Mfanyabiashara wa madini, Mathias Manga apigwa risasi

Mfanyabiashara wa madini, Mathias Manga apigwa risasi

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
attachment.php

Wakuu salama?

Hatimaye siasa za Tanzania zachukuwa sura mpya.

Habari nilizozipata muda huu ni kwamba Mathias Manga, bilionea wa jiji la Arusha, na Diwani wa Kata ya Mlangarini Arumeru Magharibi (CCM), amepigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati akielekea nyumbani.


Imeelezwa kuwa watu hao walifanya jitihada zote lengo ilikuwa ni kumteka lakini mfanyabiashara huyo alijitetea mpaka akajitoa ndio wakaamua kumpiga risasi.

Niko nafuatilia kwa karibu kujuwa soon nitawapa updates japo kwa habari za haraka haraka wanasema kuna siasa ndani yake.

======================

Updates



Amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Selian iliyopo mkoani humo, Waandishi wa habari waliopo Arusha ambao wamezuiwa kuingia katika chumba alicholazwa wamesema amepigwa risasi katika eneo la Mgongoni (Hajaumia sana).
 
Hizi habari kama za kweli Lowassa atakuwa amepata pigo kubwa sana.
 
Na nilisikia za chini alitaka ubunge au kaghairi team mamvi, few years ago alishawahi pigwa tanzanite za milioni 200 ofisini kwake sijui kesi iliishia vipi.
 
Naona system inafanya jitihada zote kuzuiya mafuriko ya El, hapa bila kumumunya maneno wazee wa kungoa kucha wamehusika, huyu jamaa amekuwa mstari wa mbele sana kumsapoti Lowassa, team Membe mko wapi?? Mmeamuwa kupita shortcut baada ya kuzidiwa na mamvi?
 
sina hakika na matumizi ya neno ""BILLIONEA"" kwa Arusha....mwenye uwezo wa kuwa na gari zuri, bia kila siku, anafanya shughuli zake mbuguni, basi ni ""BILLIONEA"".

Nimeamini kweli wewe nikiereere, issue hapa siyo ubilionea issue ni mtu kupigwa risasi
 
Wana Jf kuna tetesi kuwa Mfanyabiashara wa Madini jijini Arusha Bilionea Matias Manga Amepigwa Risasi na watu wasiojulikana Mjini Arusha
Mwenye Taarifa zaidi atujuze hapa JF ni kisima cha habari.
NB: Hizi bado ni tetesi.
 
Chadema wamehusika hapo,si alikuwa anampinga Lema

We ni mbululazi kweli wewe, hapa CHADEMA wanahusikaje?? CCM mnauwana wenyewe kwa wenyewe, Vijana wa membe naona mnasingizia CHADEMA baada ya nyie kumaliza kazi, Membe kabanwa na Lowassa hana pa kupumulia
 
Back
Top Bottom