitokea kunivutia sana kutokana na yeye kuonekana kuwa mbobezi katika sekta ya biashara au ujasiriamali.Baada ya hapo nikaanza kuwa namfuatilia kwenye mitandao ya kijamii hasa Facebook ambapo pia alikuwa anaandika madini ya kutosha kuhusu biashara.Kiufupi jamaa alinivutia sana.

Baada ya hapo nikaanza kufuatilia huyu jamaa anafanya biashara gani?.Hapo ndipo nilichoka.Kwanini? Nilichokuja kugundua jamaa anafanya biashara nyingi zaidi ya nane.Mimi nilijua biashara za mshikaji baada ya kuwa nasoma sana post zake Facebook.

Mfano baadhi ya biashara ambazo mshikaji anafanya ni (Biashara ya magari,biashara ya kuku,biashara ya mashine ya kushona masweta)nk.Ukiachana na biashara hizo pia jamaa anaigiza movie,anaimba nyimbo hasa za dini(gospal songs) na anamiliki kampuni mbalimbali kama HiTech,Master Class Worldwide,na kampuni moja ya ulinzi jina silikumbuki.

Ukiachana na biashara ambazo anazifanya pia jamaa amefanya kazi kwa muda mrefu kwa ukaribu sana na sekta binafsi na sekta za umma(Mfano TPSF,TCCIA,TIC,)nk.Ukitaka kukubaliana na mimi ni kwamba huyu jamaa huenda Mimi nikichelewa kumjua lakini naamini hata humu jamii forums kuna watu wengi walimjua kabla yangu na wakambua uwezo wake.

Nimesema hivyo kwasababu hata humu jf kuna badhi ya threads ambazo nimewahi kukutana nazo zinazomhusu jamaa ambazo nyingi ni positive.Mfano kuna thread ya jamaa kuhusu tatizo la nchi kuhusu HUMAN RESOURCE hotuba ambayo aliitoa jijini Arusha mwaka 2011.Nilijaribu kuitafuta hiyo video YouTube nikamsikiza jamaa aliongea mambo muhimu sana ambayo ni nadra kuyasikia kwa watu wengine.Ni madini tupu.Huyo ndiyo Paulo.R.K.Mashauri.
 
Katika watu wanaolezea practical about business ni huyo jamaa..yuko so inspired kwa watu..ila mapungufu yake ni mtu anayekata tamaa sana na kushika biashara au project fulani kisha Akaacha....kuna project nyingi alianzisha kwa moto kweli mara anapotea..kikubwa aongeze umakini na kuacha kuruka ruka....huwezi fanya kila biashara inayokujia na kuanza na kuacha
 
Hivi huyo jamaa si ndio yule kwenye kila post za facebook na instagram anachomekea comment yenye tangazo anaanza kutokana na mada kwa kusema"Mimi nashauri huyo mtoto kama una mtaji wa kuanzia laki 3 nione utengeneze pesa"
 
Huko Facebook anaitwaje maana naona umeshindwa kubandika hapa madini uliyosoma kwenye posts zake
 
Hivi huyo jamaa si ndio yule kwenye kila post za facebook na instagram anachomekea comment yenye tangazo anaanza kutokana na mada kwa kusema"Mimi nashauri huyo mtoto kama una mtaji wa kuanzia laki 3 nione utengeneze pesa"
Achana na uyo Tapeli
Sio anaemzungumzia mtoa mada kabisaaaa..Huyo wa 'Mtaji wa laki mbili' ni matapeli kama walivyo matapeli wengine wa kimtandao
 
Mungu hakupi vyotee Jamaa anaonesha amepungukiwa na Msimamoo. Mambo mengi sana anataka aende nayooo...
 
Back
Top Bottom